KATAVI: Walimu Zaidi ya 200 Waandamana ofisi za CCM kudai Haki yao ya kupandishwa madaraja

KATAVI: Walimu Zaidi ya 200 Waandamana ofisi za CCM kudai Haki yao ya kupandishwa madaraja

Takriban walimu 200 wa shule za msingi na sekondari Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameandamana mpaka Ofisi ya Mkoa ya Chama cha Mapinduzi wakiomba Serikali kuingilia kati madai yao ya upandishwaji wa madaraja ya mshahara baada ya kukaa kwa muda mrefu katika utumishi bila kupata stahiki hiyo.

View attachment 2766682

#AzamTVUpdates
Kazi ya ualimu ni mateso hususan shule za serikali,sijui kwanini serikali wasiboreshe maslahi ya walimu
 
Dhulma ni kubwa sana kwenye hii kada sijui huwa wanawaonaje Walimu. Intake ya 2012 Kigoma Manispaa walipanda 2019 kwa mara ya kwanza wakat wenzao sehemu nyingine walipanda 2016/17 lakin watu wapo na wanadai wanafanya kazi. Msoto ni mkali kwa hii kada
Kutakuwa na tatizo mahali hasa kwenye uongozi hasa kinachofanyw wengine wapandishiwe na wengine waachwe
 
Huko nyuma waliwaahidi madaraja mseleleko kwa walionyang'anywa madaraja yao 2016 enzi za Magu.Sijui limefika wapi?
 
Takriban walimu 200 wa shule za msingi na sekondari Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameandamana mpaka Ofisi ya Mkoa ya Chama cha Mapinduzi wakiomba Serikali kuingilia kati madai yao ya upandishwaji wa madaraja ya mshahara baada ya kukaa kwa muda mrefu katika utumishi bila kupata stahiki hiyo.

View attachment 2766682

#AzamTVUpdates
Madai ya walimu kwenye chama chetu tena ?!!! [emoji15][emoji15][emoji15][emoji23][emoji23]
 
Mahakamani bila kupitia ngazi nyingine nao ni ujuha,kuna vyama vya wafanyakazi, hata hiyo approach waliotumia ni sahihi itainua awareness,
Only in Tz...elimu elimu, yaani una matatizo na mwajiri ambaye ni serikali, hata hujui taratibu na sehemu sahihi pa kwenda na unakwenda ofisi ya chama utafikiri ndo waajiri wako! Kaazi kwelikweli....kama ndio hivyo, mtafika mmechoka mmechoka sana.
 
Dah! Kweli only in Tanzania! Hivi kwa uelewa wako unadhani walimu hawa ni majuha kiasi hicho cha kutojua taratibu! Yaani hatujui wapi tuende? CCM imetufukuza kwa kukosea kwenda kwao!? Hivi mnaelewa namna watendaji kwenye halmashauri wanavyotenda? Hivi unadhani simbachawene bila approach hii angekuja kuyasema aliyosema? Kwa taarifa yako wizara ya utumishi inajua sana ishu hii, na walimu walifika mpaka wizarani (wewe lini ulisikia chochote kuwa walimu wafika wizarani kwa madai halali ya madaraja?)
Tunapoamua kufanya jambo tunaloamini kinaongeza msukumo msituone wajinga! Yapo mambo hiyo serikali unayoisema haifanyi na si raia wala wewe unafanya lolote! Tunajua tulifanyalo ili madai yetu yatekelezwe.
 
ndio nashangaa wanaendaje pale bora wangeenda kwa mkurugenzi ambaye ni bosi wao. Mwenyekiti wa ccm mkoa anajua nini kuhusu ajira zao?
Mumuulize sasa huyo mkurugenzi kwanini alikuwa anatetema alipoitwa na mwenyekiti katika hili
 
Ccm ndiyo inasaini mkataba wa ajira ya mwalimu? Mnijuze mie jamani Nauliza tu.
Nami nikuulize tu, kwa uelewa wako ni nani unadhani anahusika kwa walimu zaidi ya 222 waliotakiwa kuwa promoted 1/5/2023 hawakuwemo kwenye bajeti? (kwa mujibu wa simbachawene)
Kuna TSC, Municipal HR na MEO...unadhani ni nani kati ya hawa na nani angeweza kuwasaidia walimu kupata haki yao (ukiuliza bila kujibu utakuwa unatafuta ubishi)
 
Back
Top Bottom