Katika hali ya kawaida Makonda hana raha kabisa

Katika hali ya kawaida Makonda hana raha kabisa

Binafsi sioni tatizo kubwa kwenye hii clip....naona tujikite kwenye zile za uvamizi wa kituo na mauzauza mengine.
Hiyo clip itakuwa hujaifahamu. Mleta hiyo clip.anasema kuwa huyo aliyekuwa ananyooshewa kidole na kupewa onyo kwa sasa ni Katibu Mkuu wa CCM. Kawa bosi wake Makonda x1000
 
hamna cha kumfanya makonda .........hizo ni akili za bavicha
Tunza hii... Hata kwa Sabaya, kuna mwana flani hivi humu JF kila siku alikuwa anakuja na UZI kuonyesha Sabaya atachomoka...!!! lakini mwisho wa siku tumeyaona... WANASEMA BORA UPOTEZE HIRIZI KULIKO KUFIWA NA MGANGA
 
Katika hali ya kawaida Makonda hana raha kabisa.

Hana raha kwa sababu hana mamlaka yoyote tena ya kumfanya afanye vitu vya kuonekana. Makonda kaondokewa na Godfather.

Makonda anatajwatajwa na watu kuwa kwa matendo yake anaweza kuwa zaidi ya Sabaya. Hata Sabaya aliwahi kumtaja kwa sifa Makonda.

Pale Sabaya alipotaka hela kwa nguvu toka kwa wafanyabiashara na kuwadhihaki kuwa "mtajua wenyewe cha kusema kama ni ujambazi au Makonda Style".

Leo hii Sabaya cha Mtoto kwa Makonda,Sabaya Yuko nyuma ya nondo,je Makonda anajisikiaje?

Makonda aliweza kwenda clouds Usiku kibabe na Special force,
Makonda alikua anapigiwa salute,Makonda alikua anaingia nyumba nyeupe vile apendavyo,

Alikua anaweza kutoa amri kwa baadhi ya watu wasionekane Dar es salaam.

Lakini sasa haijulikani Yuko wapi,anafanya nini.

Alikua governor aliishi kifahari ofisini Hadi nyumbani.

Alilalamikiwa Sana lakini hakuguswa,waliomshitaki waiiadhibiwa wao. Hata Waziri wa mambo ya nje wa USA alivyomtuhumu lakini hakuondolewa. Tena tuhuma nzito kabisa za kunyang'anya haki za watu za kuishi lakini hakuondolewa.

Asante Sana TISS kwa kumpigia fix Kisha akaenda kugombea ubunge akashindwa na aliporudi akakuta kiti chake kakaa mwingine.

Leo hii Makonda ana hofu,sijua kama Bado Pasi yake anayo au kakabidhi.

Makonda alichaguliwa kuwa Mkuu wa Wilaya mara tu baada ya kumzaba vibao Waziri Mkuu mstaafu anaeheshimiwa na watu wengi mzee Warioba.

Makonda akawa Mkuu wa Mkoa,
Akafanya mengi mazuri na mengine sio mazuri.

Akataja wauza na watumia madawa ya kulevya,
Akamtaja mtoto wa aliemteua kuwa Mkuu wa Wilaya ,Mbowe,Gwaji boi na wengine wengi.

Makonda akataja wanaume waliotelekeza watoto,akamtaja
Waziri Mkuu mstaafu Lowasa na watu wengine.

Makonda alikua na mengi bana mengine mtaongezea.

Sasa kwa hali ya kawaida Makonda hawezi kuwa na raha, kwa sababu hana mahali pa kufanya mambo ya kuonekana.

Lakini kubwa zaidi ni jinsi anayolinganishwa na jambazi sugu sabaya.nasema jambazi kwa sababu Mahakama tayari imethibitisha hilo.

Mungu fundi.
Umeongea kinafiki tu...miTanzabia mpo kuangalia tu mabaya yampate fulani,shenzi kabisa

Atavuka na zitabaki story...mnadhani kua kiongozi legelege kuna watu wanawezekana? Na wasio wezekana hamuoni ubaya wao jinsi wanavyo athiri wengine,mnaangalia tu aliyekua anajulikana ambaye ni mmoja alikua kiongozi,mnaweka mawazo ya kipumbavu kudhani alionea watu bila kujua waliominywa walikua watu gani kwenye jamii....hujawahi kuteswa na washenzi ukaenda kuomba msaada wa kiongozi wa wilaya wu mkoa ndo mana unaropoka hovyo
 
Ukitaka kujua rika la mdau yeyote JF angalia reply yake kutokana na mada yoyote inayokashifu!.
 
Humjui vizuri makonda, yote yaliyoandikwa hapa dhidi yake ukweli unaweza kuwa ni 1% the rest ni uongo. Na hatokuja kufungwa kama wengi mnavyodhani, tunza hii sms kwa kumbukumbu [emoji6]
Naweza kukubaliana na wewe kua pengine Makonda hatashtakiwa(maana kufungwa mpaka apatikane na hatia kama Sabaya)

Lakini hii haiondoi ukweli(facts) kwamba katika kipindi chake akiwa RC Dar kuna watu aliwaumiza kwa matamko yake, maamuzi yake na vitendo vyake. Na kuwaumiza kwenyewe ni kwa kihalifu kabisa

Namsifu kwa jambo moja, alikua very smart. Ukiondoa lile tukio la kuvamia radio/tv ya Clouds(ambapo actually alikwenda na vyombo rasmi vya ulinzi na usalama na hivyo inam cover) yeye hakua anaenda front kichwa kichwa kama Sabaya

Yaliyowazi kwa wengi na yanayofanya watu wafurahi anguko lake(japo si haki) ni matamko yake ya kujikweza na kujimwambafai. Mengine alikua yupo nyuma ya pazia akishika remote control.

Pia naelewa ana "connection" ya nguvu kwenye utawala huu japo kwa yaliyopita na kelele za Wananchi itakua vigumu kurudishwa madarakani angalau kwa kipindi hiki
 
Hiyo clip itakuwa hujaifahamu. Mleta hiyo clip.anasema kuwa huyo aliyekuwa ananyooshewa kidole na kupewa onyo kwa sasa ni Katibu Mkuu wa CCM. Kawa bosi wake Makonda x1000
Ni sawa ila nimeshakutana nayo mara kadhaa ikitumika kama kuonesha uovu wa Jamaa...ili hali kwa maoni yangu alichokifanya hapo ni mambo ya kawaida tu ya Viongozi.

Hilo la meza kupinduliwa sasa ni jambo lingine.
 
[emoji1][emoji1]
FB_IMG_1637211243258.jpg
 
Back
Top Bottom