Kati ya Hekima na Fedha Kipi ni Muhimu Kuliko Kingine?

Kweli kabisa mkuu, bila hekima hasingeamua mambo kwenye lile Bunge la wakeze ambalo lilikuwa na wajumbe wengi kuliko Bunge la Ndugai.
 
Hapo ni pesa tu baba, kichwa cha habari tu kimenifanya nitoe jibu maneno mengine zaidi ya hilo jibu ni upumbavu
Watu wa mwisho darasani hawakosekani kwasababu ya upumbavu wao na wewe ni mtu wa mwisho kwenye darasa hili. Ni toto tu kikuwa taacha!
 
Mwl Mwakasege aliwahi kusema akifundisha kwenye moja ya semina zake Dar kwamba "Hana uhakika kama Suleiman ameingia Mbinguni"
 
Marko.10:25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

Hilo andiko linateta wenye pesa au? Mbona halijatoa angalizo kwa Mamajusi (wenye hekima) pia?
 
Sawa mkuu
Maxence Melo Human Rights Icon of his days alitumia hekima kuanzisha jukwaa la JF, Ruge Mutahaba alikuwa na hekima kwanza alipobuni wazo la kuwa Media Mogul, Erick Shigongo alitoka Buchosa bila nauli akijificha chini ya viti vya treni Ma-TT wasimkamate na alipofika Dar alitumia hekima kuwashawishi Wahindi kumkopesha mtaji.
 
kwahiyo, hapo napata ufahamu kwamba hekima aliyoiomba Sulemani, ilikuwa ni kitendea kazi ktk ofisi yake ya Kifalme. ASANTE kwa ufahamu huo.
Lakini Mkuu, unadhani HEKIMA ni nini na ina THAMANI gani hata kuthubutu kuilinganisha na FEDHA?
Hakuambiwa achague kati ya hekima na hela apewe nini Bali aliambiwa aombe chochote kwa Mungu apewe akiwa na level ya ufalme kama ajira yake ndo Suleiman akaomba kupewa Hekima Ili aitumie kufungua mafumbo wakati wa kutoa maamuzi kama Mfalme au kutoa mashauri mema akiwa kama Mfalme kipindi hicho walikuwa ndiyo wanaoongoza kutoa dira ya Nchi iendeje na kutoa maamuzi ya kesi kuanzia ngazi ya mtu mmoja, familia mpaka jamii yote hivyo yeye aliona akipata Hekima ataweza kufungua mafumbo ya mashauri yatakayoletwa kwake na pia kutoa ushauri yenye haki baada ya kuchambua mafumbo yanayokuja kwake kama kesi na dira ya watu wake kwa mtu mmoja mmoja, hivyo hatuwezi kufananisha hekima na hela kwasababu hakuambiwa afanye uchaguzi wa hela na Hekima ila baada ya kuomba kwa Mungu kitu chema na kilichompendeza Mungu ndo Mungu alipombariki wa utajiri mkubwa wa Kila kitu yaani watoto, wake, Mali za kuhudumia hao wake na watoto, Taifa lake kubarikiwa na Hekima yenyewe aliyotumia kwenye kazi yake au maamuzi yake.
 
Hakuna mwenye hekima asiye na Pesa.
Sidhani Kuna watu wanahekima na pesa hawana na pia Kuna watu hawana hekima na pesa wanazo maana wamejua kuwa na nidhamu ya pesa tu wakaweza kuwa pesa, ila kwa Suleiman yeye alimpendeza Mungu na Mungu akambariki kwa Mali na asipungukiwe na Mali ikiwemo pesa.
 
Hekima haikai kwenye roho ya ubaguzi, udukuzi na jeuri.
Hivyo vyote ni utu mbaya au mtu mbaya uliosema yaani roho ya ubaguzi na jeuri na pengine Hekima anayo ila wakati wa kufanya maamuzi akiwa na Hekima zake kabisa anajitoa fahamu kupindisha maamuzi mazuri anachagua maamuzi mabaya makusudi tu Ili roho yake mbaya ifurahi au ajinufaishe na hayo maamuzi mabaya maana Hekima ni kufungua mafumbo magumu na ukajua ukweli utatoa maamuzi gani? Yenye haki au yasiyohaki.
 
Hekima yake ndiyo ilimfanya Mike Tyson akamuajiri, baada ya yeye Trump kupata pesa nyingi pesa hizo zikabomoa hekima yake. Kumbe pesa zinaharibu hekima lakini hekima haziharibu pesa, bora basi hekima kuliko pesa kama ni hivyo.
Pesa haikumuharibu ila ubaya wake ndo ulimuharibi hivi kama Mungu anambariki mtu hela iweje tena hela nyingi ziwe ni tatizo? Tatizo hapo ni mtu kama mtu akiwa ni mtu mbaya na matendo yake yakiwa mabaya au mtu Mwovu tu hata akipata bahati ya kupata Mali anatumia hizo Mali kuumiza watu na kufanya roho mbaya yake kama yeye mwenyewe alivyo Mwovu, hivyo tusikatae kubarikiwa Mali nyingi kama sisi ni watu wema na Mali hizo tukazifanyia wema kama kutoa kwa wahitaji.
 
Mwl Mwakasege aliwahi kusema akifundisha kwenye moja ya semina zake Dar kwamba "Hana uhakika kama Suleiman ameingia Mbinguni"
Kuna watu wananeema ya Mungu maana amesema anawajua waliowake tayari na hao kwa wema wao wanaoutenda hata pale wanapokosea huwa wanapewa nafasi au njia ya kutubu mpaka wanatubu na hao huwezi kujilinganisha nao maana wakikosewa Mungu huwa anawalipizia kisasi yeye Mwenyewe anaweza kuwa hata mtoto wako amechaguliwa na Mungu utaona anapenda kufanya haki, na wale wengine wengi wasiochaguliwa ila wataokolewa kwa Neema tu kulingana na matendo yao duniani kama yakiwa mema na Mungu haangaiki nao zaidi ya kuwanyuka tu pale anaona wanazidi kuumiza wake.
 
Marko.10:25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

Hilo andiko linateta wenye pesa au? Mbona halijatoa angalizo kwa Mamajusi (wenye hekima) pia?
Tajiri maana yake ni mtu mwenye kiburi cha kujiona anaweza Kila kitu bila msaada wa Mungu yaani yeye kama yeye anajiona kama mwenye uwezo wa jambo lolote na anapofanikisha jambo Hana shukurani yoyote kwa Mungu huyo ndo tajiri na ndo ni ngumu kwake kuingia Mbinguni ila watu waliobarikiwa Mali kwa uweza wa Mungu kuwa kwao na Mali siyo kikwazo kwao kuingia Mbinguni kama wanatenda mema, Mbingu ipo kwa watenda mema wote kasoro watenda mabaya na hao matajiri yaani wenye viburi hata kama ni masikini hawana kitu kama wanatabia za utajiri au kiburi cha kujiona wao ndo Kila kitu na walijiumba wao hawana wa kumshukuru kwa wao kuubwa basi hawataingia Mbinguni.
 
Vipi Anania na Safira?

Kitabu cha Matendo ya Mitume.5:1-11.
1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na mkewe Safira waliuza kiwanja. 2 Huku mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume.
3 Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja? 4 Je, kabla hujauza hicho kiwanja si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, fedha ulizopata si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.”
5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia. 6 Vijana wakaja, wakaufunga mwili wake sanda, wakamchukua nje kumzika.
7 Saa tatu baadaye mkewe Anania akaingia, naye hana habari ya mambo yaliyotukia. 8 Petro akamuuliza, “Niambie, je, mliuza kiwanja kwa thamani hii?” Akajibu, “Ndiyo, tuliuza kwa thamani hiyo.”
9 Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje mkakubaliana kumjaribu Roho wa Bwana? Tazama! Nyayo za vijana waliomzika mumeo ziko mlangoni, wewe nawe watakuchukua nje.”
10 Saa ile ile akaanguka chini miguuni mwake na kufa. Nao wale vijana wakaingia, wakamkuta amekufa, wakamchukua wakamzika kando ya mumewe. 11 Hofu kuu ikalipata kanisa lote pamoja na watu wote waliosikia juu ya matukio haya.

Taswira zote kwa hisani ya google.


Anania na Safira wakihesabu kwa bashasha mauzo ya kiwanja na kuficha sehemu yake wasipeleke miguuni pa Mitume.



Petro ampiga power Anania na ku-R.I.P.


Safira amzukia Petro na kumuuliza mumewe Anania yuko wapi?


Anania kwishne, jasho lake sasa kuliwa na wasiolivuja kwasababu ya uroho wake tu, angekuwa na HEKIMA HAYA YOTE YASINGEMKUTA, pesa zinaponza HEKIMA HAIPONZI.

USHAURI WA BURE.

Watu wa leo (hasa vijana ambao ndiyo Kanisa la kesho) pelekeni sehemu ya mapato yenu miguuni pa Mwingira, Kakobe, Fernandis, Mwamposa, Billionaire, Frank, Gwajima, Lusekelo, GeorDavie, Malisa, Oyedepo nk nk maana hawa ndiyo Petro wa nyakati zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…