Kati ya Marekani na Israel nani bosi na nani anamtumia nani na kwanini?

Israeli iko annexed kuwepo mashariki ya kati kwa manufaa ya USA, lengo kuu la USA ni kuhakikisha anakabiliana kwa haraka na maramoja na vitisho vyote vya mashariki ya kati.

USA kama superpower lazima ahakikishe kila upande ambako kunauwezekano wa kuwa na maadui anakudhoofisha.
Mashariki ya kati kuna historia ya giants kama Ottoman, Persian nk, Islam na Muslim ambao wamedominate eneo hilo ni kitisho kingine tena kwa USA.
 
Kama bila Wayahudi US hajiwezi kwanini US iwe na nguvu ya kuicontrol Israel badala ya Israel iwe na nguvu ya kuicontrol US? Pia nimeuliza leo Wayahudi wakisema wahamishe mitaji yao waipeleke Israel je israel itakuwa tajiri kama marekani na je hao matajiri wa kiyahudi wataendelea kuwa matajiri kama walivyo hv sasa?
Israel ndio inaitegemea mno Marekani Ili iendelee kuwepo.
 
Kwann Wayahudi waliozaliwa na kukulia israel siyo wa wavumbuzi kama wale waliozaliwa na kukulia US?
Israel imeshatoa washindi 13 wa tuzo za Nobel mpaka sasa hivi,
Softwares za udukuzi wa mawasiliano zinazotumiwa sehemu nyingi duniani zinatoka Israel.
Africa inapeleka maelfu ya wanafunzi kila mwaka kujifunza kilimo Israel jangwani.
 
Israeli iko annexed kuwepo mashariki ya kati kwa manufaa ya USA, lengo kuu la USA ni kuhakikisha anakabiliana kwa haraka na maramoja na vitisho vyote vya mashariki ya kati.

USA kama superpower lazima ahakikishe kila upande ambako kunauwezekano wa kuwa na maadui anakudhoofisha.
Mashariki ya kati kuna historia ya giants kama Ottoman, Persian nk, Islam na Muslim ambao wamedominate eneo hilo ni kitisho kingine tena kwa USA.
Sasa wewe ndio umetoa jibu kwann US inaing'ang'ania Israel
 
Sasa wewe Afrika upewe msaada sawa na Marekani kama anavyopewa Israel, unawapa nini Wamarekani?

Wayahudi waliopo USA ni 7.4m, wakati population ya pale Israel ni 9.4m, na hao 9.4m wapo pia waarabu na makabila mengine madogo madogo. Lakini wayahudi hapo Israel ni 7.2m. Kwa hiyo kuna wayahudi wengi Marekani kuliko waliopo Israel.

Na ufahamu kuwa hao 7.4m jews huko USA siyo hohe hahe, wapo wawekezaji wakubwa, wapo wataalam wa viwango vya juu kwenye tekinolojia mbalimbali, wapo wanasayansi na wagunduzi.

Leo hii wayahudi waliopo USA wakiamua kuhamishia utajiri wao wote Taifa jingine, pengo la uchumi Marekani litaonekana, na huko watakakohamishia, nchi kama ilikuwa maskini itahama na kuwa miongoni mwa nchi tajiri.

Utajiri wa mabilionea 267 wayahudi unafikia kiasi cha dollar 1.7 trillion, yaani zaidi ya mara 4 ya GDP ya Iran, zaidi ya mara 4 ya GDP ya Israel, zaidi ya mara 4 ya GDP ya South Africa, zaidi ya mara 3 ya GDP ya UAE.

Kwa hiyo, msaada wa Marekani kwa Israel, kiuhalisia siyo msaada, bali Marekani huwa inalipa fadhila ya Wayahudi waliopo USA wanaotoa mchango muhimu kwa maendeleo ya Marekani na Dunia.
Unajiona mchambuzi mwenyewe
 
Israel imeshatoa washindi 13 wa tuzo za Nobel mpaka sasa hivi,
Softwares za udukuzi wa mawasiliano zinazotumiwa sehemu nyingi duniani zinatoka Israel.
Africa inapeleka maelfu ya wanafunzi kila mwaka kujifunza kilimo Israel jangwani.
Hapo unathibitisha nilichokisema kwa sababu Katika tuzo zote 988 zilizowahi kutolewa wayahudi wameshinda tuzo 110 kati ya hzo 13 pekee ndio za wayahudi kutoka Israel.
 
Wayahudi waliopo USA ni 7.4m, wakati population ya pale Israel ni 9.4m,
This is irrelevant mbona kuna Indian Americans zaidi ya 5m ila hatuoni misaada ya kiasi hiko ikienda India?
Na ufahamu kuwa hao 7.4m jews huko USA siyo hohe hahe, wapo wawekezaji wakubwa, wapo wataalam wa viwango vya juu kwenye tekinolojia mbalimbali, wapo wanasayansi na wagunduzi
Mbona Indian Americans ina mabillionaire wengi pia wana miliki kampuni nyingi sana za IT, medicine na engineering?
Leo hii wayahudi waliopo USA wakiamua kuhamishia utajiri wao wote Taifa jingine, pengo la uchumi Marekani litaonekana, na huko watakakohamishia, nchi kama ilikuwa maskini itahama na kuwa miongoni mwa nchi tajiri.
Hii sio kweli, GDP ya Israel inaigia mara 6 kwa GDP ya California pekee so US inaweza hofia kupoteza Latin Americans waliojazana California kuliko kupoteza hao Jews wachache!!
Utajiri wa mabilionea 267 wayahudi unafikia kiasi cha dollar 1.7 trillion, yaani zaidi ya mara 4 ya GDP ya Iran, zaidi ya mara 4 ya GDP ya Israel, zaidi ya mara 4 ya GDP ya South Africa, zaidi ya mara 3 ya GDP ya UAE.
Let me put into context, makampuni ya indian Americans wanachangia 6% ya mapato yote ya kodi kwa serikali ya US. Yaani wanatoa USD 300 Billion kwa mwaka ambayo. Na pia makampuni yote US ambayo Indian Americans ni CEOs yanazalisha mapato ya USD 700 Billion ambayo ni zaidi ya GDP ya Israel USD 509 BIllion. So mchango wa wahindi kwa mapato ya USA ni mkubwa kuliko Israel.
Kwa hiyo, msaada wa Marekani kwa Israel, kiuhalisia siyo msaada, bali Marekani huwa inalipa fadhila ya Wayahudi waliopo USA wanaotoa mchango muhimu kwa maendeleo ya Marekani na Dunia.
Hapana mchango wa Indian Americans na Chinese Americans is possibly bigger than Jews so sijaelewa hii exaggeration ni ya nini. Hoja ni kwamba Israel ni kibaraka wà Marekani kulinda maslahi yake maana ndio nchi pekee isiyo ya kiislam mashariki ya kati na pia ipo eneo la kimkakati pale njia panda ya Afrika, Asia na Europe so in case of globa war American warships and submarines will need a base in that strategic part of the world. So siku matumizi yao yakiisha watapotezewa tu.
 
This is irrelevant mbona kuna Indian Americans zaidi ya 5m ila hatuoni misaada ya kiasi hiko ikienda India?

Mbona Indian Americans ina mabillionaire wengi pia wana miliki kampuni nyingi sana za IT, medicine na engineering?

Hii sio kweli, GDP ya Israel inaigia mara 6 kwa GDP ya California pekee so US inaweza hofia kupoteza Latin Americans waliojazana California kuliko kupoteza hao Jews wachache!!

Let me put into context, makampuni ya indian Americans wanachangia 6% ya mapato yote ya kodi kwa serikali ya US. Yaani wanatoa USD 300 Billion kwa mwaka ambayo. Na pia makampuni yote US ambayo Indian Americans ni CEOs yanazalisha mapato ya USD 700 Billion ambayo ni zaidi ya GDP ya Israel USD 509 BIllion. So mchango wa wahindi kwa mapato ya USA ni mkubwa kuliko Israel.

Hapana mchango wa Indian Americans na Chinese Americans is possibly bigger than Jews so sijaelewa hii exaggeration ni ya nini. Hoja ni kwamba Israel ni kibaraka wà Marekani kulinda maslahi yake maana ndio nchi pekee isiyo ya kiislam mashariki ya kati na pia ipo eneo la kimkakati pale njia panda ya Afrika, Asia na Europe so in case of globa war American warships and submarines will need a base in that strategic part of the world. So siku matumizi yao yakiisha watapotezewa tu.
Kuna wachafuzi kama watatu hapa forum ya kimataifa yaani hawa kwa kuongea pumba hawajambo yaani wanaropoka mpaka wanaropoka halafu sasa wanajiona wana facts kweli wakati wanaongea utumbo huyu sijui Bams shosti yake Tumaini nani sijui na udugu wake ward41 bila kusahau na britanicca hawa wa kupuuzwa
 
Hoja ni kwamba Israel ni kibaraka wà Marekani kulinda maslahi yake maana ndio nchi pekee isiyo ya kiislam mashariki ya kati na pia ipo eneo la kimkakati pale njia panda ya Afrika, Asia na Europe so in case of globa war American warships and submarines will need a base in that strategic part of the world. So siku matumizi yao yakiisha watapotezewa tu.
Kwa Sasa Israel lobby mfano AIPAC ina nguvu sana ndani ya Marekani....na ni kama huamua vile sera za nje za Marekani kuelekea Israel na mashariki ya kati ziweje....hata wanasiasa wa Marekani hujikomba kwa hao mabwanyenye wa kiyahudi Ili kupata ufadhili wa pesa za kampeni na kupata kura.
 
Bila fedha na silaha za Marekani, Israel ingekuwa marehemu. Huwa najiuliza. Nani anamtumia nani na kwanini?

Je hapa tatizo ni uzawa wa Israel uliotengenezwa kijambazi na wazungu kupitia Biblia au wese la waarabu? Ukiangalia misaada inayotolewa na marekani kwa Israel unachanganyikiwa.

Ni mingi na mikubwa kuliko Afrika. Je wananunua au kulipia nini? U.S. Aid to Israel in Four Charts linganisha na Bureau for Africa | Organization | U.S. Agency for International Development.
Wayahudi wanaosemwa apa ni wakina Elon Musk wa Twitter 🐦 🐦‍⬛ 🦜 na Mark Zuckerberg wa WhatsApp.
Hawa watu wana ushawishi mkubwa sana na pesa zao wawili zinaishinda uchumi wa Israel 🇮🇱 yote
 
This is irrelevant mbona kuna Indian Americans zaidi ya 5m ila hatuoni misaada ya kiasi hiko ikienda India?

Mbona Indian Americans ina mabillionaire wengi pia wana miliki kampuni nyingi sana za IT, medicine na engineering?

Hii sio kweli, GDP ya Israel inaigia mara 6 kwa GDP ya California pekee so US inaweza hofia kupoteza Latin Americans waliojazana California kuliko kupoteza hao Jews wachache!!

Let me put into context, makampuni ya indian Americans wanachangia 6% ya mapato yote ya kodi kwa serikali ya US. Yaani wanatoa USD 300 Billion kwa mwaka ambayo. Na pia makampuni yote US ambayo Indian Americans ni CEOs yanazalisha mapato ya USD 700 Billion ambayo ni zaidi ya GDP ya Israel USD 509 BIllion. So mchango wa wahindi kwa mapato ya USA ni mkubwa kuliko Israel.

Hapana mchango wa Indian Americans na Chinese Americans is possibly bigger than Jews so sijaelewa hii exaggeration ni ya nini. Hoja ni kwamba Israel ni kibaraka wà Marekani kulinda maslahi yake maana ndio nchi pekee isiyo ya kiislam mashariki ya kati na pia ipo eneo la kimkakati pale njia panda ya Afrika, Asia na Europe so in case of globa war American warships and submarines will need a base in that strategic part of the world. So siku matumizi yao yakiisha watapotezewa tu.
Uingereza ndio iliyoibua mpango wa kuwanzishwa kwa Jewish state mwaka 1917 kupitia Balfour Declaration. Uingereza iliyokuwa inatawala ardhi ya Palestina kama British mandate baada ya kuanguka kwa Ottoman ndiyo iliyotoa nafasi Palestina kwa Israel kufanya mambo yote yaliyotangulia mpaka kujitangaza wao ni nchi mwaka 1948.
USSR ilikuwa miongoni mwa mataifa ya kwanza kabisa kuitambua Israel kama nchi rasmi.
Kusema kuanzishwa kwa taifa la Israel ni conspiracy ya Marekani ni madai yasiyo na mashiko yanayopotosha ukweli wa kihistoria ulio wazi kabisa.
 
Kwa Sasa Israel lobby mfano AIPAC ina nguvu sana ndani ya Marekani....na ni kama huamua vile sera za nje za Marekani kuelekea Israel na mashariki ya kati ziweje....hata wanasiasa wa Marekani hujikomba kwa hao mabwanyenye wa kiyahudi Ili kupata ufadhili wa pesa za kampeni na kupata kura.
Yes hoja iwe ni lobbying, media, endorsements etc ila wanaosema chanzo ni jewish Population, sijui mapato ni irrelevant.
 
Huwezi kufanya lobbying Marekani kama huna pesa, tena aina ya lobbying wanayofanya AIPAC kwa vyama vyote viwili vya Republic na Democrats unahitaji pesa ndefu sana.
Pia Marekani ya sasa kukamata media unahitaji pesa ndefu sana pia.
 
Kusema kuanzishwa kwa taifa la Israel ni conspiracy ya Marekani ni madai yasiyo na mashiko yanayopotosha ukweli wa kihistoria ulio wazi kabisa.
Wapi nimesema Israel imeundwa na USA? nimesema clearly kabisa Israel ni kibaraka wake kama tu kama tu Ukraine ni kibaraka wa US na North Korea ni kibaraka wa Russia!!

Na yote ni sababu ya geopolitics, kwamba bila ally middle east je wata survive vipi USA? huwezi rely kwa saudia au Jordan maana sio stable kulinganisha na Israel.

Ndio maana USA huwa anatoa maagizo na Israel anafuata, hata Trump alisema akishinda hataki vita na unaona tayari Netanyahu kakubali mazungumzo. Sasa unasemaje Israel ndio inacontrol USA?
 
Waisrael ndo watengeneza Silaha wakubwa kwenye Jeshi la Marekani.
Kwahiyo wanategemeana,Marekani hawezi kumuacha mtaalamu wake amalizwe.
 
Wapi nimesema Israel imeundwa na USA? nimesema clearly kabisa Israel ni kibaraka wake kama tu kama tu Ukraine ni kibaraka wa US na North Korea ni kibaraka wa Russia!!

Na yote ni sababu ya geopolitics, kwamba bila ally middle east je wata survive vipi USA? huwezi rely kwa saudia au Jordan maana sio stable kulinganisha na Israel.

Ndio maana USA huwa anatoa maagizo na Israel anafuata, hata Trump alisema akishinda hataki vita na unaona tayari Netanyahu kakubali mazungumzo. Sasa unasemaje Israel ndio inacontrol USA?
Nini maana ya "kibaraka"?

Nini kinacholifanya taifa fulani kuwa kibaraka wa taifa lingine?
 
Huwezi kufanya lobbying Marekani kama huna pesa, tena aina ya lobbying wanayofanya AIPAC kwa vyama vyote viwili vya Republic na Democrats unahitaji pesa ndefu sana.
Pia Marekani ya sasa kukamata media unahitaji pesa ndefu sana pia.
Lobbying sio pesa ni kupenyeza watu wako kwenye sekta muhimu tu. Hao Black Americans wana pesa gani mbona walilobby hadi kupata Rais mweusi na sasa wàna VP mweusi?

Kingine hizo pesa za kampeni ni donations ila nmetoa hoja kuwa makampuni ya Indian Americans wanachagia 6% ya mapato yote ya IRS. Kwahiyo hapo issue sio uchumi ni kuchangia. Kwahiyo tuseme mabilionea wa kiyahudi wamejiinvolve kwenye siasa kuliko pengine wahindi. Ingawa kuna wahindu wawili kwenye serikali ya Trump, yule director wa CIA Tulsi gabbard na Bosi wa DOGE Vivek Ramaswamy but ingekua ndio Jews hao ungesikia kelele kibao kuwa Israel "inaitawala USA".
 
Back
Top Bottom