Kati ya Jay Moe na Fid Q nani mkali?

Kati ya Jay Moe na Fid Q nani mkali?

Hakimbizi vizazi vyote acha kudanganya watu.
Ndo maana nimesema watoto wa 2010 kama nyinyi lazima utasema mkali fidQ kitambo hicho anatafutwa mkali wa mistali jay mo anashindanishwa na wakali wenzake wakina afande sele na kina profesa jay huyo fidQ wako bado yupo mwanza analima sikiliza ngoma kama maisha ya boarding pia sikiliza ngoma kama mvua na jua zote hizo zinaishi mpaka dunia tutakufa wote lafu kasikilize ngoma kama ulimwengu ndo mama ndo utamjua vizur jay mo
 
List Ya Jay Moe.

1:Mpenzi kwa heri ft Tid
2:Mvua na jua
3:Maisha ya boarding.
4:Mshamba
5:Cheza kwa steps
6:Kimya kimya vs Ngwea
7:Stori tatu.
8😛esa ya Madafu
9:Famous ft p funk.
10:Kama unataka demu ft solo thang&sir nature.
Alafu mtu anakwambia fidQ mkali kuliko jay mo kama hiyo ngoma ya kwanza jamaa katumia akili sana kutunga anawasimulia story jamaa zake maskan jinsi alivyo opoa mtoto jamaa kichwa sana
 
Fid Q

Fid Ni hazina kwa taifa letu, mpaka sasa hapajakuwapo msanii mwenye mashairi ya kufikirika kama fid. Majani mwenyewe alishakirii, fid ni Legend, and HE DO FOR SAKE OF HIP HOP not pesa au umarufu.
Ingawa anajua ustaa mzigo wa miba, fid amekubali kubeba, inasikitisha mnapomkonyeza kwenye giza, au kwenye mwanga mnavyompakaa punda stripe ili awe Zebra, fid yupo High level ndo maana humwoni, na atabaki juu kama kizIbo cha soda. Fid hazeeki anavua magamba kama nyoka,fid is man and half, fid ni simba ambaye ni raster.
 
Najaribu kuzicheki ngoma kali za jay mo za kukaa mzani sawa na ngoma kama neno, ielewe mitaa professional, august 13, mwanza, sipati

Mo tekniksi ana ngoma kadhaa kali ila sio za kuzidi hapo.. Haraka haraka nazipata stori 3, famous(hizi ngoma ni daraja lake) kina mvua na jua, bishoo, maisha ya boarding zitafata huko nyuma.
Sasa hizo 2 tu kwenye playlist nikizikuta zimekaa na ielewe mitaa, nitaziplay mwisho baada ya ielewe mitaa.

Sehemu mo alifanya kazi inawiana na ngosha ni kolabo za girlfriend na zeze, humu uzani sawa au alimzidi fid kwenye umbo namba 8
 
Wote wa kawaida

Tz hip hope ni
Father Nelly
Sugu
Prof jay

Ni ao tu wengine watoto Wadogo hawana wanachoimba
 
Tufanye kulist hit songs za kila mmoja

Naanza fid Q
1. Am professional
2. Mwanza mwanza
3. August 13
4. Ielewe mitaa
5. Propaganda
6. Ulimi mbili
7. bongo hiphop
8. Utaua game
9. Danger
10. Shimo limetema
11. Usinikubali haraka
13. Maselabration
14. Tajiri yangu
15. Temanoleji
16. Bendera ya chuma
17. Sumu
18. Ole chizza
19. Neno
20. Mwanamarundi
21. Ripoti za mtaa
22. Ngosha the swager don


Mje na list kama hiyo[emoji115] kuthibitisha ubora wa hao mnaowaweka mizani na FID Q sio kelele tu

Mtu aje na list ya jay Mo mchopanga tafadhari[emoji120]
 
Tufanye kulist hit songs za kila mmoja

Naanza fid Q
1. Am professional
2. Mwanza mwanza
3. August 13
4. Ielewe mitaa
5. Propaganda
6. Ulimi mbili
7. bongo hiphop
8. Utaua game
9. Danger
10. Shimo limetema
11. Usinikubali haraka
13. Maselabration
14. Tajiri yangu
15. Temanoleji
16. Bendera ya chuma
17. Sumu
18. Ole chizza
19. Neno
20. Mwanamarundi
21. Ripoti za mtaa
22. Ngosha the swager don


Mje na list kama hiyo[emoji115] kuthibitisha ubora wa hao mnaowaweka mizani na FID Q sio kelele tu

Mtu aje na list ya jay Mo mchopanga tafadhari[emoji120]
1. Bishoo
2. Misosi Mitungi na Pamba ft Ay
3. Kama unataka demu ft Solo & Q chief
4. Safari Njema ft Dudubaya & Complex
5. Kimya kimya ft Ngwea
6. Cheza kwa step ft Ngwea
7. Maisha ya boarding ft Dully
8. Tingisha ft TID
9. Story 3
10. Mshamba ft Sir Nature
11. Majukumu
12. Kasimama peke yake ft Shakii
13. Twende kwa mganga
14. Mwingine ft Raha P
15. Famous ft Majani
16. Mpenzi kwaheri ft TID
17. Narudi Shule Ft Fa
18. Nisaidie kushare
19. Pesa ya madafu
20. Mawazo
 
Ndo maana nimesema watoto wa 2010 kama nyinyi lazima utasema mkali fidQ
1986 ni mtoto wa juzi kabisa wewe. Tumeanza kufatilia Hip Hop tangu enzi za Yo! Rap Bonanza, za marehemu Kim Mgomelo akina Adili Kumbuka,Ibony maalim. Enzi za Weusi Wagumu Asilia. Too Proud akiwa wamoto. Kiroboto kabla ya TMK, Enzi za Don Bosco, Soundcrafters na Mawingu. Majani akiwa bado anarap na Master J akiwa ulaya masomoni.

By the way bwana mdogo hakuna sehemu yoyote ile niliyoandika Fid Q ni mkali zaidi ya Jay Mo.
 
Back
Top Bottom