Kati mamba, simba na chatu yupi mrahisi kuokoka tukikutana naye?

Kati mamba, simba na chatu yupi mrahisi kuokoka tukikutana naye?

Sio kweli, mamba akipiga pigo moja tu we ni mlemavu au mfu, mfano akicrush katikati na kichwani lazima ufe na hutopata nafasi ya kutumia panga lako, Simba muoga sana bila hata siraha, tochi tu ukimfata kwa ujasiri anakimbia labda ka ananjaa sana na yuko pekeake sababu Simba wanawinda kindugu (kundi)...chatu akikuua na uko na hilo panga lako we ni bonge la....

Chatu utamuweza. Hana mbio ya kukushambulia, kukupata ni mpaka akuvizie

Unamkata hapo kichwani

Simba ndo atakumaliza kirahisi, ana nguvu, mbio kuliko wewe,

Kucha 1.5 in kama nyembe, akikurukia na kilo zake 200+ utadondoka tu

Na pia unakuwa umejengewa 'fear trigger' ya kumuogopa simba, anavyosimuliwa, ukimuona kwenye video,

kwahiyo mkikutana macho kwa macho utakuwa na hofu kubwa, hutoweza kufikiri haraka haraka
Wanyama wote hapo juu ni hatari. Chatu ni vye pesi kukuweka kwenye Target. Chatu huwinda sehemu inyoendana na mazingira ya ngozi yake. Na ana mu detect prey kwa umbali mrefu. Ana naswa swala mwenye mbio sembuse Binadam. Chatu ni kiumbe kinachotisha mzee. Tunamuogopa tu Cobra au nyoka hawa wadogo sebuse hilo jitu. Chatu ni habari nyingine sio mchezo.
 
Anaconda ni mkubwa kuliko huyo na kwenye risasi hakuna mnyama ambae analeta ubishi ila huyo Mwanajeshi angeingia kwenye Ambush ya Chatu haina ujanja anakumeza.

Kumbuka yeye Chatu anawinda MLO akisikia NJAA lakini ukimkuta KASHIBA KALALA hana Harakati.
Kwani Simba anawinda ka kashiba? Simba muda wake mwingi huutumia kulala na ukiona wanawinda elewa wananjaa.
 
Sasa kuna chatu wakubwa Tanzania? uko na panga ukauliwa na chatu we ni...
Ujasiri wa kumkata panga utautoa wapi ??
Ngozi ya Chatu mkubwa haiwezi kukatwa na Panga. Panga litakuwa linadunda.

Nakumbuka Jan/2016 nilikuwa Pori la KIGOSI (Pori ambalo lipo kati kati ya Ushirombo na Runzewe) kama ulishawahi pita njia ya kahama - bukoba hilo pori unalijua. Mle ndani kuna makundi ya ma elfu ya ng'ombe.

Mmoja wapo na mimi nimewahi kuishi humo nikiwa nachunga ng'ombe wa Digii.

Siku moja Jioni mwaka 2016 kama kawaida ya sisi wachungaji wa ng'ombe tunakuwa na urafiki sana na mbwa, na hao mbwa huwa kama walizi wetu maporin haswa kwa maadui ambao hatuwezi kuwatambua kwa kuwanusa harufu zao hata kama wapo karibu mfano fisi au mbwa mwitu. Nk

Katika harakati za kulundi kambini sasa, si unajua tena mbwa anapenda sana mishe mishe za uwindaji wa sungura ama digi digi.

Kumbe maeneo anayopita na yeye ana windwa, kulikuepo na mtambo wa chatu. Eee bwana wee yule mbwa akawa amenaswa, mbona ulisikika mlio mmoja tu wa mbwa, na mbwa naye hakuwa wa kinyonge lilikuwa dume la mbwa kweli kweli.

Yule mbwa alikufa chap na haraka lakini yule chatu hakufanikiwa kumeza, uzuri tulikuwa karibu na kambi, makambini tunakuwaga na zile SOLO pamoja PARANEX kwa ajiri ya kuuwa kupe.

Kwa muda mfupi sana yule chatu alikuwa kashaaza process za kumeza yule mbwa.
Tulichofanya tukawa tumeweka paranex na kuweza kumnyunyuzia Machoni, yule mbwa akawa amemuachia.

Baada ya kumnyunyuzia yule chatu akawa anaficha kichwa chake kwenye Majani, na akafanikiwa kuigiza kichwa chake kweny shimo, ila mwili hakufanikiwa kuuigiza wote kutokana na ukubwa wake.

Sababu giza lilikuwa limeshaaza kuigia so ttuliamua kumuacha na ku deal naye siku inayofuata tulijua hataenda mbali.

Kesho yake asubuhi ikaandaliwa timu ya vijana walioshindikanaa porini, unajua maziwa ni kama bangi. Ukinywa maziwa muda mrefu hurewesha watu na akili inakuwa kama sio yako.

Tulifanya maandalizi ya kila aina ya silaha (majembe, shoka, panga), lakini nikuambie tu tulikuwa tukimkata kwa jembe, jembe lilikuwa linadunda.

Tulitumia siku nzima tunahagaika naye kumuua. Tulifanikisha kumuaa.

Nakuja na scenario ya mtoa maada ya kuji defend kwa panga pale unapokutana na Chatu hiyo njia huwezi kuifaulu. Utaliwaa

Pia nina exprience na simba, simba yeye anaogopa sana Moto. Moto kwake ni Adui

Pia simba kwa panga huwezi kumfanya kituu. Utaliwa.
 
Naombeni mniambie mimi sijawahi kukutana na mamba wala chatu ila nahitaji kujua je ukikutana na Hao Wanyama.

Assume una upanga mkali yupi ukipambana naye Shambani huko ng'anya yake sio ndogo.

Yaani yupi ukijiingiza kwenye mfumo wake wa mtego pambano lake atakuzidi kirahisi na yupi mwepesi kumshinda.
Mamba na simba ni hatari sana, hawa ni hard workers. Ukiwakuta wananjaa, kitapigika. Ila chatu ni tofauti, yeye ni slay killer. Atakulia timing hata lisaa ila ukijaa, tofauti n simba au mamba, yeye harudi nyuma. Yupo tayari kumake hata 50 attempts, yani ukikutana nae n ukajaa, kitapigika hata masaa 2 hadi either umjeruhi vbaya ndio asepe au ufe tu. Hana historia ya kukuacha mlemavu au mzima, yani either umuuwe, umjeruhi au yeye akuuwe, no extra option.
Alafu mnaosema chatu hana mbio mnamjua chatu nyinyi??? Alafu ubaya wake, akiwa anakukimbiza au kukufuatilia, unamskia anavyokukimbiza. Mlio wa miti anayoivunja n majani yaliyokauka unavuruga sana. Mnamsikia 3D akikufuatilia, acheni kabisa, ukichoka basi tena, dear landlord wa 6 feet under.
Alafu wazee, chatu haitaji kukulia timing. Imagine ameingia kwako na mkaonana uso kwa uso. HUTOKI. Kitapigika hadi umuuwe au ufe. Simba anaweza kuliwai jiko la gesi, ukiliwasha tu umemvuruga. Mamba ananguvu sana ukimkuta ghetoni mwake. Chatu haelewi. Kavurugwa. Hatareee. Kuwazidi maarifa wengine ni rahisi. Imagine kwenye maji kifo, juu ya mti au kitu chochote kifo, kwenye pori kifo, jangwani kifo. Ila mamba ni territorial majini, simba ukipanda mti au ndani ya maji hana ujanda. Yani afadhali ukutane nao kwenye cages tu mselfike, ila mbugani ndani ya territories zao, ni kama kunywa petrol lita nzima then kushushia sigara alafu kuexpect kupona. Tuombee kukutana nao kwenye cages, ndotoni au papa hapa jamii forums, ila live wote ni kifo express.
 
Mimi nimeshakutana na simba, ombea ukutane na simba labda wapo pride (kundi lina majike na madume na watoto). Hilo kundi ujue lina uhakika wa kula.

Sasa katika vitu usiombee ni kukutana na mbarara (simba dume vijana ambao hufukuzwa kwenye pride na baba yao). Hawa huwa wana njaa mda wote maana kuwinda kwao ni changamoto.

Simba jike aliejitenga na pride ili azae na kukuza kwanza watoto. Usiombee pia.

Ila yote ya yote katika mapori haya usiombe kukutana na kundi la mbwa mwitu. Hao ukiwaona kwa mbali wala usikimbie tafuta tu mti upande.

Hawa wakikukamata wanaweza kuwa wameshakukula robo tatu ya mwili wako kabla roho yako haijatoka. Yani unaliwa huku unajiona.
Semenya hilo zali la kukutana na mbwa mwitu nalitamani nakuliombea sana linitokee. Yani huo mkono ntakavyoutembeza hakuna kupanda mti.
 
Chatu utamuweza. Hana mbio ya kukushambulia, kukupata ni mpaka akuvizie

Unamkata hapo kichwani

Simba ndo atakumaliza kirahisi, ana nguvu, mbio kuliko wewe,

Kucha 1.5 in kama nyembe, akikurukia na kilo zake 200+ utadondoka tu

Na pia unakuwa umejengewa 'fear trigger' ya kumuogopa simba, anavyosimuliwa, ukimuona kwenye video,

kwahiyo mkikutana macho kwa macho utakuwa na hofu kubwa, hutoweza kufikiri haraka haraka
Mimi Mamba sitoboi ila hao wengi chatu na Simba vita nyepesi hiyo nikiwa na upanga tu kama alivyosema mleta mada.
 
Mimi Mamba sitoboi ila hao wengi chatu na Simba vita nyepesi hiyo nikiwa na upanga tu kama alivyosema mleta mada.
Simba wanawinda usiku malanyingi, afu wanakuwa wengi, Simba tochi kali tu inamtosha ukiwa jasiri, naongea kwa uzoefu sio hadithi, Simba ukimfata kwa ujasiri anakimbia, Mamba pia naongea kwa uzoefu sio hadithi, ile video ilotrend sana ya "nikasikia paaaa afu aiiiii.." yule jamaa mie nimeishi nae kwa kipindi fulani miaka ya 2018-2019 nikiwa na kazi fulani kule, chatu uko na panga unamuua wakati anaanza kukuzunguka, mapanga ya watu wa maporini yanakata zaidi hata ya wembe.
 
Kihistoria, mara nyingi watu huwa wanaokoka/ kuokolewa wakiwa wanashambuliwa mamba kuliko na hao viumbe wengine.

Ukiingia kwenye target ya Simba au Chatu unakuwa na maisha magumu sana, siyo tu kwa binadamu ila hata kwa wanyama wengine.

Ova
Mamba ndiye hatari kuliko wote kwa sababu maji ndio sehemu yake kuliko wewe,nguvu yake ni kama simba.Kuokolewa mara nyingi kunatokana na mazingira anayoishi mara nyingi binadamu wanakuwa jirani.Katika wote hao kama hakuna muokoaji basi bora ya simba na chatu.
 
Hiyo Picha huyo Chatu kammeza Mlinzi wa WFP mwenye AK47 wakati anavuka Fensi ndio akapigwa Zap akaing'ata Fence ndio kufia hapo hapo na asubuhi akakutwa hivyo hivyo.

Sudan Kusini.
Duh, hatari sana mkuu
 
Back
Top Bottom