Mimi nimeshakutana na simba, ombea ukutane na simba labda wapo pride (kundi lina majike na madume na watoto). Hilo kundi ujue lina uhakika wa kula.
Sasa katika vitu usiombee ni kukutana na mbarara (simba dume vijana ambao hufukuzwa kwenye pride na baba yao). Hawa huwa wana njaa mda wote maana kuwinda kwao ni changamoto.
Simba jike aliejitenga na pride ili azae na kukuza kwanza watoto. Usiombee pia.
Ila yote ya yote katika mapori haya usiombe kukutana na kundi la mbwa mwitu. Hao ukiwaona kwa mbali wala usikimbie tafuta tu mti upande.
Hawa wakikukamata wanaweza kuwa wameshakukula robo tatu ya mwili wako kabla roho yako haijatoka. Yani unaliwa huku unajiona.