Na yeye ndo chanzo cha Mgogoro wa sasa, anataka kuwa Kiongozi wa hicho Kikosi kisicho rasmi kwa maisha.
Ana roho mbaya na Ubinafsi, ukiacha ya Darfur, wakati wa mwanzo wa Maandamano ya kumuondoa Bashir, alitoa Amri kuwapiga Risasi wastani wa Waandamaji 100.....
Utofauti kati yake na Mkuu wa Majeshi ya sasa ulionekana kwenye Maandamano.
Hata Raia wengi wa Sudan hawampendi.
Ukiwauliza raia wa Sudan wanampenda Burhan kuliko Hemedti. Burhan pamoja na kwamba alifanya mapinduzi ya kijeshi kumuondoa madarakani PM aliyekuwa anakubalika miaka miwili baada ya Bashir kuondolewa kwa mapinduzi, bado Burhan ana unafuu maradufu.
Kiufupi ni kwamba, Hemedti aliongoza Janjaweed na alikuzwa na al Bashir kama buffer kuzuia jeshi lisimpindue baada ya kuchokwa na raia. Hemedti alitokea kwenye kuuza ngamia, baada ya kuwa close confidant wa al Bashir akaanza kufanya smuggling ya dhahabu kule Darfur na ndio akawa anafanya mauaji ambayo al Bashir anatuhumiwa nayo hadi sasa.
Mwaka 2019 kutokana na sanctions uchumi wa Sudan ukawa mbovu na ikumbukwe miaka ya nyuma hapo ndio South Sudan imetoka kujitenga baada ya gharama za vita kuwa kubwa kwa Sudan. Jeshi na RSF (Janjaweed mpya) ya Hemedti wakakubaliana wampindue al Bashir kuokoa muelekeo wa nchi baada ya maandamano ya mauaji ya watu miezi kama minne (yalianza pale bei ya mkate nayo ilipopanda).
al Burhan mkuu wa majeshi akawa mwenyekiti wa serikali ya mpito na Hemedti akawa msaidizi.
Baadae pressure ya kimataifa na maandamano yakafanya wachague serikali ya mpito ya kiraia na PM wao mzuri sana yule. Baadae wakaipindua tena. Ugomvi wao umekuzwa kutokana na tofauti zao, General Burhan anataka kukabidhi madaraka kwa raia ndani ya miaka miwili wakati Hemedti hataki kabisa kusikia hilo.
Hemedti miaka ya hivi karibuni ana support ya Wagner ya Urusi hasa kwenye kuchimba dhahabu, ana utajiri mkubwa kutokana na kuuza madini ya wizi Dubai yale yaliyomfanya aue watu Darfur. Saudi Arabia na UAE zinamuunga mkono.
Upande wa serikali ya Burhan unapewa support hasa na Misri (kwa sababu Sudan na Misri zinapinga GERD ya Ethiopia), nchi zote zisizo na maslahi binafsi zinamuunga mkono Burhan. Ni mwendawazimu pekee na asiyejua historia ya Sudan atamuunga mkono Hemedti.
Kuanzia Februari mwaka huu Sudan imekubali ujenzi wa naval base ya Urusi kwake, nahisi ni kutaka kuishawishi Urusi iondoe ushirikiano na Hemedti. Marekani imepinga ujenzi huo.
Kwahiyo iko hivi. Marekani hakuwa na maslahi na Sudan mpaka pale Urusi ilipotaka kujenga naval base, mpaka sasa sijui Marekani yuko upande upi ila inawezekana kwa kuwa Saudi Arabia na UAE zipo kwa Hemedti hata Marekani atakuwa uko (ukitaka Waarabu wagombane wewe wachonganishe, huwa wanachukiana kuliko wanavyoichukia Israel). Qatar nayo ina kiherehere kwenye vita za Kiislamu ila hapa siioni, wao bado wako busy na Al Shabaab.
Urusi serikali iko na maslahi na Burhan ila Wagner PMC yake iko na maslahi na Hemedti waibe madini. Kwahiyo Urusi inakula kotekote itakachotazama ni wapi kuna maslahi zaidi ila nadhani itaenda na Burhan.
Hemedti akishinda sahau kuhusu uchaguzi wala serikali ya kiraia, sanctions zaidi, ushirikiano mbovu kimataifa na umaskini maradufu. Burhan ni bora mara elfu na wala hana mpango na utawala. Kwanza kinachomfanya aendelee kuwa mtawala ni Hemedti ambaye hakubaliani na transition.
Kidogo nisahau jambo moja. Hemedti anashirikiana na vigogo wa zamani wa al Bashir ili kuhakikisha nchi haikaliki kiraia kusudi wasifunguliwe mashtaka, kutaifishwa mali zao na waendelee kuchaguliwa kwenye teuzi. Utawala mfupi wa PM aliyepinduliwa uliwaona kama takataka ukatafuta watu wapya. al Bashir mwenyewe yuko jela wanaogopa wasimfuate uko, Hemedti ana mashtaka pia hivyo anajitafutia kinga ya kushtakiwa.