DOKEZO GE2025 Kashfa kubwa mchujo wa Ubunge Mwanga. Kama wewe sio Muislam hupiti. Sikiliza audio iliyovuja

DOKEZO GE2025 Kashfa kubwa mchujo wa Ubunge Mwanga. Kama wewe sio Muislam hupiti. Sikiliza audio iliyovuja

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mchakato wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuwapata wagombea wa ubunge na udiwani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 umeelezwa kuingia katika hali ya sintofahamu kufuatia tuhuma nzito dhidi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Ibrahim Mzava.

Mzava anatuhumiwa na wanachama wenzake kuendesha mchakato huo kwa misingi ya ubaguzi wa kidini na pia kuomba fedha kutoka kwa baadhi ya watia nia wa ubunge katika Jimbo la Mwanga

Sauti inayodaiwa kuwa ya Mzava imevuja na kusambaa mitandaoni, ikimuonesha akizungumza na mmoja wa watia nia huku wakisisitiza umuhimu wa nafasi ya ubunge kushikiliwa na mtu kutoka dini ya Kiislamu

Katika sauti hiyo, mtu anayedaiwa kuwa mwenyekiti huyo anasikika akisema: "Tutakuja ulizwa siku ya kiama, tutaulizwa. Hivyo tuhakikishe tunatafuta Muislamu safi wa kukaa hapo kwenye kiti"

Mbali na kauli hiyo, kuna kauli inayodaiwa kumhusisha Mzava akizungumza na mtia nia mwingine kuhusu mahitaji ya fedha, hali iliyozua tuhuma za kuomba au kupokea rushwa

"Wewe nitumie tu kwenye namba hii…tena nilikuwa na hali ngumu sana jina Ibrahim Mzava…Kuna mahali fulani tunakwenda na Sheikh nilikuwa ninakutafuta ili utusaidie mafuta…tulikuwa na vikao vya kata, Sheikh alikuwa alikuwa anakwenda kuonana na Wajumbe Mkutano Mkuu wa kila kata, sasa tulikuwa tunahangaika mafuta, nimekupigia tangu juzi…”, alisikika akiongea anayeelezwa kuwa Mzava baada ya anayeongea naye (mtia nia) kumwambia kuwa angemtumia Shilingi laki moja na nusu au mbili

Hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la Nipashe la Julai 15, 2025, Mzava alikana kuhusika moja kwa moja na sauti hiyo alipopigiwa simu akisema: “Mimi si Mkurugenzi wa Uchaguzi. Hayo masuala aulizwe Mkurugenzi wa Uchaguzi”, kisha akakata simu na hakupatikana tena kwa mawasiliano ya ziada

Wakuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wameendelea na uchunguzi kuhusu tuhuma mbalimbali zilizowasilishwa na wagombea, wajumbe na wafuasi katika mchakato wa kura za maoni sehemu mbalimbali, wakieleza kuwa macho hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa October 2025

ruuuu.png


Chanzo: Jambo Tv
 
Kwani wanaolalamika huku mitandaoni na kuleta audio clips za kuchonganisha ni Sisi Makobazi a.k.a Vibaraghashia (kamq mnavyotuita) ama nyie Wagalatia a.k.a Wanaswara a.k.a Wala Nguruwe?
Wasabato na Judaism hawali nguruwe wala kufuga!
 
Vipo vifaa vingi tu vya kufanya hivyo. Kumbuka enzi zile maongezi ya baadhi ya viongozi yaiivyonaswa na kupelekea kudondoshwa kisiasa k.m. Nape.
BIla shaka hiyo ilitokea kipindi kile TCRA walipokuwa hawajawataka makampuni ya simu kutoruhusu mtu kumrekodi mwenzie pasipo yeye kujua kuwa anarekodiwa. Kama sikosei hiyo ilianza katikati ya 2023.
 
Smartphone nyingi siku hizi zinaweza kufanya hivi bila kutumia application au ujuzi wa ziada.
Simu ndogo za kawaida pia ipo hiyo 'feature'.
Na je, kumrekodi mtu unaeongea nae kwenye simu bila ridhaa yake ni sahihi kisheria?
 
Mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni za kuwania nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani, zimeingia dosari baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Mwanga, Ibrahim Mzava, kudaiwa kuendesha mchakato huo kwa ubaguzi wa dini pamoja na kuomba rushwa kwa baadhi ya watia nia wa Ubunge kwenye jimbo hilo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Sauti iliyovuja inamuhusisha Mwenyekiti huyo, ikisikika akizungumza na mmoja wa watia nia, wakijadiliana umuhimu wa nafasi ya Mbunge wa jimbo, ikishikwa na mtu anayetokea kwenye dini ya uislamu.

Sauti hiyo ilisisitiza kwamba ili mchakato huo uende vizuri, lazima mgombea awe Muislamu badala ya watu wa imani nyingine.

#KitengeUpdates

View attachment 3406128
Jogoo atawika mara tatu kabla hajatukana na kutusaliti.
 
Mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni za kuwania nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani, zimeingia dosari baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Mwanga, Ibrahim Mzava, kudaiwa kuendesha mchakato huo kwa ubaguzi wa dini pamoja na kuomba rushwa kwa baadhi ya watia nia wa Ubunge kwenye jimbo hilo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Sauti iliyovuja inamuhusisha Mwenyekiti huyo, ikisikika akizungumza na mmoja wa watia nia, wakijadiliana umuhimu wa nafasi ya Mbunge wa jimbo, ikishikwa na mtu anayetokea kwenye dini ya uislamu.

Sauti hiyo ilisisitiza kwamba ili mchakato huo uende vizuri, lazima mgombea awe Muislamu badala ya watu wa imani nyingine.

#KitengeUpdates

View attachment 3406128
Japo hii ni clip ya uchaguzi wa 2020, mzee anayetajwa hapo keshatangulia, lakini
huu ni udukuzi ni kosa la jinai!, na anayesambaza hii, anafanya jinai!.
P
 
Itakua ndio maagizo y CHURA a.k.a Dalali ju ya iyo dini yao.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Huu ni udukuzi ni kosa la jinai!, na
anayesambaza hii, anafanya jinai
!.
P
Kwanza hilo poyoyo linalouliza hayo maswali na lafudhi yake tu, unajua hili poripori la vijijini
Mipumbavu hii mingi haijui sheria huwa inatumwa na mihemko ya tope zilizo jaa vichwani mwao.
 
Back
Top Bottom