Katika dunia ya sasa, mheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Lazima maneno yapate nguvu kwa maana binadamu hawana jema mkuu.
 
Kwakweli mimi habari za kutembeleana huwa sitaki kabisa . Sipendi kabisa kwenda majumba ya watu na hata nikienda nakaa dakika 10 tu, labda kuwe na sherehe au msiba

Wengine hujifanya kuja kukusalimia ila ni umbea tuu kutaka kujua unaishije.
 
Mimi tumezaliwa wawili kwetu ila tunakaa miezi mnne hatujapigiana simu, ila wote tuna wasiliana na mama, mama yangu kwao walizaliwa wanne wamebaki wawili nao pia hawawasiliani, mara ya mwisho kwenda kwa uncle na mama mkubwa ilikua 2001, huwa hatupigiani simu labda itokee kuna tukio kama msiba au harusi, cousins na nephews hakuna tunayewasiliana kama hamna tukio, baba yangu alifariki tukiwa wadogo so hatujawahi kuwa na ukaribu na upande huo, familia yetu kila mtu na marafiki zake unaweza kufa ikapita mwaka na ndugu wasijue, kwetu undugu hakuna na hatuna bifu tukikutana ni salamu na bia mbili tunaachana tutakutana baada ya miaka mingi, ikifika xmass huwa naumia natamani na sisi tungekua familia kubwa tukutane tusherekee ila ndio ishakua hivi, nakumbuka siku ya graduation yangu alikuja bimkubwa peke yake tulipotoka kwenye mahafari tukarudi nyumbani akanipa mpunga nikasherekee mtaani, nikaenda kwa mshikaji wangu nae alikua amegraduate nikakuta sherehe na ndugu wengi nilitamani sana

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Undugu wakati mwingine ni lawama tu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…