Naombeni mniambie mimi sijawahi kukutana na mamba wala chatu ila nahitaji kujua je ukikutana na Hao Wanyama.
Assume una upanga mkali yupi ukipambana naye Shambani huko ng'anya yake sio ndogo.
Yaani yupi ukijiingiza kwenye mfumo wake wa mtego pambano lake atakuzidi kirahisi na yupi mwepesi kumshinda
Hao wote ni balaa, usiwachokoze tu.
Maporini huko Botswana natembea zangu mara chatu hilo linapita,nikatoka baru naenda mbele Duma (leopard yuko mtini) nikageuza kiupoole.
Kuna siku tunaota moto na kuchoma Nyama za Nyati,
Simba alikuwepo pale anaskiliza story tu..
E bana fisi sijui walitoka wapi wakaanza kuchekachek
a pale,Yule Simba akatambaa nao wote.
Sasa lile vurumai,moto umevurugwa,nyama chali si wenyewe unakimbia mpk unapitiliza camp yako.
3.Siku Simba nae kaingia cha kike.
Hamna mnyama Simba anaogopa km mbwa mwitu(Wolf)
E bana sijui walifumaniana wapi huko Mbio.
Katika mbio simba kazama kwenye tent letu alafu kageuka anachekshia wale walikua wanamfukuzia.
Hajui hata km kuna binadamu mule.
Yaani hapo ikawa unajikojolea,kunya,sio kwa woga ule.
Unafkiria akigeuka huyu jamaa twafa.
Dah,bahati nzuri wale mbwa mwitu walipitiliza hawakumuona yule Simba kama tuko nae ghetto.
Wangemkuta mle ndani wote tungegeuzwa nyama.
Walipita wanabweka tu km 10 hivi.
Simba alivyookoka aah hana hata story na sisi huyo kaondoka zake kimya kimya.