Katika jambo kubwa ninalojivunia, ni kutambua kuwa hakunaga UCHAWI

Ili ukatae hakuna uchawi itabidi pia ukatae hakuna Mungu .
 
Nikueleweshe Tena uchawi upo Kwa maana ya kufanywa yaani matendo yake
Ndege

Bado unaendelea kujikanyaga. Umekubaliana kwamba uchawi upo katika hali ya kutenda matendo yake.

matendo hayo yanafanyika ila hautendi lolote kama ni hela utazipatia kwenye kazi utalipwa na sio eti uloge uende chumbani ukute mahela yamejaa
Una maanisha nini kusema hautendi lolote?

tunarudi pale pale. Kuamini uwepo wa Mungu unapaswa kuamini uwepo wa shetani kitu ambacho moja kwa moja unapaswa kuamini uchawi upo.

Kusema hautendi lolote ni kwenda kinyume na kumpinga Mungu na vitabu vyake vitakatifu.

Unakubaliana kwamba Mungu anasema uchawi upo? Na katika vitabu vyake Yakima Koran na biblia yameelezwa mambo haya?

Unaamini Vipi Mungu yupo na unasema hautendi lolote uchawi?
 
Madam boss kumbe na wewe una fikra safi kiasi hiki , wengi wamejengwa kwenye fikra duni za kuamini hizi habari za uchawi miaka nenda rudi bila kujitambua wanaamini kitu ambacho hakipo, hongera sana MadamπŸ‘πŸ‘
 
Kasome Machapisho ya Dr. Fr. David Clement Fumbuka, Padri Mzungu aliyefanya extensive research kuhusu jamii ya Wasukuma na mwanzilishi wa Sukuma Museum pale Bujora, Mwanza. Ndo utajua wewe na Fr.Clement nani anaujua ukweli wa haya mambo.
Ni kweli SEMA wengi hatupendi kujielimisha.
Pia
The late Professor Isaria Kimambo aliandika maandiko mengi na tafiti mbali mbali za history hapa nyumbani kwetu TANZANIA mfano
""A political history of pare of Tanzania"" by professor Isaria .N. Kimambo by then ambapo alikua senior professor in history department at the University of Dar es Salaam. The book was published in 1969. Jump ndani kachambua kwa kina hizo Imani kwa wapare..

Kuna watu humu naona wanavaa miwani za mbao
 
Hizo ni story tu hazina ukweli wowote , japo zinamafundisho ndani yake.
 
Mkuu hayo ni mambo ya kawaida tu ambayo hata mimi ninayo ila hayana uhusiano na uchawi , wala hizo hadithi za Mungu na shetani ,ni kawaida tu sema labda elimu yake ndio hauna ndio maana ukaamua kuya overrate
 
Mama unalijua ZONGO?
 
Kaka Mshana Jr unaitwa uku.
 
Mtoa mada unapajua Handeni Kwamsisi,Sumbawanga na Gamboshi-Bariadi?
 
Hakuna kitu kama hicho , umeongea hivyo as if magu hakuna aliye fika hawana cha uchawi wala nini sema wana imani zisizo na mashiko yoyote.
 
Kutokuwa muumini namaanisha kwamba fikra hizo hazinitawali tena
Mheshimiwa Dkt Gwajima.

Kutokuwa Muumini fikra kutokukutawala halimaanishi kwamba jambo hilo Halipo katika muktadha wa Dini.

Kama mimi si muumini kwamba kwenye Bendera ya Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ hakuna Rangi nyeusi haiondoi uhalisia kwamba rangi nyeusi haipo.

Kukubaliana Na Mungu ni kukubaliana na uwepo wa shetani moja kwa moja.

Unafikiri ni njia ipi sahihi ya kuendelea kuifundisha jamii kutokana na athari za kuwepo kwa imani za kishirikina?
 
Madam boss kumbe na wewe una fikra safi kiasi hiki , wengi wamejengwa kwenye fikra duni za kuamini hizi habari za uchawi miaka nenda rudi bila kujitambua wanaamini kitu ambacho hakipo, hongera sana MadamπŸ‘πŸ‘
Kwa kweli nawashukuru wazazi wangu na Walezi wangu na babu wa babu zangu na bibi wa bibi zangu kwa kuwa hii ajenda haikuwa kabisa sehemu ya ukoo wetu si kwa baba si kwa mama.

Niliwahi kumuuliza babu yangu mmoja kuhusu je amewahi waona wachawi? Akiwa na miaka takribani 78 hivi na mimi nimeshamaliza Chuo kikuu udaktari alinijibu "hayo mambo mimi nayasikia tu stori kila mtu anasema naye kasikia, mimi sijayawahi hata yaona" RIP Babu yangu na Bibi yangu na wazazi wangu kwa ujumla, mlinifanya imara nitabaki kuwa imara daima.

Nawasihi wote tuepuke hizi fikra za Imani ya uchawi kwani ni adui wa maendeleo. Inawezekana kuendelea na kufanikiwa nje ya fikra hizi na nje ya kufanyiwa ushirikina shirikina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…