Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Unaweza kutoa ushahidi nje ya Quran na Hadithi zake kuwa Musa, Daudi na Issa walikuwa Manabii wa Majini pia ?Swali lako la pili unauliza kuwa mtume wa Majini alikuwa nani...
Mwenyezi Mungu anakujibu
Quran 35:
24. Hakika Sisi tumekutuma wewe kwa Haki, kuwa ni mbashiri na mwonyaji. Na hapana umma wowote ila ulipata mwonyaji kati yao.
25. Na wakikukanusha basi walikwisha wakanusha walio kuwa kabla yao. Mitume wao waliwajia kwa dalili wazi wazi na kwa maandiko na Kitabu chenye nuru.
26. Kisha nikawakamata walio kufuru. Basi kuchukia kwangu kulikuwaje?
Mwenyezi Mungu anasema kuwa hakuna Umma (taifa) lolote ila aliupelekea Mwonyaji kati yao. Yaani kabla ya mwanadam kuumbwa. Majini waliishi juu ya mgongo wa ardhi hii na walifanya ufisadi mkubwa sana , ila Mungu aliwaletea waonyaji waliotoka miongoni mwao wakiwaonya kuwa Wamuabudu Mungu mmoja tu.
So waonyaji wa majini kabla ya mwanadam kuumbwa walikuwa ni majini wenzao, baada ya kuja mwanadamu na kupewa utawala katila ardhi hii.
Waonyaji wa majini na binadamu ...wamekuwa ni binadam. So Mtume wa majini kipindi cha Tawrat alikuwa ni Mussa. Mtume wa majini kipindi cha zaburi inateremka alikuwa ni Daudi kisha mwanawe suleymani, kipindi cha injili inateremka Mtume wa wanadam na majini wa kipindi hicho alikuwa ni Issa (,Yesu) mwana wa mariamu na kipindi cha Quran inateremka mtume wa binadamu na majini alikuwa ni Mtume Muhammad s.a.w
Maana nje ya Biblia ushahidi upo wa kutosha kuwa Musa, Ibrahimu na Yesu Kristo walikuwa Manabii wa Watu tu.
Na hakuna Andiko la Waizraeri linalo kiri kwamba Mitume wao walikuwa Manabii wa Majini pia.