Naomba kuchangia hoja hapa.
Mimi Kwa maoni yangu, Mchango wangu wa kisomi na kitaaluma katika Jambo hili ni kwamba Katiba yetu ya sasa ni dhaifu sana kiasi ibara zake ni bora na zinaweza kuleta maendeleo kwa kionhozi mzalendo na pale anapotokea kiongozi mwenye maslahi binafsi utumia katiba hiyo kudhoofisha misingi ya taifa, Demokrasia, na kukipendelea chama chake pia.
Hivyo basi Hoja ya mabadiriko ya katiba ni muhimu zaidi kuliko tamanio la kwamba Chama kingine kishike madaraka kama hamu ya kuona mabadiriko ya uongozi katika ngazi za kisiasa na vyama vya siasa, hoja muhimu zaidi pia ni pamoja na Vyama hivyo vipewe dhamana na wanananchi lakini katiba ikiwa dhaifu itachangia jamii kuona kwamba chama tawala kinaminya demokrasia ya kisiasa hili kujibakisha madarakani, lakini katiba ikiaeka wazi na kuweka usawa na usimamizi basi wananchi watakuwa huru kuchagua kile watakacho na kitakuwa hivyo basi hoja si chama fulani kitoke madarakani, hoja ni
je, kipo madarakani kihalali.? Hapo sasa ndipo katiba inaingia na kujibu swali hilo naomba kuwauliza swali zito na la kisomi kabisa na Naona ni muhimu kuliuliza swali hilo hili kupata jibu la swali la hapo awali, ambalo ni
Je, Kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 1977 kuna Mamlaka yaliyowekwa yenye Jukumu la Kusimamia Ufuasi wa Katiba.?
JIbu nitakalolitoa na ni Ndio ukweli wenyewe ni kwamba,
Hakuna Mamlaka hayo Chini ya Muhimili wowote hule iliyowekwa na Katiba ya Mwaka 1977.
Kutokana na hoja za uzi huu, na hamu yangu ya kuona Taifa Letu linakuwa na Muundo Bora na wenye Kutoa Majibu ya Maswali yote kama haya, nikaona ni muhimu Sana kuchangia mada hii na kwasababu Ndani ya Rasimu ya katiba niliyoitoa kama Maoni Kwa Umma imeweka Muundo bora na kuweka Mamlaka hayo Chini ya Muhimili wa Nne "
Baraza la Usimamizi wa Taifa", nimeona nitoe muongozo kidogo Kuhusu Rasimu hiyo ya Katiba.
Katika pendekezo la Katiba linalopatikana kwenye Tovuti ya
www.katibampya.com Imeanzisha Muundo wa Dola Lenye Mihimili Minne ya Kitaifa, Yaani.
1.
BARAZA LA USIMAMIZI WA TAIFA ( Muhimili wa Usimamizi wa Misingi yote ya Taifa, Mamlaka ya Kimuungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, Mamlaka yenye Jukumu la Kutoa Tathimini zote za Kitaifa na muongozo, Mlinzi wa Demokrasia, Mamlaka ya Usimamizi wa Ufauasi wa Katiba, Tunu za Taifa, Maadili ya Taifa na Mengineyo mengi.)
2.
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (Muhimili wa Utendaji, Utekelezaji wa Sera za Taifa, Dira ya Taifa, Ulinzi na usalama wa Taifa, Mamlaka yenye Dhamana ya Uwakilishi wa kimataifa, na Mengineyo mengi.)
3.
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (Muhimili wa Uwakilishi wa Wananchi katika ngazi za Majimbo, Mamlaka ya kutunga Sheria, kupitisha Bajeti zote za Taifa, mijadala ya Muelekeo wa Taifa, na ni Mamlaka yenye Dhamana ya Uwakilishi wa Demokrasia ya Kisiasa Kwa hoja na ukosoaji Chanya.)
4.
MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA(Muhimili wa Utoaji Haki, Hukumu za Kisheria, Matatizo wa migogoro ya Kikatiba na Kisheria, na Ndio Mamlaka ya Mwisho kabisa ya utafasiri wa Katiba na Sheria za Nchi.)
Muundo Huu imetoa Majibu ya Maswali kalibia yote yanayolikabili Taifa Letu Hivi Leo na Napenda kusema kwamba Mamlaka hayo ni Baraza la Usimamizi wa Taifa ambalo limetamkwa Katika
SURA YA NNE kuanzia Ibara ya 98 mbaka ya 116, Hivyo Basi Majukumu, Muundo, Mamlaka, na Mipaka ya Baraza yametamkwa kwenye Ibara Hizo.
Pia Muundo Huu wa Dola hasa Uwepo wa Mihimili Minne ya Kitaifa imetoa Jibu Lenye Muundo Bora juu ya madai ya Katiba yenye
Serikali Tatu, Kwa maana Rasimu hiyo haijaweka
Serikali Tatu Bali
imeweka Baraza la Usimamizi wa Taifa ambao Ndio Muhimili wa Nne na ndio Muhimili wa Usimamizi wa Misingi yote ya Taifa na pia Ndio
Mamlaka ya Kimuungano Kwa Pande zote mbili za Muungano, Yaani hoja Kuu si Uwepo wa Serikali Nyingi, Bali hoja ni Uwepo wa Mamlaka yenye Nguvu ya kutoa Tathimini, muongozo na kusimamia Misingi ya upande Husika wa Muungano, hoja hii unapewa Nguvu na swali la Kikatiba linalosema Ikiwa madai ya Katiba Mpya ni utaki wa Uwepo wa Serikali Nyingi. swali ni
Je, Serikali Hizo nitakuwa na Nguvu ya Namna Gani ili zisiweze kuvutana ua kushindana? Pia swali lingine ni
• Je, nini kitatokea Endapo Pande zote Tatu za Serikali zinakuwa na Marais wa Vyama vya Siasa vinavyovutana Kisiasa na kuzaa uhasama wa itikadi za Vyama hivyo?
• Je Usalama wa Taifa utakuwa Kwa Kiwango Gani?
• Je migogoro hiyo itatatuliwa na Nani.?
Maswali kama haya ni mengi sana na kila mtu anaweza kuwa na maswali yake yanayoendana na haya na maswali hayo Ndiyo yanayolipa Hadhi
Baraza la Usimamizi wa Taifa kama Chombo kimoja, Taasisi moja na Kwa lugha rahisi ni Sawa na kusema "
Baraza la Usimamizi wa Taifa ni Mamlaka ya Kimuungano iliyounda Muundo wa Muungano wa Taasisi moja ya Kitaifa Yenye Hadhi ya kuweka Usawa wa Kimuungano Kwa Mihimili mingineyo yote"
Ndani ya Baraza la Usimamizi wa Taifa hasa Kuhusu Mamlaka ya Kimuungano kuna Taasisi mbili za Ushauri wa Kitaifa kutoka Kila upande wa Muungano Ambazo ni:
1.
Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
2.
Tanganyika Social Council.
Taasisi hizo zinaongozwa Kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa ambayo ni Sheria ya Usimamizi wa Taifa na pia Chini ya wenyeviti wake ambao ni
Marais wa Baraza la Usimamizi wa Taifa kutoka Kila upande wa Muungano wanopatikana Kwa Kura za Maoni na si wanasiasa, itikadi za Kisiasa wala Awana uwanachama wa Chama chochote cha Siasa.
Pia ndani ya Rasimu hiyo ya katiba kqenye ibara ya 176 imeanzisha "
Mchakato wa Utjibitisho wa uhalali wa Madaraka na kupingwa kwake" Mchakato huo unamaana kwamba Hakuna anaeweza kuapishwa kuwa Rais, Mbunge au Diwani isipokuwa Athibitishwe mbele ya
Mahakama ya Katiba Juu ya kura zilizopigwa, sifa na mengineyo mengi.
Kiufupi uthibitiaho huwo unawawezesha vyama vyote kuwa na mawakala kila kituo cha kupiga kura, kuhesabu kula zao wao wenyewe lakini awaruhusiwi kujitangaza kabra ya tume kutangaza matikeo, kisha kila chama kitatoa kiapo chake mbele ya
Tume ya haki jinai na usimamizi wa sheria Ambapo kiapo hicho
kitakuwa ni cha Kukubariana na matokeo ya kura za ngazi zote au
Kutokukubaliana na Matokeo kwa baadhi ya Ngazi za wagombea wao. Kama endapo Kiapo kitakuwa ni cha Kutokukubaliana na matokeo basi wanakuwa na haki ya kufunguwa shauri mbele ya mahakama ya katiba na ngazi husika ikiwa ni urais, ubunge au udiwani utakuwa na uchunguzi wa siku 30 mbaka 71, shauri hilo mbele ya mahakama litakuwa na hadhi ya ushaidi uliowekwa kwenye ibara ya 176, 212 na 213.
Pia kuna Tume huru ya Uchaguzi kwenye ibara ya 212
Naomba nifunge hoja zangu kwamba, Katiba yetu ya mwaka 1977 Haina Mamlaka ya Usimamizi wa Ufuasi wa Katiba hivyo Basi Katiba inapovunjwa inachukua ugumu Sana Kwa Mwenye kuivunja kuwajika ama kuwajibishwa hasa pale ambapo Yule anaeivuja anapokuwa na Madaraka makubwa.
Rasimu kamili hipi kwenye tovuti ya
www.katibampya.com na Napenda Kuwasilisha kwenu Hoja zangu na Bandiko Hili Kwa Ujumla, ni Mimi
mrxtz2026