Sidhani kama kwenda UN ni kupiga hatua. Au kuwa na hyo exposure unayoisema. Si mara ya kwanza Tanzania kuhudhuria hivyo vikao. Toka Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete. Tena Kikwete aliizunguka dunia nzima.
Magufuli kwenda UN hakuwahi hata siku moja. Lakini aliifanya Tanzania kuwa ya kisasa. Katika utawala wake Tanzania ilisikika kila mahala. Watu waliiongelea Tanzania kwa mafanikio ya kiuchumi. Nilishawahi kusema humu. Nchi fulani Ulaya walikuwa wakijadili Magufuli alivyo weza kuwa na miradi mikubwa ya kiuchumi.
Reli ya SGR,kufufua reli ya Moshi Arusha hadi Dar. Kujenga Bwawa la Nyerere, kufungua masoko ya madini, na kiwanda cha uchenjuaji. Kuhamishia Makao Dodoma, kufufua shirika la ndege ATCL, kuyawezesha mashirika ya Posta na Simu. kujenga hospitali na vituo vya afya muhimbili sasa ni moja ya hospitali zinazoaminika. Kujenga madaraja na barabara za kisasa. Ni mengi kutaja huyu mnae msema hakuwa na exposure, lakini kafanya haya yote ndani ya miaka 5.
Watanzania baadhi ni wanafiki, wamezoea kujipendekeza ili wapate vyeo au njia za kujipatia pesa. Magufuli aliziba mianya yote, waliotegemea vyeo hawakupata. Wakaanza kujenga chuki zisizo na maana. Ndo maana hadi leo wanachukia hadi marehemu, wanafurahi mtu kufa utadhani wao wataishi milele.
Mama Samia apewe muda msimpe sifa zisizo stahili. Make hadi sasa ni ngumu kujua tunaelekea wapi. Nini hasa vision ya kiongozi wetu. Anaeogopa kutatua kero za wananchi hadharani. Kutwa nzima ni safari. Kikwete alisafiri lkn hatukuwahi kuona exposure hiyo ikiletwa Tanzania. Nilishawahi kwenda nchi fulani, katika mji wao mmoja ni mji wa kawaida tu. Nikafika hotel moja, nikaambiwa Rais Kikwete alipenda kufikia pale kalala mara kadhaa. Nikajiuliza Rais wa nchi anazurura hadi kuwa mteja wa hotel.
Msiyo mpenda Magufuli mtazidi umia na kuangaika. Yeye amepumzika. Alifanya yake kwa Tanzania. Swala kujiuliza wewe hapo umeifanyia nini Tanzania? Je japo unaishi haki gani unaitenda kwa wananchi wengine na kwa nchi yako?
Mauaji na utekaji umekuwepo Tanzania vipindi vyote. Wakati wa Kikwete tulijionea wasio julikana wakimteka Ulimboka, waandishi wa habari wakiteswa na kuuwawa. Mwanasiasa Mkongwe wa NCCR Dr. Mvungi alilalamika anafatiliwa baadae alivamiwa na kukatwa mapanga hatimaye alipoteza maisha.
Leo tunajifanya mabaya yote ni ya Magufuli. Tuache uzandiki. Magufuli aliirejesha heshima ya Tanzania.
Hakuna nchi duniani iliendelea kwa Demokrasia never. Marekani yenyewe wanawake wameanza kupiga kura miaka ya 60 japo walipata uhuru wao toka karne ya 18. Nchi nyingi za Ulaya zimeongozwa kimabavu ndo maana zilifanikiwa.
Leo mnadanganyika na Demokrasia na Human Right.
China inademokrasia gani? Na human rights zipi? Nchi za arabuni, Dubai, Saudia na nyinginezo wapi demokrasia na human right, mbona zimeendelea kuliko sisi tunao thamini wazungu.
Rwanda leo inasonga mbele wapi Demokrasia na human rights? Ethiopia inakuwa kwa kasi haijawahi kuwa na demokrasia wala human rights zenu. Libya ilikuwa bila demokrasia. Walipotaka Demokrasia wamejikuta kubaya.
Nasema hatuhitaji kuiga kila tuletewacho na mzungu. Tuwe na demokrasia yetu model tofauti na wazungu. Tunatofauti kubwa za kitabia na mazingira na wao hatuhitaji kuiga kila kitu. Kama ni human right Marekani imeua watu wangapi huko mashariki ya kati? Ni watu wangapi uuwawa marekani kila siku?
Imeua viongozi wangapi kwa uongo wa demokrasia.
Watanzania tubadilike hasa wachache tusiyoitakia mema nchi yetu kisa chuki binafsi. Umieni tu Magufuli atabaki kuwa kiongozi wa aina yake. Alie paisha jina la Tanzania. Nikizunguka ulimwenguni uwa naulizwa nchi ya Nyerere, kingine Magufuli alikuwa kiongozi mleta maendeleo, utasikia vizuri havidumu. Hao ndo wanao ongelewa sana.
Nawapenda Haiti, walikuwa hawampendi Rais wao, waliandamana kumpinga hakuleta maendeleo, ila alipouwawa Haiti waliumia, walihudhunika. Walisema japo walimpinga lakini hakustaili kuuwawa.
Hawa watu wanaubinadamu. Siyo baadhi ya watanzania, ambao kufa wanadhani ni kwa watu fulani tu, wanashangilia. Nami nasema mfanyao hivyo nanyi mtakufa na hamjajiuliza mtakufa vifo vya namna gani.
Narudia kusema Mch. Mtikila Nyerere alipo kufa alisheherekea. Leo yupo wapi? Je, kifo chake kilikuwaje? Japo tunapingana lkn tujifunze kuwa na utu. Pia tusidhani Mzungu ni kila kitu. Tunawaabudu sana. Na mzungu ukimshobokea anakusanifu. Wanapenda msimamo wa mtu.
Kuna mengine umesema yaliyo sahihi lakini kuna mengine, umesema kwa mahaba.
Hivi kwako wewe 12,000km+ na 2,000km +; nani amefanya kazi kubwa zaidi? Awamu ya Kikwete, zaidi ya 12,000km za barabara za lami zilijengwa. Barabara ndefu za kilometa nyingi. Wakati wa Magufuli zimejengwa chini ya 3,000km, nyingi ni barabara za mitaa mijini. Nani alifanikiwa zaidi?
Wakati wa Kikwete, per capita kwa miaka 10 ilipanda kwa $380, wakati wa Magufuli kwa miaka 5, ilipanda kwa $80. Nani alifanya vizuri zaidi?
Wakati wa Kikwete utalii ulikuwa unakua kwa 15%, wakati wa Magufuli 3.6%. Nani alifanya vizuri zaidi?
Ukuaji wa jumla wa uchumi wakati wa Kikwete ulikuwa 7%, wakati wa Magufuli ulishuka mpaka 1.9%, kisha ukapanda mpaka 4.5%, ndiyo ikawa mwisho.
Wakati wa Kikwete, ujenzi wa chuo Kikuu Dodoma. Wakati wa Magufuli hakuna.
Wakati wa Kikwete, ujenzi wa hospitali kubwa na za kisasa Mloganzila, taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Benjamin Mkapa. Wakati wa Magufuli ujenzi wa vituo vya afya na hospitali, thamani yake yote haikufikia thamani ya Mloganzila pekee.
Magufuli alifaa kuwa msimamizi. Kwenye ujenzi wa barabara wakati wa Kikwete alisimamia vizuri, lakini kwenye uongozi mkuu wa nchi alipwaya sana. Hii naongelea kwa ujumla, siyo kwa kumlinganisha na Samia au Kikwete.
Ili tutoke mahali tulipo, tunahitaji kiongpzi mwenye uwezo mkubwa zaidi kuliko Magufuli, kuliko Kikwete, kuliko Samia, na kuliko Mwinyi. Tulihitaji kiongozi mwenye uwezo, angalao wa kiwango cha Mkapa. Watu wengi hawajui, lakini mambo aliyoyafanya Mkapa, ukimwacha Nyerere, hakuna Rais mwingine aliyeweza kuyafikia. Hata mafanikio madogo yaliyopo sasa, msingi wake ulijengwa na Mkapa.