Father of All
JF-Expert Member
- May 30, 2026
- 458
- 843
Hilo swali hapo juu huwa linanisumbua. Nikiwaangalia wawili tajwa, na;pata taabu kidogo. Kila mmoja anajionyesha kama mwokozi wa taifa letu.
Wawili hawa wametawala siasa za nchi yetu hadi kuanza kuvutia mataifa na mashirika ya nje. Lissu ni mfungwa. Samia ni rais.
Lissu anajionyesha kama mwanasiasa machachari ilhali Samia akijionyesha kama mtawala asiyejali kitu. Ugomvi wao umeligandisha taifa.
Sijui wawili hawa wanafanya wafanyayo kumnufaisha au kumuumiza nani.
Je, sisi wananchi tunawekwa upande gani? Je, inakuwaje nchi yetu igeuzwe mali ya wawili? Tunanufaikaje au kuumia na ugomvi huu usio wa lazima wala wa maana?
Nawasilisha baba yenu.