Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Kama wananchi hawataiona ccm kama ndio sababu ya wao kuwa maskini wa kutupwa, basi tusubiri hadi Yesu alete nabii wa kuwafunulia.Kwanini walianzisha mchakato ambao umetafuna fedha za wananchi maskini wa taifa hili?Iko siku watawajibika kwa wanayoyatenda.
 
Waliotoa maoni ya serikali tatu ni asilimia 64 kwa mujibu wa Tume , so wewe hao wanyongwe unaosema ni hao wajumbe wa NEC au?

Asilimia 64 ya asilimia 26 waliozungumzia kuhusu Muungano
 
Hayo ni maoni ya ccm sio maoni ya watanzania,

Watanzania 64% wametoa maoni yao mbele ya tume ya mzee wetu Warioba kuwa wao wanataka muungano wa serikali tatu.

Maoni ya umma wa wengi yaheshimiwe,
 
Sawa kabisa serikali mbili tu, anayetaka tatu ahame nchi. Cha msingi marekebisha katiba ya zanzibar na ya muungano kukidhi mapendekezo mengine chanya katika rasimu sio kubomoa badala ya jujenga. Kwanza Warioba kazi yake kashamaliza lakini anaendelea kuwafanyia kazi kina Jussa utadhani katumwa.
 


Wewe ni mmoja kati ya MAADUI wa Zanzibar.
 
Naona dalili za kupata katiba mpya sasa zimeeanza kuonekana mapema serikali mbili ndiyo mpango mzima ndiyo zimetufikisha hapa tulipo.
yes zimetufikisha hapa kwenye huu umasikini chini ya jemadari KJ
 
Kwa namns hii, hili BUNGE la KATIBA halina maana tena, maana kwa jinsi lilivyoudwa ki-CCM basi maamuzi ya NEC ndiyo yatakayopita. Inaniuma sana jinsi tulivyoingia gharama zisizo na msingi, tumeunda TUME ya kukusanya MAONI, na sasa tumeunda BUNGE la KATIBA, yote haya ni ufujaji wa pesa, kupoteza muda na dharau kubwa kwa wananchi.
 
Kweli ccm hamna aibu! Tumetumia muda mwingi kuelezea kwa nini tunataka serikali 3 leo mnatudharau? ngoja mtaona joto ya jiwe. Mlikuwa wapi wakati znz wanavunja katiba kwa kutangaza mipaka, wimbo n.k.
 
kama naona Muamsho vile wanajipanga?maoni ya wengi kuachwa ni dalili tosha ya mabavu,
 
Naamini wanaotaka serikali mbili watashindwa......time will tell.
 
mtu akikutukana kuwa una akili kama ya ccm, ujue ni tusi kubwa sana.

ngoja waipitishe bungeni halafu tuikatae kwenye kura za maoni. hivi hawa maccm hawakujufunza kenya? duh inaskitisha kweli?
 
Mimi sioni kama wamehamua vibaya, hata mimi hapa siyo mwanaccm lakini nataka serikali mbili yaani Serikali ya Zanzibar na Serikali ya TANGANYIKA basi

 
Nikijibiwa maswali haya 99 nitaacha kuidai Tanganyika, naanza na maswali matano.... 1. Waziri mkuu wa JMT huwa anaenda ZNZ na kushughulika na miradi ya maendeleo? 2. ZNZ kwenye maboresho ya katiba yao waliitambua ni nchi na mkuu ni Rais, Rais wa Tanganyika yu wapi? 3. Wabunge kutoka bara wapo ZNZ? 4. Mawaziri toka bara wanachaguliwa ZNZ? 5. M-ZNZ RUKSA KUMILIKI ARDHI BARA, JE MTZ BARA KWA NINI SIO RUKSA KUMILIKI ARDHI ZNZ? Kuna usawa hapo? Ukweli ni kwamba Nchi kama Marekani ni Muungano wa nchi nyingi tu lakini ni utaratibu tu... Ni bora niambiwe Tanganyika na ZNZ zina mawaziri wakuu na Rais ni 1 wa JMT kuliko Muungano wa nchi 2 zenye serikali 2
 
kulikuwa na haja gani ya kuunda tume ya kupita na kukusanya maoni kwa wanachi ikiwa maoni ya ccm ndio yanayofaa kuwa katiba ya tanzania?
 

Hii nchi si mali ya CCM bali ni mali ya watanzania wote na ndio wenye maamuzi.

Swala la katiba linaweza kupelekea ghasia na vurugu zitakazomuondoa JK madarakani.

Tumechoka kuendeshwa na hili genge la watu wachache kwa maslahi yao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…