Kati Ya Vyombo Vya Dola na Viongozi Wa Dini Nani Hapaswi Kujihusisha Na Siasa?

Kati Ya Vyombo Vya Dola na Viongozi Wa Dini Nani Hapaswi Kujihusisha Na Siasa?

and 100 others

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2023
Posts
4,515
Reaction score
14,999
Mimi nijuavyo vyombo vya dola kama polisi, jeshi, na idara za usalama vinapaswa kuwa huru na kutenda kazi kwa misingi ya sheria bila upendeleo. Kujihusisha na siasa kunaweza kusababisha ubaguzi na matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya wapinzani wa kisiasa au raia wa kawaida.

Taasisi za serikali ni kwa ajili ya kuhudumia wananchi wote bila kujali itikadi au chama. Kujihusisha na siasa kunaweza kuathiri maamuzi yao na kuyafanya kuwa ya upande mmoja au kwa maslahi ya kundi fulani badala ya taifa zima.

Kinachoendelea mimi sioni kama viongozi wa dini wanajiingiza kwenye siasa bali ni kawaida wao kama viongozi wa dini iwe Ukristo, Uislamu, Uhindu, na nyingine nyingi hufundisha maadili ya haki, huruma, usawa, na utetezi wa wanyonge. Kwa hiyo, ni jambo la asili kwa viongozi wa dini kusimama kwa misingi hiyo.

Viongozi kama Martin Luther King Jr ,alikuwa mchungaji, Desmond Tutu ambae alikuwa askofu, na wengine wamekuwa mfano wa namna viongozi wa dini wanavyoweza kuwa sauti ya haki bila kuwa wanasiasa.

Kwa kuhubiri haki, viongozi wa dini wanaweza kusaidia kuondoa chuki, ubaguzi, na uonevu, na hivyo kuchangia kujenga jamii yenye amani na mshikamano.

Sielewi mtu anayesema viongozi wa dini wasijihusishe na siasa badala ya kukataza taasisi za kiserikali na vyombo vya dola kujihusisha na siasa, hii tuite ni unafiki.
 
huku kwetu ni tofauti vyombo vinaruhusiwa, had unaambiwa kesi ya mwana ccm na asiye ccm ni tofauti

askari wanajikomba kwa wana ccm, ila wana dini wao wanatakiwa kusema mazuri tu ya serikali ukikosoa umefanya siasa
 
Swali zuri

Ila kwa Wakristo, Yesu kama kiongozi wao alikataa kabisa kuingilia mambo ya siasa

YOHANA 6:15

15. Kisha Yesu, alipotambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.
 
Bongo Hovyo Hovyo Style
Wanaotakiwa Kuwa Neutral Ndiyo Wamechagua Upande Wale Jamaa Halafu Hawana Aibu Kabisa


Dini Zinapokemea Zinatishwa Na Sufuria, Bakuli, Kijiko, Mwiko,,(Vyombo,)
 
Back
Top Bottom