Katika hali ya kawaida Makonda hana raha kabisa

Binafsi sioni tatizo kubwa kwenye hii clip....naona tujikite kwenye zile za uvamizi wa kituo na mauzauza mengine.
Hiyo clip itakuwa hujaifahamu. Mleta hiyo clip.anasema kuwa huyo aliyekuwa ananyooshewa kidole na kupewa onyo kwa sasa ni Katibu Mkuu wa CCM. Kawa bosi wake Makonda x1000
 
hamna cha kumfanya makonda .........hizo ni akili za bavicha
Tunza hii... Hata kwa Sabaya, kuna mwana flani hivi humu JF kila siku alikuwa anakuja na UZI kuonyesha Sabaya atachomoka...!!! lakini mwisho wa siku tumeyaona... WANASEMA BORA UPOTEZE HIRIZI KULIKO KUFIWA NA MGANGA
 
Umeongea kinafiki tu...miTanzabia mpo kuangalia tu mabaya yampate fulani,shenzi kabisa

Atavuka na zitabaki story...mnadhani kua kiongozi legelege kuna watu wanawezekana? Na wasio wezekana hamuoni ubaya wao jinsi wanavyo athiri wengine,mnaangalia tu aliyekua anajulikana ambaye ni mmoja alikua kiongozi,mnaweka mawazo ya kipumbavu kudhani alionea watu bila kujua waliominywa walikua watu gani kwenye jamii....hujawahi kuteswa na washenzi ukaenda kuomba msaada wa kiongozi wa wilaya wu mkoa ndo mana unaropoka hovyo
 
Ukitaka kujua rika la mdau yeyote JF angalia reply yake kutokana na mada yoyote inayokashifu!.
 
Humjui vizuri makonda, yote yaliyoandikwa hapa dhidi yake ukweli unaweza kuwa ni 1% the rest ni uongo. Na hatokuja kufungwa kama wengi mnavyodhani, tunza hii sms kwa kumbukumbu [emoji6]
Naweza kukubaliana na wewe kua pengine Makonda hatashtakiwa(maana kufungwa mpaka apatikane na hatia kama Sabaya)

Lakini hii haiondoi ukweli(facts) kwamba katika kipindi chake akiwa RC Dar kuna watu aliwaumiza kwa matamko yake, maamuzi yake na vitendo vyake. Na kuwaumiza kwenyewe ni kwa kihalifu kabisa

Namsifu kwa jambo moja, alikua very smart. Ukiondoa lile tukio la kuvamia radio/tv ya Clouds(ambapo actually alikwenda na vyombo rasmi vya ulinzi na usalama na hivyo inam cover) yeye hakua anaenda front kichwa kichwa kama Sabaya

Yaliyowazi kwa wengi na yanayofanya watu wafurahi anguko lake(japo si haki) ni matamko yake ya kujikweza na kujimwambafai. Mengine alikua yupo nyuma ya pazia akishika remote control.

Pia naelewa ana "connection" ya nguvu kwenye utawala huu japo kwa yaliyopita na kelele za Wananchi itakua vigumu kurudishwa madarakani angalau kwa kipindi hiki
 
Hiyo clip itakuwa hujaifahamu. Mleta hiyo clip.anasema kuwa huyo aliyekuwa ananyooshewa kidole na kupewa onyo kwa sasa ni Katibu Mkuu wa CCM. Kawa bosi wake Makonda x1000
Ni sawa ila nimeshakutana nayo mara kadhaa ikitumika kama kuonesha uovu wa Jamaa...ili hali kwa maoni yangu alichokifanya hapo ni mambo ya kawaida tu ya Viongozi.

Hilo la meza kupinduliwa sasa ni jambo lingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…