Kati ya waislam na Allah nani muongo kwenye hili?

Muhammad alianza Utume na kuhubiri dini tangu akiwa Makkah vipi unasema alipoenda Madinah ndio akaona aanzishe dini ili apate wanajeshi?

Na kama alikuwa ana tamaa ya kuwa mfalme mbona Maquraish walimuahidi kumpa utajiri na ufalme endapo angeachana na kuwahubiria Dini ya Allah lakini alikataa?
mi nimetoa historia ya mudi kama nilivyosoma kwenye maktaba ya mtandaoni yenye vitabu vingi vya kale(the lost books of eden) kama wewe ni msomaji wa historia na mambo mbalimbali utakuwa unaijui hii maktaba! Sijatoa kwenye bible wala quran sasa wewe unaniletea stori za uongo za kwenye quran eti mudi akapewa utajiri na ufalme akakataa! Kwanza alipewa ufalme wa wapi? Hujui historia wewe! Unachojua ni ilimu dunia na ubwabwa! Kwa taarifa yako huyo mudi wenu historia inamtambua kama mmoja wa wafalme ambae alipata wanajeshi wengi kwa kutumia ujanja ujanja sana! Halafu naona unanijibu kwa mihemuko! Mi nimetoa historia ya mudi na dini yake hiyo!
 
Mimi pia nimekupa historia
 
Kwa mujibu wa mahubiri ya mchungaji wako ?? Kumbe kwa Mungu na yeye si Mungu ?

Hiv una hoja nyingne ukiacha kukana Yesu si Mungu?.
Ina wauma nn?.

Tukubali kutokukubaliana.

Je mna hoja nyingne?.
 
Unazungumzia uislam bila shaka, tuikatae kabisa hii dini ni janga la dunia.

Sijui kama unajua matoleo ya Biblia mengi yaliyopo madukani na yanayogawanywa huko mashuleni sio lile toleo la King David...imesha chakachuliwa.
Na kwa sasa kuna toleo jipya la Biblia lipo jikoni ambapo kuna vifungu kadhaa vimefutwa kwani havina ushahidi wa hadithi za kale umeonekana ni wanafunzi walijitungia...
Mbona hujiulizi kwa nini Yesu ameshindwa kuilinda Biblia unakimbilia kwa Waislam
Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndio uangalia kwa jirani.....
Ona kitu kama hiki kweli?; MUNGU ALIMUUMBA BINADAMU, BINADAMU AKAMKOSEA MUNGU, BINADAMU AKAMPIGA MUNGU HADI MUNGU AKAFARIKI, MUNGU ALIKUBALI KUPIGWA HADI KUFARIKI ILI AMSAMEHE BINADAMU DHAMBI??? huyo Mungu si atakuwa dhaifu sana anakubali apigwe hadi kufariki na kiumbe alichokiumba mwenyewe? Alishindwa nini kumsamehe binadamu kama kweli ana mamlaka yote hadi asubiri apigwe hadi kufariki
 
Maswali yako mazuri ila unaonaje tuanze na mada iliyopo Kisha tunakuja kwenye Maswali yako

Mada iliyopo mlishajibiwa lakini mnakuja na ubishi hata hivyo nakujibu kwa muhtasari baadaye unijibu maswali yangu

Swali​

Surah 6:115 na 18:27 zinaeleza kwamba maneno ya Allah hayawezi kubadilishwa.

Torati (Tawrat) na Injili ni maneno ya Allah.

Kwa hivyo, maandiko ya awali ya Biblia yamehifadhiwa dhidi ya kuharibiwa.

Majibu​

1. Kuelewa Mistari ya Qur’ani​

Surah 6:115:
"Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua.

Surah 18:27:
"…Na soma uliyo funuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hapana wa kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio isipo kuwa kwake.

Katika Uislamu, mistari hii inahusu hasa Qur’ani na funuo za kiungu kwa ujumla. Inasisitiza kwamba ahadi na amri za Allah zinalindwa, na ujumbe wake wa kweli umehifadhiwa.

2. Hali ya Maandiko ya Awali (Tawrat na Injili) katika Uislamu​

Qur’ani inatambua Torati na Injili kama zilivyofunuliwa asili na Allah (Surah 3:3, 5:44-46).

Lakini Qur’ani pia inaeleza wazi kwamba binadamu walibadilisha au kutafsiri vibaya maandiko haya kwa muda:

Surah 2:75:
"…Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wakayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua?

Surah 5:13:
"…Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

Ufafanuzi wa Kiislamu: Torati na Injili awali zilikuwa maneno ya Allah, lakini sasa zimebadilishwa na binadamu, kwa kuongeza, kupunguza, au kutafsiri vibaya.

3. Kanuni Muhimu ya Kiislamu​

Allah anahakikisha ujumbe wake umehifadhiwa, lakini ulinzi huu unahusu kikamilifu Qur’ani tu (Surah 15:9).

Funuo za awali (Tawrat, Zabur, Injili) zilitunzwa wakati wa kufunuliwa, lakini baadaye binadamu waliziharibu, kwa makusudi au kwa kutozingatia.

4.Jawabu kwa wakristo​

Wakristo wanasema: "Ikiwa maneno ya Allah hayawezi kubadilishwa, basi Biblia lazima isiharibike."

Uislamu unajibu:

Ndiyo, maneno ya Allah hayawezi kubadilishwa kwa asili, lakini Qur’ani tu ndiyo iliyo salama kikamilifu.

Torati na Injili zilikuwa na maboresho ya binadamu kwa karne nyingi, ndio maana Waislamu wanategemea Qur’ani kama mwongozo wa mwisho usioharibika (Surah 5:48).

Kwa ufupi: Qur’ani inaonyesha tofauti kati ya maneno ya kiungu kwa asili na nakala zilizobadilishwa na binadamu. Kuwa Torati na Injili awali maneno ya Allah haimaanishi Biblia ya leo ni sawa kabisa na ile ya asili.

Muhtasari

Maneno ya Allah kweli hayawezi kubadilishwa, lakini hii haimaanishi Biblia ya leo ni sawa kabisa na Torati na Injili ya asili.

Qur’ani inafundisha kwamba maandiko ya awali yalibadilishwa au kutafsiriwa vibaya na watu, kwa hivyo Qur’ani pekee ndiyo iliyo salama kikamilifu hadi mwisho wa wakati.

Kwa hiyo, hoja ya Kikristo inadhani kwamba maandiko yalihifadhiwa bila kuharibika, jambo ambalo Uislamu haukubali.
 
😆😅😂Mi nimfate mazinge? Hata Allah mwenyewe simfuati.

Ila we jamaa inaonekana una knowledge, sasa kwa nini unaendelea kuwa muislam?
Sasa mbona umeleta hoja ya Mazinge kama humfuati na humkubali?

Mimi ni Muislam kwa kuwa nimeona ndiyo dini sahihi
 
Kwenye Torat na zaburi ni nini wamebadili , kuongeza au kupunguza?.
 
Sijui kama unajua matoleo ya Biblia mengi yaliyopo madukani na yanayogawanywa huko mashuleni sio lile toleo la King David...imesha chakachuliwa.
Na kwa sasa kuna toleo jipya la Biblia lipo jikoni ambapo kuna vifungu kadhaa vimefutwa kwani havina ushahidi wa hadithi za kale umeonekana ni wanafunzi walijitungia...
Mbona hujiulizi kwa nini Yesu ameshindwa kuilinda Biblia unakimbilia kwa Waislam
Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndio uangalia kwa jirani.....
Ona kitu kama hiki kweli?; MUNGU ALIMUUMBA BINADAMU, BINADAMU AKAMKOSEA MUNGU, BINADAMU AKAMPIGA MUNGU HADI MUNGU AKAFARIKI, MUNGU ALIKUBALI KUPIGWA HADI KUFARIKI ILI AMSAMEHE BINADAMU DHAMBI???
Toleo jipya ambalo lipo jikoni, hebu tueleze vizuri. Jikoni wapi? Hilo jiko linaongozwa na nani? Vifungu gani hivyo vimefutwa? Yaani wanafunzi wa Yesu walijitungia tu! Ni nani sasa mwenye kuweza kuwasahihisha wanafunzi ambao wao walikuwa wapo na Yesu kila anapoenda. Yaani unamaanisha kuna watu wanajua zaidi habari za Yesu kuliko wanafunzi wa Yesu?
 
Back
Top Bottom