Katika utawala wake, hayati Magufuli hakwenda New York kuhutubia UNGA, je tulirudi nyuma kiuchumi na kisiasa?

waliovunja vibanda juzi usiku.
Ndio hao hao, kwenye vita wewe kama kiongozi lazima uwe na mtu/watu wa kubeba lawama! Nyerere alikuwa na Kawawa, Mkapa alikuwa na Sumaye, Kikwete alikosa huyo mtu, matokeo yake akanyanyasika sana hadi ikabidi aanze na kuwatumia matapeli wa kisiasa akina Mbowe na wenzake kufanikisha ishu zake, JPM alikuwa nao wengi; Makonda, Kabudi, Kangi n.k.! Mama ni mapema bado, but naona kama Mwigulu anaweza kuibeba hiyo role
 
Ila ww ni mpumbavu sana hata kifaa alichotumia kuingia hapa ni cha mzungu au kuna kiwanda cha simu hapa bongo?
[emoji23][emoji23][emoji23]Sasa kama utaendelea kuwaabudu namna hii utajitoa lini hapo ulipo ili nawe uwe na kifaa chako?

Mibavicha bure kabisa
 
Kama unammisi sana dikteta twende tukakufukie kwenye kaburi lake msituchoshe.

Zama za kishamba zimekwisha lazima mlikubali hili na hii nchi hatuwezi kurudia kosa kuwakabidhi washamba.
Dikteta alikuchapa akiwa hai na bado anakuchapa akiwa mfu!
 
tukijaribu kusimamia hoja na sio ushabiki..

Exposure na kwenda pamoja na dunia ni jambo zuri kuliko kujifungia ndani, sio ujanja kutohudhuria hivi vikao kama mkuu wa nchi, uwepo wa UN na mambo kama haya una maana ndio maana ukawepo huo utaratibu...Dunia imetoka mbali na kufika hapa na taasisi hizi zina mchango wake kuhakikisha dunia iko hapa.....

UN ilianzishwa kwa madhumuni maalumu hapa duniani baada ya miaka ya nyuma dunia kuwa shaghala bhaghala na watu kujifanyia mambo watakavyo kiasi cha vita na mauaji kuwa mengi...uwepo wa UN angalau umeleta amani na ustawi duniani...Vikao vya marais hufanyika kuwaweka pamoja marais na nchi zao kujadili ya duniani na kuwa na muafaka na mambo mbalimbali..

Mfano sasa marais wote duniani wasiwe wanahudhuria hivi vikao...maana yake UN itakufa...UN ikiwa haipo unafikiri maisha yatakuwaje duniani hapa?
 
Misukule ya dikteta mnatapatapa Sana, kwakuwa mungu wenu alikuwa haendi kwenye hiyo mikutano ya kimataifa,,mlitaka na Samia hasiende kuiwakilisha Nchi
 
Nitafurahi kama tunaweza ku discuss, bila kumbeza marehemu, exposure ni personal, sio transferable useme kwa vile Balozi Dr. Mahiga amekaa Marekani na kuzunguka dunia 20 years, hivyo baada ya kuteuliwa na JPM, anaihamishia hiyo exposure yake kwa JPM. Exposure ni kama dose, ili upate exposure, ni lazima wewe ndio uwe exposed na sio kuwakilishwa.

Mtu ujifungie chumbani kwako for 5 years huku ukituma watu wakuwakilishe, what do you expect?.
P
 
Angeenda kuongea nini wakati mtu mwenyewe ni kilaza alichoweza yeye kufokafoka hovyo na kutisha wengine kwa kujiona ni mwamba,yule mtu hakustahili kabisa kuwa kiongozi mkuu.
 
Asante kwa majibu na pia nakubaliana na tahadhari uliyoitoa.

Kwa ufahamu wangu ni kuwa raisi ni taasisi iliyosheheni uwakilishi wa mamlaka ya raisi sehemu mbalimbali ndani ya nchi na nje ya mipaka yake kwa mujibu ya sheria na katiba ya nchi husika. Uwakilishi huo lazima uzingantie taaluma au uelewa wa mambo fulani kwa undani zaidi ili kuweza kusaidia raisi kufanya maamuzi yaliyo sahihi kutokana na ukweli kuwa raisi hana uelewa wa profession zote hata angekuwa nani.

Kwa mustakabali huo, raisi kwa utashi wake pekee hawezi kuongoza nchi na ukategemea mambo yaende inavyopaswa, tuchukulie mfano, raisi aliyesomea taaluma ya sanaa akajipeleka yeye kama yeye kichwa kichwa kupata ushauri au kufunga makubaliano yahusuyo taaluma ya sayansi bila kutegemea technical expertise kutoka kwa Msaidizi wake atakuwa akijidanganya na kulipeleka taifa shimoni.

Realistically, President is just nation’s political icon who has to resonate with his colleagues about all national aspects prior to its adherence, meaning that, the exposure of his associates is akin and very crucial than what you might be thinking.

Miaka minne ya Trump bila kuja Africa haikumzuia yeye kuwa exposed na yale yanayoendelea huku, zaidi zaidi aliipunguzia serikali/ wanachi mzigo wa gharama za kusafirisha presidential delegation, Kupanga ni kuchagua, na raisi wetu aliyepita kwa hili alilipanga vizuri sana. Ninachokiona hapa ni hali ya kutaka kushindana kuhudhuria vikao vya maraisi na first world countries ambazo kwa namna moja ama nyingine they have managed to do so using our own resources, this is according to colonialism without forgetting to mention the ongoing neocolonialism.
 
Nchi huongozwa kwa Principles na si matakwa au utashi wa mtu mmoja! Magufuli hakuwa na exposure yoyote na pia hakuwa mjuzi wa lugha yoyote zaidi ya kisukuma, hivyo kufanya mapungufu yake binafsi kuwa msingi wa kuendesha Taifa ilikuwa ni ujinga na unafiki tu!
Wito kwa akina Mwigulu wanaoonekana kuupenda sana Urais,hawana budi kujenga communication skills kwani hatutakubali tena kuwa na Rais very poor on communication skills kama alivyokuwa Magufuli.
 
Exposure ya mawaziri isingeweza kumsaidia Rais Magufuli kwa namna yoyote ile. Magufuli hakuwa mtu wa kuamini katika mawazo ya watu wengine. Aliamini katika anachokitaka yeye tu.

Kumpa exposure Magufuli kupitia mawaziri ni jambo ambalo lisingewezekana kabisa. Na uthibitisho wa hilo, angalia alivyoongoza nchi such primitively huku akijisifu na kuwajaza ujinga mwingi watu wasio na uelewa.
 
Angeenda kuongea nini wakati mtu mwenyewe ni kilaza alichoweza yeye kufokafoka hovyo na kutisha wengine kwa kujiona ni mwamba,yule mtu hakustahili kabisa kuwa kiongozi mkuu.

hahaaa,na alijua kuwafilimba.
 
Ni juha tu anayeweza kufikiri kwamba akijifungia tu Nyumbani kwake bila kutembelea majirani na marafiki Wenye maendelo kuliko yeye kubadilishana nae Mawazo kutamletea maendelo.

Huko kukosa exposure ndio kumepelekea uwanja wa kimataifa kujengwa porini usipotumika, kununua ndege cash money Kama tajiri wa madawa kulevya.
Na hayo ni Yale tunayoyajua tu, yapo mengi ya Siri ambayo amepigwa kimya kimya Kwa Ushamba tu
 
Kuna mengine umesema yaliyo sahihi lakini kuna mengine, umesema kwa mahaba.

Hivi kwako wewe 12,000km+ na 2,000km +; nani amefanya kazi kubwa zaidi? Awamu ya Kikwete, zaidi ya 12,000km za barabara za lami zilijengwa. Barabara ndefu za kilometa nyingi. Wakati wa Magufuli zimejengwa chini ya 3,000km, nyingi ni barabara za mitaa mijini. Nani alifanikiwa zaidi?

Wakati wa Kikwete, per capita kwa miaka 10 ilipanda kwa $380, wakati wa Magufuli kwa miaka 5, ilipanda kwa $80. Nani alifanya vizuri zaidi?

Wakati wa Kikwete utalii ulikuwa unakua kwa 15%, wakati wa Magufuli 3.6%. Nani alifanya vizuri zaidi?

Ukuaji wa jumla wa uchumi wakati wa Kikwete ulikuwa 7%, wakati wa Magufuli ulishuka mpaka 1.9%, kisha ukapanda mpaka 4.5%, ndiyo ikawa mwisho.

Wakati wa Kikwete, ujenzi wa chuo Kikuu Dodoma. Wakati wa Magufuli hakuna.

Wakati wa Kikwete, ujenzi wa hospitali kubwa na za kisasa Mloganzila, taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Benjamin Mkapa. Wakati wa Magufuli ujenzi wa vituo vya afya na hospitali, thamani yake yote haikufikia thamani ya Mloganzila pekee.

Magufuli alifaa kuwa msimamizi. Kwenye ujenzi wa barabara wakati wa Kikwete alisimamia vizuri, lakini kwenye uongozi mkuu wa nchi alipwaya sana. Hii naongelea kwa ujumla, siyo kwa kumlinganisha na Samia au Kikwete.

Ili tutoke mahali tulipo, tunahitaji kiongpzi mwenye uwezo mkubwa zaidi kuliko Magufuli, kuliko Kikwete, kuliko Samia, na kuliko Mwinyi. Tulihitaji kiongozi mwenye uwezo, angalao wa kiwango cha Mkapa. Watu wengi hawajui, lakini mambo aliyoyafanya Mkapa, ukimwacha Nyerere, hakuna Rais mwingine aliyeweza kuyafikia. Hata mafanikio madogo yaliyopo sasa, msingi wake ulijengwa na Mkapa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Sasa kama utaendelea kuwaabudu namna hii utajitoa lini hapo ulipo ili nawe uwe na kifaa chako?

Mibavicha bure kabisa
Ni kweli nchi inahitaji kujenga uwezo wa ndani. Lakini utajengaje ukijitenga na waliokutangulia?

Tujifunze toka China. Wachina siku za nyuma walijitenga na nchi za Magharibi. Matokeo yake ikawa hohe hahe.

Baadaye wakagundua makosa yao. Wakafungua milango kwa makampuni ya mataifa ya Amerika na Ulaya. Makamouni ya Ulaya na America yakawekeza heavily in China, na yanaendelea kuwekeza. Mpaka leo China ndiyo nchi inayovutia wawekezaji wengi toka Ulaya, America na Asia kuliko nchi yoyote.

Matokeo yake, uchumi wa China ukapaa maradufu, maendeleo ya tekinolojia yakaongezeka sana. Leo hii, angalao katika makampuni makubwa 10 nchini Chima, moja, kampuni ya Huawei, ni kampuni ya China. Mengine yote ya kigeni, lakini wanapiga hatua. Ukijitenga hufiki popote. Unakuwa nao, huku unajenga uwezo wako wa ndani.
 
Upo vizuri.
 
Hatukurudi nyuma! Tuliingia uchumi wa kati ambapo hatukuwa. Watanzania tunaona na tunamkumbuka kwa mazuri
Anayefikiria kuwa Magufuli ndiye alituingiza kwenye uchumi wa kati, ni mjinga hasa, asiye na uelewa wowote.

Mkapa alipandisha per capita yetu kwa $400, Kikwete alipandisha per capita yetu kwa $380, na Magufuli alipandisha kwa $80. Nani alikuwa the weakest performer?

Projections za Mkapa, ilikuwa kwa vile Mwinyi alipandisha per capita $50, yeye kwa $400, anayefuata (Kikwete) akipandisha angalao kwa $800, na Rais anayefuata (Magufuli) angepandisha hata kwa $800 hiyo hiyo, Tanzania tungekuwa kwenye uchumi wa kati wakati wa awamu ya 5; tukiwa na per capita ya $2,400. Lakini mpaka leo tupo kwenye $1,100. Hatujafikia hata 50% ya matarajio ya Mkapa. Lakini wajinga wanashamgilia.

Ukweli ni kwamba, mpaka leo, Tanzania bado ni maskini sana, na mwanga haupo. Nchi kama Botswana ina per capita $18,110. Namibia $4,175, Madagasca $17,320 Ukiacha Madagascar iliyopata uhuru mwaka 1960, haya mengine ni mataifa yaliyopata uhuru baadaye sana baada ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…