92 jerrie
JF-Expert Member
- Feb 28, 2022
- 7,273
- 16,705
[emoji23][emoji23][emoji23]Sawa Mungu mgawa ridhiki....ukitaka nitapata tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23]Sawa Mungu mgawa ridhiki....ukitaka nitapata tu
Naunga mkono hoja, kuna aina mbili za familia.Hata hivyo mtu yeyote anaweza kukaa SITI ya MBELE iwe Mama au MKE au mtoto itategemea Kwa maana hayo ni mambo madpfp ila kama kuna mazingira ya kuonyesha Nani anastahili kukaa MBELE basi MKE ndiye anayestahili. Maana kuna Wamama wengine wanachokochoko Sana. Kumzaa MTU hakukupi Haki ya kuvunja itifaki ya nature na kumfanya MTu uliyemzaa kuwa mtumwa. Nafasi lazima ziheshimiwe.
Kisheria na kikanuni, kwenye familia mama na Baba anashika nafasi ya tatu Huko kama sio ya nne. Kwa mtiririko huu.
1. Mume na MKE.
Hawa ndio nafasi ya Kwanza. Yaani MKE lazima Ampe mumewe nafasi ya Kwanza halikadhalika na Mwanaume/mume lazima Ampe Mkewe nafasi ya Kwanza katika familia.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
mama mkwe wako ni muelewaMiaka 5 nyuma ilitokea scenario kama hiyo nikajiongeza kukaa nyuma mama mkwe akaniondoa akaniambai siti yako huko mbele na mume wako yeye akakaa nyuma. Fast foward mwaka huu nikiwa na binti tayari mama mkwe alimfungulia binti mlango akae mbele na baba yake mimi na yeye tukakaa siti ya nyuma. ( ingawa sipo na mwanae tena). So mke anatakiwa akae mbele na ubavu wake.
Sent using Jamii Forums mobile app
wa hivyo unampotezea itafika mda atachoka,mi hata akitaka amfulie mwanae namuacha tu(sina mamamkwe wa hivyo)Mama mkwe wako anafanana mama mkwe wa mama yangu, (bibi) tabia za kisirani, mfano kuna siku alimwambia mkamwana ampishe ana maongezi na mwanae yani kwenye chumba chake mkamwana, hebu fikiria mamkwe kama huyo,, hata kwenye gari anapenda seat ya mbele balaa ni wale mama wakwe wenye gubu la mwendokasi, ndo hivyo maza alishampuuza
Hachoki yule mtu,, nyie kuna wanawake wanaolewa kuchungu sana,wa hivyo unampotezea itafika mda atachoka,mi hata akitaka amfulie mwanae namuacha tu(sina mamamkwe wa hivyo)
kazi iko ni kichomi haswaHachoki yule mtu,, nyie kuna wanawake wanaolewa kuchungu sana,
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Na sisi wenye bodaboda mshikaki nani atangulie[emoji16]
Your mother, is senior to you too, are you older than your mother?Among the two, wife and mother; who's senior to the other?
Natumaini hiyo gari ni saluni, mke atakaa mbele. Ikiwa ni pick up, na kiti ni kimoja, Mama atakaa mbele au kama mke anaweza kuendesha, basi mume atakaa nyuma. Kama pick up ina kiti kipana, wote watakaa mbele.KATI YA MAMA NA MKE NANI ANAPASWA KUKAA SITI YA MBELE WAKATI UNAENDESHA GARI?
Anaandika, Robert Heriel
Rafiki yangu Hosea amenipigia simu akaniuliza hivi; Kati ya Mama yake na MKE wake Nani anastahili kukaa SITI ya MBELE ya GARI wakati yeye(Hosea) anaendesha Gari? Nikaona niilete mada Hii kwenu. Ili tujifunze wote.
Imekuwa ni kawaida ya Watu kutaka kuwalinganisha MAMA na MKE kuwa Nani zaidi ya mwenzake.
Nataka kusema kuwa ni makosa makubwa kulinganisha vitu au Watu wasiolingana. Mke ni daraja jingine na Mama ni Daraja jingine.
Pili, Kati ya MKE na Mama hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake isipokuwa ubora wao utapimwa Kwa namna watakavyo au walivyotekeleza majukumu yao Kwa nafasi zao. Mama kuzaa pekee yake haimfanyi kuwa Bora isipokuwa yapo majukumu mengine kama malezi. Halikadhalika MKE kukuzalia Watoto pekeake haitoshi kumfanya awe Bora kwako isipokuwa majukumu yake Kwa Watoto pamoja na wewe kama mumewe.
Kama utapima uzito wa majukumu ya MKE na Mama bila kujali madaraja Yao basi utagundua MKE ni zaidi ya Mama, na hapo nazungumzia kimajukumu na kiwajibu. Hata hivyo hiyo haimfanyi MKE kuwa Bora zaidi ya Mama.
Asubuhi nilitoka kuelezea mada isemayo Watu Maskini na wajinga hupenda kuongozwa na Mitazamo na Maoni ya Watu zaidi kuliko Kanuni na sheria. Kama tungefuata Kanuni na sheria Hilo swali lisingekuwepo na haya mambo ya kulinganisha MKE na Mama yasingekuwepo. Kwa sababu Kanuni na sheria zipo wazi kabisa.
Rafiki yangu Hosea aliponiuliza swali hilo nilimjibu Kwa kumuuliza maswali yafuatayo;
1. Nikamuuliza; Kitandani mwako unalala na Nani?
Mbona haukuniuliza Kati ya MKE na Mama yako Nani ambaye utalala naye kitanda kimoja?
Akaguna, akasema hayo mambo ni tofauti na mambo ya SITI za magari.
2. Nikamuuliza, Kati ya Mama na MKE wako Nani anaitwa Mrs. Hosea? Akajibu MKE wangu.
3. Nikamuuliza, Wakati Mama yako anakaa SITI ya MBELE na wewe, je Mkeo atakaa nyuma na Baba yako(mkwewe)? Yaani Wakati Mama yako anang'ang'ania kukaa SITI ya mbele, Baba yako anakuwa yupo wapi au mumewe anakuwa yupo wapi?
4. Nikamuuliza, Watoto wako watakubali Mama Yao(Mkeo) umuweke Nyuma ilhali wewe ndiye mume wake(Baba Yao)? Huoni utajenga kitu kwa Watoto kuwa humpendi Mama Yao na umemuweka katika nafasi ya pili?
Huoni hiyo itakuathiri Huko baadaye Watoto wakikua?
Hata hivyo mtu yeyote anaweza kukaa SITI ya MBELE iwe Mama au MKE au mtoto itategemea Kwa maana hayo ni mambo madpfp ila kama kuna mazingira ya kuonyesha Nani anastahili kukaa MBELE basi MKE ndiye anayestahili. Maana kuna Wamama wengine wanachokochoko Sana. Kumzaa MTU hakukupi Haki ya kuvunja itifaki ya nature na kumfanya MTu uliyemzaa kuwa mtumwa. Nafasi lazima ziheshimiwe.
Kisheria na kikanuni, kwenye familia mama na Baba anashika nafasi ya tatu Huko kama sio ya nne. Kwa mtiririko huu.
1. Mume na MKE.
Hawa ndio nafasi ya Kwanza. Yaani MKE lazima Ampe mumewe nafasi ya Kwanza halikadhalika na Mwanaume/mume lazima Ampe Mkewe nafasi ya Kwanza katika familia.
2. Watoto
Hawa ndio wanashika nafasi ya Pili. mume na MKE huhangaika Kwa Ajili ya Watoto wao kuwalea mpaka wakikua.
3. Wazazi
Baba na Mama. Hawa ndio hushika nafasi ya tatu katika mahusiano ya familia. Baba na Mama yako ni familia nyingine yenye uhusiano wa karibu wa kidamu na ninyi. Ila haina maana wao ndio wawe namba moja.
4. Ndugu
Hawa ni wale mliozaliwa pamoja iwe Baba mmoja, Mama mmoja, mtoto wa Mama mkubwa au mdogo, wajomba, mashangazi n.k.
5. Jamaa
Hawa ni wale wenye undugu wa mbali, undugu wa Tochi.
6. Marafiki.
Hawa ni wale ambao hamna undugu lakini mnaukaribu na mahusiano mazuri.
Zingatia Watoto utakaowazaa wewe kwako ni namba mbili lakini wakishakua na kuanzisha familia wao watakuweka namba tatu. Na wajukuu watakuwa nafasi ya nne Huko, hivyo unakosa mamlaka ya kuingilia familia zao labda wakuombe ushauri.
Jukumu kubwa la mzazi ni kuwalea Watoto wake katika miaka yote ya uhai wake. Lakini sio kudai nafasi zisizo zako. Jukumu la mtoto ni kuwaheshimu wazazi wake, kwa kusikiliza mashauri Mema.
Kama Mama yako anakupenda Sana basi atapaswa aonyeshe upendo huo Kwa Baba yako mzazi. Yaani abaki kwenye nafasi yake. Nafasi ya mume wake asikupe wewe. Wala wewe usimpoke Baba yako nafasi yake Kwa Mama yako. Kila mmoja abaki kwenye nafasi yake.
Baba yako ndio anapaswa kumfanya Mama yako namba moja na sio wewe. Kumfanya Mama yako namba moja ni kutomheshimu Baba yako na kutokumpa heshima Mkeo.
Ni Sawa na Mkeo asikupe nafasi ya Kwanza kama mumewe, lazima ujihisi kudharaulika.
Hujawahi sikia Watu wakilalamika Wake zao hawawasikilizi ila wanasikiliza Wazazi wao.
Ukiona Mkeo hakusikilizi na hakupi nafasi ya Kwanza, fukuza mapema, Huko mbeleni sio salama. Ukiona Mumeo anajifanya anawapenda Ndugu au wazazi wake kuliko wewe kimbia, Achana naye huyo Hana Akili na hajitambui. Mwambie akalale na hao Ndugu zake. Wala usimuonee aibu wala usimfiche, mpe makavu.
Ni hatari kuoa au kuolewa na MTU asiyejua kutenganisha mipaka na makundi ya Watu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Naunga mkono hoja, kuna aina mbili za familia.
1. Nucleus Family
Hapa familia ni baba, mama na watoto. Hizi ni familia za kizungu, wazazi, uncles na aunts sio sehemu ya familia na wakizeeka wanakuwa abandoned kwenye nursing home till death do them away!. Usually familia za hivi zina standard car ya 4 seater, baba na mama mbele, watoto wawili seat ya nyuma. Babu na bibi wakija for visit, they rent a 7 seater, baba na mama wanakaa mbele, watoto wanakaa seat ya pili, babu na bibi wanakaa seat ya nyuma.
2. Extended family
Baba, mama, bibi, babu na watoto.
Hizi ni typical African family, mtu muhimu kuliko hata wewe ni baba na mama, mke, watoto.
Wazazi wakija seat ya mbele unakaa na baba au Mama, mke na Mama au baba seat ya pili na watoto wanakaa kule mwisho.
Akija kaka yangu au ndugu yangu, mke anakaa nyuma na watoto.
Kiafrika undugu ni wa damu tuu, hivyo ndugu ni baba Mama waliokuzaa, wale mliozaliwa nao na watoto wenu, mke sio ndugu na ndugu wa mke ni jamaa tuu!.
Mke ni mtu tuu wa kuja na kupita, anaweza kuachwa ukaoa mwingine au wakaolewa hata wake 10!. Familia za hivi wazazi ndio muhimu zaidi, mama akija home, mke lazima ajishushe kumpisha mama in control.
Wazazi wakizeeka wanakuwa taken care na watoto kwa upendo mpaka siku yao ikifika.
P
Hujaelewa alichouliza mwenye kuanzisha mada. Soma upyaYour mother, is senior to you too, are you older than your mother?
Kuna uzi wa 'makapuku' utafute mkajadiliane huko!! [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Tusio na gari tunaandika wapi?
😅😅😅 naomba link mkuuKuna uzi wa 'makapuku' utafute mkajadiliane huko!! [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]