Kati ya mhitimu wa VETA na mhitimu ya kitivo cha Uhandisi utamwajiri yupi?

Kwa hiyo unataka kusemaje?
 
Namuajiri anaejua Kazi,sijali amesoma wapi ilimradi nikimpa Kazi anafanya nakumaliza,kuna watu kwenye makaratasi vipanga lakini kazini zero
 
Ndio hawa wapuuzi humu wanaandika ujinga wa kuponda Engineers waeleze,labda veta kuna astronauts na aviation Engineers au technicians
Mimi siwaelewi kabisa, ila ninachoelewa ni kwamba spokes za baiskeli yangu zimetoka China na India, hata kengele pia imetoka hukohuko. Angalau madaktari wanasema sasa hivi wanapandikiza figo na kuweka maputo tumboni kupunguza uzito, hawa maenginia wanafanya nini? Janani hata midoli ya watoto wetu mmeshimdwa achilia mbali baiskeli.
 
We jamaa inaonekana hata chuo hujafika wewe
Sijafika chuo kipi? Mimi sijui inginia anasomaje lakini najua inginia anatakiwa aisaidie nn jamii. Jamii inaagiza majembe chapa jogoo kutoka China, hii ni sawa? Jamii inajenga majengo ya serikali yanayopata nyufa muda mfupi TU baada ya kukabidhiwa, yanavuja na yanaanguka mengine. Hii ndiyo sawa?
 
Mbona mifano hai tunayo mkuu.

Rejea sakata la kariakoo.

Walikusanyana Mafundi mchundo, waka ignore the roles of engeneers, wamwambia bwana mkubwa hili tunaliweza ni chapu tu.

Kilichotokea wote tunakijua, Na haya ndo mazara ya kutumia nguvu nyingi akili kidogo
 
Mainginia wetu msione aibu kuwa saidia fundi kwenye miradi mikubwa ya wachina kama sehemu yenu sahihi ya practical na internship kupata skills mlizozikisa kwenye vitivo vyenu substandard. Kule mta observe, practice na kupata experience. Waulizeni maswali na mchukue notes. Kupitia wachina mtapata vitu 3 muhimu; knowledge, skills na attitude.
 
Kwahyo hayo yoooote yanaibuka baada ya PM kudis shahada za watu sio?Au mnajaribu kuvalidify kauli ya mhe. Kwakuwa ni desturi yetu wabongo kwamba kiongoz ni malaika?.

Kama kweli tunadhani PM ameongea kizalendo kwanin hajawah pinga ongezeko la mishahara ya wabunge wakati kazi yao ni kusifu?
Na huo mchakato wa kuwalipa wenzi wa viongoz mbona haoni kama ni upotevu wa pesa?.

Tusiwe wepesi wa kudharauliana sis kea sis kwakutaka kuunga hoja za viongoz hata kama ni invalid.

Anyway unawezaje kujiona timamu kudiss products wakati mtaala wa elimu wameufuata kama ulivyo?
 
Hiyo CoET umefanya nn Cha maana Kwa t,
Mkuu hakuna cha maana walicho kifanya maana inategemeana kwako wewe tafsri ya "kitu cha maana ni nini".

Kama kwako wew kitu cha maana ni kutengeneza uchawi, kuuza na kutengeneza unga, kutakatisha fedha na kut**bana tuu basi CoET hawaja fanya cha maana kabsaa.
 
Viongoz wanatakiwa kuangalia kauli zao hyo kauli ya PM imedharaulisha taaluma za watu kichiz sion tofauti yake na dotto magari.
Wasomi/wataalam wangekuwa na roho ya nyegere wange cheza rafu kwenye taaluma zao hasa watu wa afya nadhan tungeelewana vzuri.
 
Aasa Sasa mkuu kati ya huyo aliyesoma kulingana mwongozo wa serikali na serikali ambayo haiwaamini watu waliosoma mtaala kulingana na miundo mbinu iliyopo chini ya serikali yenyew, yupi hapo umemtukana msenge
 
Tanzania haiishiwi vituko muhitimu wa shahada ya uhandisi mnae msimanga kuwa sio bora ukilinganisha na wa veta, Ndio huyo huyo ambaye nafasi za ajira zikitangazwa veta anaomba na kupata na kuwa mkufunzi wa veta hao mnaowaita bora zaidi.
 
Ukweli hapa PM ni Mtanzania kama sisi, nae anayo haki ya kushangaa kwanini madakatari wamepunguza gharama za wagonjwa kwenda India, SA, UK, Israel, nk kwenda kutibiwa moyo na figo lakini wahandisi miaka nenda hawajawahi kutupunguzia gharama za kuagiza matrekta, baiskeli, vipuli, sindano za kushonea vishikizo wala zip za suruali za wananchi. Kitivo kimebemendwa? Hadi leo kama unataka kujenga kiwanja cha mpira lazima uende china, na kama unataka kadaraja imara kidogo kasikozolewa na tumaji twa tumvua tuchache tu lazima uongee na Rais Xi akupe vijana wake, kwanini kitivo kisivunjiliwe mbali? Kimedumaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…