Katika suala zima la ndoa, dini ya Kiislamu ipo vizuri

Unaweza kutoa ushahidi nje ya Quran na Hadithi zake kuwa Musa, Daudi na Issa walikuwa Manabii wa Majini pia ?

Maana nje ya Biblia ushahidi upo wa kutosha kuwa Musa, Ibrahimu na Yesu Kristo walikuwa Manabii wa Watu tu.

Na hakuna Andiko la Waizraeri linalo kiri kwamba Mitume wao walikuwa Manabii wa Majini pia.
 
Acha kupotosha ... Sheria ya talaqa ipo wazi Mungu hajakosea kusema kuwa kuwe na mashahidi wanne. Hii inaonesha jinsi gani uislam unajali na kuhifadhi haki za mwanamke. Sheria hii inamlinda mwanamke asionewe/kusingiziwa uchafu. Leo hii mtu unaweza ukamkuta mtu kasimama na mkeo moja kwa moja ukamtuhumu kuwa kazini, jambo hili ni baya so ili usimvunjie heshima mwanamke ndio iliwekwa hiyo sheria kuwa either kuwepo mashahidi wanne walioshuhudia tendo likifanyika au hata kama ukiwepo wewe mwanaume mmoja umemfumani mkeo anafanya mapenzi na mwanaume mwengine unaweza kuwa ni shahidi tosha ila masharti yake ni kuwa Ukaape mara 4 mbele ya waumini kuwa kweli umemshuhudia mkeo akizini na pia mwanamke ikiwa anaona ameonewa inatakiwa aape mara 4 kuwa hajazini na kiapo cha mwisho mnatakiwa muombe laana iwakute ikiwe mmoja wenu anasema uongo na kumsingizia mwenzake. Huu ndio uislam.
 
Quran 46:29 -32

Na wakati tulipo waleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur'ani. Basi walipo ihudhuria walisema: Sikilizeni! Na ilipo kwisha somwa, walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya.

Wakasema: Enyi kaumu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilicho teremshwa baada ya Musa, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake, na kinacho ongoza kwenye Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka.

Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu, na muaminini, Mwenyezi Mungu atakusameheni, na atakukingeni na adhabu chungu.

Na wasio mwitikia Mwitaji wa Mwenyezi Mungu basi hao hawatashinda katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotovu ulio dhaahiri.
 
Quran 46:29-32

ALLAH anaelezea habari kuwa majini walipita jangwani wakamkuta Mtume s.a.w akiisoma Quran kwa wanafunzi wake, wakaisikia na wakajiunga kuyasikiliza yale maneno kisha wakagundua kuwa ni maneno yanayosadikisha yaliyopita kwenye kitabu cha Musa a.s waliamini kisha wakarudi kwa mataifa yao kwenda kuwapelekea habari juu ya yale waliyoyasikia na kuwaonya kuwa wamwamini Mtume wa Mwenyezi Mungu.
 
Hujajibu kabisa maswali yangu niliyokuuliza.

Unataka kusema Musa na Ibrahimu walikuwa Mitume wa Majini pia kama Muhammadi?

Unataka kusema Majini nao walitumia mafundisho ya Vitabu vya Torati na Zaburi na Injiri ?
Ndio majini walitumia mafundisho ya Tawrat, zabur, injili na Quran

Ushahidi soma Quran 46:29-32
 
Thin Tisha uwepo wa uislamu kabla ya Muhamad
Quran 42:13

Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.


 
Ndio majini walitumia mafundisho ya Tawrat, zabur, injili na Quran

Ushahidi soma Quran 46:29-32
Shida ni kuwa habari hizo zinapatikana kwenye vyanzo vya dini ya Kiislamu tu.

Sasa mtu kama sio Mwislamu ataziamini vipi ?

Ni Allah anazungumza basi.

Na zimeanza kusikika wakati wa Muhammadi.

Hakuna habari za Majini kuwa na Dini wakati wa Ibrahimu wala wakati wa Musa wala wakati wa Daudi wala wakati wa Yesu Kristo. Kwenye vyanzo vya Waisrali ambao Mitume wao walihudumu.

Hapa namaanisha kuwa lazima Waisraeli wangeandika kwamba Mitume wa kabila lao waliamriwa pia kuwahubiria sheria za Mungu pia na Majini ingawa Majini hawakutii.

Vitabu vya Historia ya Wayahudi havielezi popote kuwa Mitume wa Kiisraeli, kuwahubiria Dini yoyote ile Majini.

Kwahiyo habari hizo ili mtu aziamini ni lazima awe Mwislamu, na azisome kwenye vyanzo vya Kiislamu Tu.

Hapo ndipo penye changamoto.
 
Moja ya kiashiria kuwa Suleiman alikuwa amepewa uwezo wa kuwatumikisha majini ni katika ujenzi wake wa msikiti wa baytul maqdis

Soma kitabu cha 1 wafalme 6:7
 
Habari za majini ni habari za ulimwengu wa ghaibu (unseen) , ni ufunuo kutoka kwa Mungu pekee. Mwenyezi Mungu amewaelezea kupitia Quran na hadith vizuri sana.
 
Habari za majini ni habari za ulimwengu wa ghaibu (unseen) , ni ufunuo kutoka kwa Mungu pekee. Mwenyezi Mungu amewaelezea kupitia Quran na hadith vizuri sana.
Ndio maana jamii isiyokuwa ya Kiislamu haiamini hizo habari.

Maana kwa mfano,
habari za Yesu Kristo.
Wabudha wa India hawawezi kuziamini kwa kusoma Biblia tu na Hadithi zake.

Ili kuamini kwanza wanazitafuta katika vitabu vya historia ya Waisraeli, na si hivyo tu wenye uwezo wanafunga safari hadi Israeli ili kuthibitisha.
Huyu mtu alikuwa Nabii ni
Mwisraeli kweli
Je alizaliwa kijiji cha Nazareti kweli
Je alihubiri Injiri kweli
Je alisulubiwa Msalabani kweli
Je Alikufa kweli

Sasa habari za Majini na Dini hazipatikani popote zaidi ya kwenye vitabu vya Dini moja tu ya Kiislamu.

Mimi Msomi asiye Mwislamu nitaziamini vipi.
Kwakuwa huku kwenye Elimu ya Kidunia hakuna hizo taarifa.

Na kama hakuna basi hata ukweli wake ni wa kutiliwa mashaka.
Maana anaye zieleza ndio huyo huyo tu anayezithibitisha.

Hivyo zinakosa mashiko ya kuaminika.
 
Habari za majini ni habari za ulimwengu wa ghaibu (unseen) , ni ufunuo kutoka kwa Mungu pekee. Mwenyezi Mungu amewaelezea kupitia Quran na hadith vizuri sana.
Sasa Waisraeli si Wangethibitsha kuwa Mitume wao akina Musa waliagizwa kuwahubiria Torati na Majini pia. ?

Wangeeleza kuwa÷

"Kijana wetu Musa Mungu wake alimwagiza aitangaze Dini yake na kwa Majini pia"

Au ilikuwa ni siri ya Musa tu basi.
 
Nimeshakwambia jua kwanza dini yako ndio uje uandike , huyu hapa allah anawaamrisha wasirudi nyuma wakapambane na majabari mpaka wachukue nchi ya wa palestina
Koran 5:21 Enyi watu wangu! T'iini amri ya Allah. Ingieni ardhi takatifu aliyo kujaalieni Allah muingie, wala msirejee nyuma kuwaogopa hao watu wake majabari, mkaja kukosa nusura ya Allah na radhi zake.
 
Afisa tabibu, mwanamke ana uwezo wa kuvumilia kuliko mwanaume. Ndio maana unaona vifa vya baba kumparamia mwanae! Umeshaona mama kumparamia mwanae wa kiume?
Sio mama kwa mwanawe tu ila pia sijawahi kuona wala kuskia mwanamke akimbaka mwanaume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…