Katiba Mpya au Chama Kipya? Je, Tunataka Kubadili Mfumo au Viongozi?

Samia sio kiongozi bora , kumtolea mfano sio sahihi
 
Sijui kama wengi wetu tutakuelewa ila una hoja ya msingi.
 
Sijui kama wengi wetu tutakuelewa ila una hoja ya msingi.
Shukran mkuu hoja ipo
Asante kwa kuliona hilo

Mimi binafsi nikifatilia mijadala hapa jukwaani
Napata mashaka na kitu wengi wetu tunachokitaka na ukiangalia mijadala bila kua na mihemko utagundua ninachokuambia

Kwenye uzi kama huu pia huwezi kuwakuta abadani wale wanazi wa vyama
 
Viongozi bora.

Ukiwa na kiongozi mzalendo kwa nchi na ana akili kubwa, katiba sio ishu sana ila ukiwa na viongozi wapuuzi hata ukiwa na katiba nzuri vipi haina maana yoyote, ndicho kinawakuta Marekani.
Katiba ina maana mkubwa sana, Marekani wanaweza kuweka chama fulani lakini ubora wa katiba yao unawapa wanafasi ya kubadili hao viongozi wapuuzi. Tanzania wananchi hawana nafasi ya kubadili kiongozi mpuuzi mpaka wapuuzi wenzake wakae na kuamua kumchomoa huyo mpuuzi kwa sababu anawaharibia katika ulaji.
 
Marekani inasaidiwa zaidi na utawala wa majimbo mengi yenye mamlaka karibia sawa na nchi,
 
Imagine Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi
Anachaguliwa na mwenyekiti wa ccm

Yaani hili hata mtoto wa darasa la pili linaweza kumshangaza sana

Waliotunga hizi kanuni aiseee
Nchi zilizo endelea kisiasa wanafanyaje kupata tume ya uchaguzi tuangalie hilo tujifunze?
 
Katika Tanzania kuna ushindani. Kila kitu ni usimba na uyanga au uccm na uchadema. Vyama havina itikadi ni huyu anasema katiba mpya na huyu anasema hapana.

Ukweli Madai ya katiba mpya ni kuwa Samia anayefaidi keki ya taifa na familia yake, atoke ili na sisi tufaidi.

Katiba mpya ni ile itakayopunguza mamlaka ya Rais full stop. Jiulize katika hali ya Leo na uchawa ulivyo, ni binadamu yupi atakubali kujinyonga kwa mbeleko yake.

Kuna njia za kufikia katiba mpya nayo ni kuanza na mgombea huru. Ukisema hilo, hata chadema wanakataa.

Ni uhuni tu!
 
Dada mtoa mada kusema ukweli mifumo wetu wa kiongozi umekua mbovu Sana sasa Katiba ni muhimu zaidi irekebishwe kwanza ili kuweza kuweka utaratibu mzuri wa uongozi ili Kila mtu awajibike vizuri kwenye majukumu yake na pia Katiba ikiwekwa sawa naamini itatupa nguvu sisi wananchi kuweza kuwawajibisha vizuri wale viongozi watakao enda tofauti na utaratibu maana kwa sasa sisi wananchi tunajiona hatuna nguvu kabisa katika maamuzi ya Nchi hii yaani viongozi wanafanya wanavyotaka wao sasa tukipata Katiba nzuri itatlsaidia Sana haijalishi viongozi watakua CCM au Chadema lakini Katiba mpya itaweka mambo mengi vizuri na sisi wananchi tutajiona ni sehemu ya Nchi hii maana saivi wananchi tupotupo tuh hatuna maamuzi yeyote yale hata nyie si mmeona uchaguzi watu wamejifanyia wenyewe na wameshinda.
 
Kuna mifumo ya uengenezaji katiba mpya. Bila hiyo mifumo ambayo inazuia watengeneza na wapitisha katiba kujinufaisha katika katiba mpya, huwezi pata katiba mpya bora ila bora katiba mpya. Mfano, mtayarishaji na mpitisha katiba inatakiwa asiruhusiwe kugombea yeye na mweza wake cheo chochote kwa muda wa miaka 20.
 
Nchi zilizo endelea kisiasa wanafanyaje kupata tume ya uchaguzi tuangalie hilo tujifunze?
Tume huru huanzia kwenye Katiba bora na sheria imara zinazolinda uhuru wake, zikifuatwa na utekelezaji wake kwa vitendo.
 
Kuanza na mgombea huru asiefungamana na chama chochote

Kwanini unadhani hata chadema wanakataa hili?

Mimi niligundua kitambo kuhusu hili kua issue sio katiba tu wengine nao wanataka kufaidi kama watangulizi nasema hivyo kwa sababu

Kuna wakati viongozi pinzani huonekana wameboronga ila hua hawataki kuhojiwa na hizi ni tabia za wenye madaraka kwa sasa

Kwahiyo kuna tabia ni sawa sawa ni kwa vile wengine hawana uwezo wa kuonesha reaction yao kama upande uliopo mezani
 
Upo sahihi tukiwa na katiba mpya tena bora basi kuna kero zitatuliwa
 
Sasa hivi, watu wanaogopa kusema ukweli kwa kuzibwa midomo na suala la kudhaminiwa na chama. Ukiwa tofauti na chama, unafukuzwa na ukifukuzwa katika chama na nafasi yako imeondoka. Mfano Nchimbi. Kama mgombea huru angekuwa anaruhusiwa, angekuwa bado katika nafasi yake na moto ungewaka. Nakuhakikishia kwa sasa ndani ya bunge akina Nchimbi wapo wengi ila kikwazo ni kuogopa kuchukuliwa kadi.
 
Katiba ni kakijitabu tu, especially kama watanzania hatutabadilika from within.

Nimependa maneno ya Nyerere, naamini bado yanaishi, if we're to move forward as a nation
1. Siasa safi, huwezi kuitoa katiba kwenye hili. The whole Tume ya taifa ya uchaguzi needs to be overhauled, hakuna kitu pale, mode ya uchaguzi needs to change, wateuliwa wa raisi ambaye ni mwenyeketi wa chama ndio wasimamizi wa uchaguzi, that's bullshit.
2. Watu, bongo kali(aliandika), bila attitude yetu kubadilika individually expect nothing to change.
3. Ardhi, maendeleo bila rasilimali ardhi hakuna.
4. Uongozi bora, tuna mengi ya kufanyia kazi wakuu, as a nation we're doomed wala sio utani.
 
Ni kweli ukinyanyua ulimi unawekwa pembeni iwe chama tawala au kwa wapinzani

Ila kwa Nchimbi sijui nisemaje!
 
Shukran sana kwa maoni mazuri babu 🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…