Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?

Yaliyopita ni Ndwele kama bado tunaendeleza upuuzi ule ule utakaotu-cost; na badala ya kulaumu waliovunja tulauma walioingia hio mikataba na wanaoendelea kuingia hio mikataba; wakati naambiwa nimlipe huyo jamaa kwanini sikuambiwa vipengele siku anapewa mkataba ?!!!

Shauri yenu,

Dr Ackson Tulia (Daktari Wa Sheria, Mbunge Wa Mbeya, Speaker Wa Bunge, Mgombea Uenyekiti Wa Mabunge Yote Duniani, Mwalimu Wangu Wa Sheria TLS) amewaomba Ma-Chief wawafanyie ulozi na kuwaroga wote mnaopinga mikataba mibovu na sheria mbovu. [emoji219][emoji219][emoji219]

#Huyu Maza Kaanza Kudata![emoji23][emoji23][emoji23]
 
Haya yote yanayotekea ni matokea ya watu wanye mzaa na nchii hii, hu mzaa mzaa Kuna siku utatufikisha pabaya, tutakua na taifa lenye watu walipoteza matumaini na halitakua taifa Tena Bali mbuga ya wanyama.
Viongozi amkeni fanyeni mabadliko yatakayomfanya Kila mtanzania kuwajibika ipasavyo.
 
Viongozi wetu hewa sn aisee, yan mm nikibahatika kuiongoza hii nchi akyaMungu ndani ya mwez mmoja sitomaliza madarakani salama maana nitatekeza fangasi wte waliowahi kipindi change Nyuma na wte watakaoendelea kusababishia taifa letu hili hasara yn kila mwehu aliyewahi kutumia akili zke timamu kututia hasara lzm ataregret to the max... I swear to God and may God the creator give me such power to conquer the evil deeds [emoji298]
 
Wanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazima tulipe.

Haya yote ni matokeo ya kazi ya wanasheria wabovu na baadhi yao vilaza!. Leo nimeianza siku kwa bad news kutoka Marekani, Tanzania tumeshindwa kesi, tunadaiwa tozo ya dola za Marekani zaidi ya Millioni 100!, na lazima tulipe!.

Soma taarifa hii hapa chini
View attachment 2692021
  1. Kama Tanzania tulipitisha sheria kuwa kwenye uwekezaji hakuna mashauri yoyote ya nje ya nchi!. Mashauri yote ni hapa nchini kutumia sheria za Tanzania!, sasa haya mashauri yanaendelea vipi kupelekwa nje?.
  2. Hii maana yake ni ama tuna sheria mbovu, ama tuna wanasheria wabovu wanaotunga sheria mbovu, zinazotupa mikataba mibovu, na mwisho wa siku tunaishia kupigwa na kutozwa matozo ya ajabu ajabu!.
  3. Huku kila siku kushindwa kesi za kimataifa na kupigwa tozo nako ni ama tuna sheria mbovu za mikataba mibovu ama kama sheria ni nzuri, then tuna wanasheria wabovu wasio na uwezo wa kushauri the right thing to do!, hivyo serikali yetu inavunja mikataba kitutusa na mwisho wa siku tunaishia kuumizwa kwa kushindwa kesi na kupigwa tozo!.
  4. Kabla ya kuvunja mkataba wowote, serikali yetu inaomba ushauri wa kisheria kufanya kitu kinachoitwa mitigation, wanasheria hawa huishauri vibaya serikali yetu, mwisho wa siku, tunaishia kuumizwa!.
  5. Issues ya Richmond, Dowans, tukaunda tume, ikatoa matokeo kwa mbwembe kuwa Richmond ni kampuni hewa hata tukivunja mkataba, hatutashitakiwa popote!.
  6. Tukamfanya Edward Lowassa ni mbuzi wa kafara, tukavunja mkataba!.
  7. Tukashitakiwa tukashindwa, tukapigwa tozo!. Waliotushauri tuvunje mkataba wakajiapiza "over my dead body!, hatulipi". Tulilipa kisiri siri every cent!. Hawa wanasheria walifanywa nini?
  8. Mitambo ya Richmond ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule na tukawalipa!.
  9. Chuma JPM, alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, tukapigwa tozo, Chuma JPM, akagoma hatulipi!
  10. Mama kaingia, tumelipa fasta fasta, kimya kimya!. Wanasheria waliotufikisha hapa walifanywa nini?!.
  11. Tulipotunga sheria mbovu, watu humu tulishauri Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?, leo baada ya kutuletea hii IGA mbovu, watu tumeeleza matatizo yake kibao!.
  12. Wanasheria hawa hawa, Bunge letu hili hili wanaipitisha hivyo hivyo ilivyo, wanaiambia serikali yetu hii IGA ni nzuri, safi na haina matatizo yoyote!.
  13. Wanasheria hawa wanao tufikisha hapa, tukiwaita ni wanasheria wabovu au vilaza, itakuwa ni kuwaonea?.
  14. Tanzania tutaendelea kufanywa shamba la bibi na kichwa cha Mwendawazimu na wanasheria wabovu na vilaza wa aina hii hadi lini?!.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
Tunaposema tatizo la nchi hii ni ccm muwe mnaelewa. kwamba kwa miaka 30 ya mikataba mibovu, serikali ya ccm haijapata uzoefu wa kunegotiate mikataba? si kweli

Kuna watu ndani ya ccm ndiyo wanawaelekeza hata hawa wawekezaji kufanya mikataba mibovu na baadaye watu haohao wanashawishi mikataba ivunjwe, kisha wanawashawishi wawekezaji waishtaki tz, faini zikitoka wanakula cha juu.
 
Iwe ni marufuku miaka miwili kabla ya Uchaguzi Mkuu Serikali kuingia Mikataba ya aina yeyote ile na wawekezaji wenye mapato zaidi ya Serikali yetu. Vilevile, Serikali isitishe kuikopea miradi yeyote ile yenye ubia na sekta binafsi, yaani isifanye kuwakingia(Insure) wawekezaji wowote wale wanaohusishwa na kuchangia Uchaguzi- miaka miwili ya mwisho kabla ya Uchaguzi.

Watakao kiuka wanyongwe hadharani
 
Wanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazima tulipe.

Haya yote ni matokeo ya kazi ya wanasheria wabovu na baadhi yao vilaza!. Leo nimeianza siku kwa bad news kutoka Marekani, Tanzania tumeshindwa kesi, tunadaiwa tozo ya dola za Marekani zaidi ya Millioni 100!, na lazima tulipe!.

Soma taarifa hii hapa chini
View attachment 2692021
  1. Kama Tanzania tulipitisha sheria kuwa kwenye uwekezaji hakuna mashauri yoyote ya nje ya nchi!. Mashauri yote ni hapa nchini kutumia sheria za Tanzania!, sasa haya mashauri yanaendelea vipi kupelekwa nje?.
  2. Hii maana yake ni ama tuna sheria mbovu, ama tuna wanasheria wabovu wanaotunga sheria mbovu, zinazotupa mikataba mibovu, na mwisho wa siku tunaishia kupigwa na kutozwa matozo ya ajabu ajabu!.
  3. Huku kila siku kushindwa kesi za kimataifa na kupigwa tozo nako ni ama tuna sheria mbovu za mikataba mibovu ama kama sheria ni nzuri, then tuna wanasheria wabovu wasio na uwezo wa kushauri the right thing to do!, hivyo serikali yetu inavunja mikataba kitutusa na mwisho wa siku tunaishia kuumizwa kwa kushindwa kesi na kupigwa tozo!.
  4. Kabla ya kuvunja mkataba wowote, serikali yetu inaomba ushauri wa kisheria kufanya kitu kinachoitwa mitigation, wanasheria hawa huishauri vibaya serikali yetu, mwisho wa siku, tunaishia kuumizwa!.
  5. Issues ya Richmond, Dowans, tukaunda tume, ikatoa matokeo kwa mbwembe kuwa Richmond ni kampuni hewa hata tukivunja mkataba, hatutashitakiwa popote!.
  6. Tukamfanya Edward Lowassa ni mbuzi wa kafara, tukavunja mkataba!.
  7. Tukashitakiwa tukashindwa, tukapigwa tozo!. Waliotushauri tuvunje mkataba wakajiapiza "over my dead body!, hatulipi". Tulilipa kisiri siri every cent!. Hawa wanasheria walifanywa nini?
  8. Mitambo ya Richmond ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule na tukawalipa!.
  9. Chuma JPM, alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, tukapigwa tozo, Chuma JPM, akagoma hatulipi!
  10. Mama kaingia, tumelipa fasta fasta, kimya kimya!. Wanasheria waliotufikisha hapa walifanywa nini?!.
  11. Tulipotunga sheria mbovu, watu humu tulishauri Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?, leo baada ya kutuletea hii IGA mbovu, watu tumeeleza matatizo yake kibao!.
  12. Wanasheria hawa hawa, Bunge letu hili hili wanaipitisha hivyo hivyo ilivyo, wanaiambia serikali yetu hii IGA ni nzuri, safi na haina matatizo yoyote!.
  13. Wanasheria hawa wanao tufikisha hapa, tukiwaita ni wanasheria wabovu au vilaza, itakuwa ni kuwaonea?.
  14. Tanzania tutaendelea kufanywa shamba la bibi na kichwa cha Mwendawazimu na wanasheria wabovu na vilaza wa aina hii hadi lini?!.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
Leo wewe umewageuka wenzio?
 
Kuna wakati tutaoshuhudia nchi inauzwa na hatuna cha kwetu tena.
Aisee,mbona tulishaoonywa? Unafikiri Spika aliyestaafishwa Job Ndugai aliyasema yale hivi hivi tu? Mjue wakati vinapikwa viongozi kama spika wanakuwa na ndoondo za ki-aina, alisha ona huku kwa DPW
Nchi ishauzwa, manake ukiondoa Bandari tu huna lwako, yaani uachie asilimia 40%ya mapato yako chini ya Mkoloni....utapona kweli?
 
Hahahahaaa.... Na hakika kumbukumbu hazipotei.
 
Tanzania tutaendelea kufanywa shamba la bibi na kichwa cha Mwendawazimu na wanasheria wabovu na vilaza wa aina hii hadi lini?!.

Ungewataja majina anza na yule anaitwa Fenesi sijui Felesi
✍️
 
Back
Top Bottom