Kati ya mhitimu wa VETA na mhitimu ya kitivo cha Uhandisi utamwajiri yupi?

Kati ya mhitimu wa VETA na mhitimu ya kitivo cha Uhandisi utamwajiri yupi?

Engineer nimtaalam na hashiki nyundo kupaua nyumba .

Kazi ya Engineer ni kudesign na kumsimamia fundi Kutoka Veta ili ashike nyundo vizuri na kujenga mjengo aliodesign kama inavyotakiwa.

Usitegemee Fundi kutoka Veta aweze kudesign au kusimamia structure ya jengo kama lile la Bandari .

Wanapoambiwa waende Veta ni kwa ajili ya kujifunza namna ya kushika ,beleshi ,kijiko , Kobilo na nyundo na kupaua jengo au kujenga jengo alilodesign yeye mwenyewe ili ajiajiri yeye mwenyewe kwenye ujenzi mdogo mdogo.
Lakini pia veta kuna kozi nyingi za kujiajiri kama upishi, kusuka nywele ,mapambo , kutengeneza unga wa lishe ,kusindika vyakula ns vinywaji, kutengeneza sabuni n.k
Kwa hiyo unataka kusemaje?
 
Naenda maonyesho ya sabasaba kila mwaka, huwa napitia mabanda ya VETA, SIDO na Kitivo cha UHANDISI UDSM kote nakutana TU na mashine za kufyatua matofali zenye ingini kutoka China, ninashindwa kutofautisha viwango vya ujuzi kati ya taasisi hizi tatu. Je, ni mhitimu yupi Bora kati ya wanafunzi wa VETA na wale wa kutoka Kitivo cha UHANDISI UDSM? Kama mwajili utapenda kutoa ajira kwa mhitimu yupi?
Namuajiri anaejua Kazi,sijali amesoma wapi ilimradi nikimpa Kazi anafanya nakumaliza,kuna watu kwenye makaratasi vipanga lakini kazini zero
 
Ndio hawa wapuuzi humu wanaandika ujinga wa kuponda Engineers waeleze,labda veta kuna astronauts na aviation Engineers au technicians
Mimi siwaelewi kabisa, ila ninachoelewa ni kwamba spokes za baiskeli yangu zimetoka China na India, hata kengele pia imetoka hukohuko. Angalau madaktari wanasema sasa hivi wanapandikiza figo na kuweka maputo tumboni kupunguza uzito, hawa maenginia wanafanya nini? Janani hata midoli ya watoto wetu mmeshimdwa achilia mbali baiskeli.
 
We jamaa inaonekana hata chuo hujafika wewe
Sijafika chuo kipi? Mimi sijui inginia anasomaje lakini najua inginia anatakiwa aisaidie nn jamii. Jamii inaagiza majembe chapa jogoo kutoka China, hii ni sawa? Jamii inajenga majengo ya serikali yanayopata nyufa muda mfupi TU baada ya kukabidhiwa, yanavuja na yanaanguka mengine. Hii ndiyo sawa?
 
Dah km$mk nchi ya ajabu hii apa wapo walimu,wat wa maendeleo ya jamii na wahasibu wanawajadili ma injinia na hamna wachoelewa,
Mimi kama injinia na weza kufanya kazi za technician ila technician ni ngumu mnoo au hawez kabisa kufanya kazi za engineer..
Technician ni mtu wa implementation tu,kazi izi ngumu sana k$#me zinanzia kichwani from the idea,designing kwenye step tofaut tofaut,quality assuarance na kuandaa bill za material kuendana na design na budget iliokuepo ..
Hali ikiwa ngumu michongo hakuna ma injinia wengi t tunatafutaga machaka ya u technician tuish,ila technician hawez kwenda kufanya kazi za injinia hata kama anaopenda hela nyingi.
So tuheshimu sana proffesional za watu..
Unaenda kupanda ghorofa posta pale uko very comfortable una amani ujue Kuna kazi kubwa sana imefanyika ya akili na mahesabu mengi.
Mbona mifano hai tunayo mkuu.

Rejea sakata la kariakoo.

Walikusanyana Mafundi mchundo, waka ignore the roles of engeneers, wamwambia bwana mkubwa hili tunaliweza ni chapu tu.

Kilichotokea wote tunakijua, Na haya ndo mazara ya kutumia nguvu nyingi akili kidogo
 
Mbona mifano hai tunayo mkuu.

Rejea sakata la kariakoo.

Walikusanyana Mafundi mchundo, waka ignore the roles of engeneers, wamwambia bwana mkubwa hili tunaliweza ni chapu tu.

Kilichotokea wote tunakijua, Na haya ndo mazara ya kutumia nguvu nyingi akili kidogo
Mainginia wetu msione aibu kuwa saidia fundi kwenye miradi mikubwa ya wachina kama sehemu yenu sahihi ya practical na internship kupata skills mlizozikisa kwenye vitivo vyenu substandard. Kule mta observe, practice na kupata experience. Waulizeni maswali na mchukue notes. Kupitia wachina mtapata vitu 3 muhimu; knowledge, skills na attitude.
 
Wako more bookish, kukariri kwaajili ya mitihani na kuiba maswali pamoja na chabo nyingi. Kifupi wako more theoretically, kwenye educational psychology hii ya kwao tunaiita rote learning. Majengo ya mkoloni yapo mpaka Leo imara lakini malengo ya hawa jamaa yamejaa nyufa na kuvuja.
Kwahyo hayo yoooote yanaibuka baada ya PM kudis shahada za watu sio?Au mnajaribu kuvalidify kauli ya mhe. Kwakuwa ni desturi yetu wabongo kwamba kiongoz ni malaika?.

Kama kweli tunadhani PM ameongea kizalendo kwanin hajawah pinga ongezeko la mishahara ya wabunge wakati kazi yao ni kusifu?
Na huo mchakato wa kuwalipa wenzi wa viongoz mbona haoni kama ni upotevu wa pesa?.

Tusiwe wepesi wa kudharauliana sis kea sis kwakutaka kuunga hoja za viongoz hata kama ni invalid.

Anyway unawezaje kujiona timamu kudiss products wakati mtaala wa elimu wameufuata kama ulivyo?
 
Hiyo CoET umefanya nn Cha maana Kwa t,
Mkuu hakuna cha maana walicho kifanya maana inategemeana kwako wewe tafsri ya "kitu cha maana ni nini".

Kama kwako wew kitu cha maana ni kutengeneza uchawi, kuuza na kutengeneza unga, kutakatisha fedha na kut**bana tuu basi CoET hawaja fanya cha maana kabsaa.
 
Viongoz wanatakiwa kuangalia kauli zao hyo kauli ya PM imedharaulisha taaluma za watu kichiz sion tofauti yake na dotto magari.
Wasomi/wataalam wangekuwa na roho ya nyegere wange cheza rafu kwenye taaluma zao hasa watu wa afya nadhan tungeelewana vzuri.
 
Aasa
Acha usenge, hapo chuoni kwako mlikuwa wanafunzi wangapi, walimu wangapi, vifaa vya kufundishia vipingapi na wasimamizi wangapi wenye elimu gani wa field practical kuwafanya wote muwe competent kwenye hands on? Uwiano wa wanafunzi na walimu ukoje kwenye kitovo chenu?. Hata serikali yenyewe haiwaamini wahitimu wake, incompetents. Kazi zote wanazoa wachina.
Sasa mkuu kati ya huyo aliyesoma kulingana mwongozo wa serikali na serikali ambayo haiwaamini watu waliosoma mtaala kulingana na miundo mbinu iliyopo chini ya serikali yenyew, yupi hapo umemtukana msenge
 
Tanzania haiishiwi vituko muhitimu wa shahada ya uhandisi mnae msimanga kuwa sio bora ukilinganisha na wa veta, Ndio huyo huyo ambaye nafasi za ajira zikitangazwa veta anaomba na kupata na kuwa mkufunzi wa veta hao mnaowaita bora zaidi.
 
Kwahyo hayo yoooote yanaibuka baada ya PM kudis shahada za watu sio?Au mnajaribu kuvalidify kauli ya mhe. Kwakuwa ni desturi yetu wabongo kwamba kiongoz ni malaika?.

Kama kweli tunadhani PM ameongea kizalendo kwanin hajawah pinga ongezeko la mishahara ya wabunge wakati kazi yao ni kusifu?
Na huo mchakato wa kuwalipa wenzi wa viongoz mbona haoni kama ni upotevu wa pesa?.

Tusiwe wepesi wa kudharauliana sis kea sis kwakutaka kuunga hoja za viongoz hata kama ni invalid.

Anyway unawezaje kujiona timamu kudiss products wakati mtaala wa elimu wameufuata kama ulivyo?
Ukweli hapa PM ni Mtanzania kama sisi, nae anayo haki ya kushangaa kwanini madakatari wamepunguza gharama za wagonjwa kwenda India, SA, UK, Israel, nk kwenda kutibiwa moyo na figo lakini wahandisi miaka nenda hawajawahi kutupunguzia gharama za kuagiza matrekta, baiskeli, vipuli, sindano za kushonea vishikizo wala zip za suruali za wananchi. Kitivo kimebemendwa? Hadi leo kama unataka kujenga kiwanja cha mpira lazima uende china, na kama unataka kadaraja imara kidogo kasikozolewa na tumaji twa tumvua tuchache tu lazima uongee na Rais Xi akupe vijana wake, kwanini kitivo kisivunjiliwe mbali? Kimedumaa.
 
Back
Top Bottom