Pre GE2025 Katibu Mkuu CCM, Balozi Dkt. Emmanueli Nchimbi amehitimisha ziara ya siku mbili mkoani Singida kwa kusambaratisha hoja zote za Lissu za kibaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu angekuwa anapendwa na kuungwa mkono angekuwa kanunuliwa gari mpaka muda huu.

Embu fikiria kama watu laki moja tu wangechangia elfu moja moja maana yake mpaka sasa angekuwa amepata millioni mia moja.yaani

1000x100,000=100,000,000/=

Sasa cha ajabu hata watu elfu sita hawajafika katika wale waliomchangia. Sasa anapendwa na akina nani hao? Ukute hata wewe ni mnafiki tu mkubwa umegoma kumchangia.
 
Bila picha hainogi tafta na picha weka
 
Bwana lucas pole sana, ila uchawa si kazi kwakweli, i feel chngamoto zako ni ngumu
 
Watanzania bado wanasubiri majibu ya hoja za Lissu! Michango ya gari kake inaendelea.
 
Lissu Hana Hoja Zaidi ya Kauli za kibaguzi na chuki zake zinazotokana na kukatalika na watanzania.
Mkuu wewe ndiye mwenye shida ama ya uwezo wa kufikiri au unafanya makusudi kwa sababu Tundu Lisu kastate facts in accordance to the two constitutions na Samia hajawahi kukanusha.

Mkuu wewe tu na kimbele mbele chako mbuzi, umejipachika msemaji wa Samia na CCM kinyume na utaratibu wa ajira ya CCM na kuleta porojo ushuzi usio na mashiko kikatiba!!!

Kama wewe kweli ni muumini wa hoja kujibiwa kwa hoja basi kwa kuzingatia katiba zote mbili jibu hoja hizi 5 za Tundu Lisu:

1. Je, rais Samia kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar sio Mzanzibari??

2. Sema kweli kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, Zanzibar sio nchi???

3. Sema kweli kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, mtangayika anaruhusiwa kuajiriwa na serikali ya Zanzibar au kumiliki Aridhi Zanzibar!???

4. Sema kweli kwa mujibu wa katiba ya JMT nani anasimamia mambo ya Tanganyika ndani ya Muungano kama ilivyo kwa Zanzibar.

5. Sema ukweli kwa mujibu wa katiba ya JMT kina nani ndio wawakilishi wa Tanganyika kwenye bunge la Tanzania kama ilivyo kwa Zanzibar ???

Na kama kwa kusema hayo Tundu Lisu anachochea ubaguzi kwa nini JMT isimfungulie mashtaka na sio kupanda majukwaani kupangua hoja zake.

Lucas ukijibu hoja hizo alizo hoji Mheshimiwa Tundu Lisu kwa usahihi, tutaamini kweli Lisu anasambaza ubaguzi na chuki, tutakabiliana naye wenyewe bampa to bampa.

Kama hutaweza, maneno yako yatabaki kuwa porojo ushuzi tu! Muda ukifika utatulia kama Musiba!
 
Usimlinganishe Galileo na hizi pumba zako unazojaza humu. Galileo alikuwa mtafiti tofauti na wewe unayesifia viongozi ili utupiwe makombo.
 
Yeye kaenda na kaondoka, Lisu ni kwao, hivi yuko njiani kuelekea Singida na gari lililoshambuliwa kwa risasi. Mwambie Katibu wako arudi wafanye mdahalo.
Nchimbi ni mtupu hana uwezo wa kuchegama na Lissu kujenga hoja.
 
Sasa ndio utuambie amesambaratisha kwa hoja gani?sio porojo tu.

Katika machawa watakao chelewa uteuzi ni wewe.

Una ngonjera nyingi sana zisizo nanfacts wala ushahidi.

Jifunze kwa hiki kitoto ChoiceVariable japo chenyewe kina screeshort tu hata takataka.
 
Umempiga spana kaka harudi hapa nakuambia

Yaan katika machawa wasio na facts na watachelewa sana kuteuliwa ni huyu Luca ass.

Viongozi wake wanaona alivyo mwepesi na pumba nyingi
 
Hoja hazisambaratishwi kama kupuliza majivu ya mabua halafu yachafue mashati na blauzi za watu.Siyo hivyo!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Amesambaratisha hoja za ubaguzi wa kikabila na maeneo kinyume kabisa na maadili ya Nchi hii kama waasis walivyoturithisha.

Wananchi wamekataa ubaguzi wa omba omba Lisu maana mnaowaona wanachinjama chanzo ni Hawa vibaraka wa Ulaya,wakati mnachinjana wao watakimbilia Ubelgiji,Ulaya na Marekani Kwa bwana zao huku Wana wazoom kusema ona Hawa nyumbu πŸ˜†πŸ˜†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…