Katuni ya Masoud Kipanya inamaanisha nini?

kumbe ulikuwepo upinzani na ile hoja kuwa hakuna upinzan ulishakufa unasemaje au unakufa mara nyingi nyingi.
Upinzani ulikuwepo japo mwendazake aliupunguza kasi ila kwa kinachofanyika sasa ni kuufifisha kwa maridhiano, sioni mpinzani wa kuchuana vikali na SSH 2025.
 
Kinachoiua Chadema sio maridhiano, kinachoiua Chadema ni point za ovyo zinazoshambulia kundi kubwa la ambao hatuna ajira na mamalishe. Sote tunafahamu ajira ni tatizo la kidunia kwa sasa.

Wakati serikali yetu ikijitahidi kuangalia jinsi ya kutatua tatizo hili, na baadhi yetu kujishikiza kwenye ajira hizi anatokea kichaa anazungumza yake! Tunajua kuna fedha huko kilimo kwa ajili ya pilots project za kilimo, lakini haiwezekani kuanza na Watanzania wote.

Mbowe usikatishwe tamaa, tutafika tunapotaka kwa njia ya kukaa mezani. Naamini very soon mchakato wa katiba mpya mama ya Tanzania utaanza na kumalizia kwa amani.

Tumuombee Mungu Rais wetu, Allah amjaze hekima ya kutuongoza kwa amani, Amin.
 
Kwisha habari yao...

Sasa hivi hawana tofauti na Prof wa Uchumi, au Rangi ya zambarau kamw sio Mzee Momose...

Una weza kutoa mifano kibao kushadihisha hili

Kifo cha mende, Chaliii. kwa sauti Prof wa Uchumi
 
Uhafidhina uko pande zote, kuna wanao faidi na siasa za marubano na mateso lazima wapinge maridhiano hayo......
Kwani hayo mateso walikuwa wanayapata kwa kutokukubali mariadhiano?
 
Kwa maoni yangu....Upinzani una, na ina maana ya upinzani wa Sera na Hoja za sera hizo.


CCM ina sera na imezijengea hoja katika ilani yao.


CHADEMA wana listi ya mbinu za kufanya Uharakati. Haina Sera wala hoja.

Kwa nini usimezwe! ngaaa' mu!
Lazima wamezwe hakuna namna
 
Ni ajabu sana kwamba bado kuna Watanzania wengi ambao bado wanatamani sana nchi iongozwe na chama kimoja kile kile (CCM) ila kwa ndoto ya kuwa na Raisi aina ya Magufuli - kama masihi vile - atakeyeletwa ama toka "mbinguni" au na "deep system". Kama Wayahudi walivyokuwa wakimdai Nabii Samweli awateulie mfalme enzi zile baada ya kutoka Misri. Wanaamini hiyo ndiyo namna pekee ya nchi kupata ustawi (sijui kwa wote au kwa makundi yao ya kibinafsi?)!

Hawa Watanzania hawataki demokrasia na hawataki kabisa upinzani dhidi ya serikali na chama tawala na hawako tayari kujishughulisha kufikiri kuhusu undani wa mifumo ya utawala wa nchi. Wao wanataka huyo masihi ndiye afikiri kwa niaba yao, awaaamulie na kuwafanyia kila kitu! Wanaona Magufuli kwa kauli na kashkash zake alitosha kabisa na bado wana hangover ya kutamani atokee mwingine wa aina yake. Tangu miaka wanahangaika kuona upinzani hasa CHADEMA ukipoteza nguvu na kufa kabisa, by any means. Ndio faraja yao.

Waingereza wanasema: "the devil is in the details". Kwa akili za hawa wenzetu ambao ni wengi, maendeleo tutaendelea kuyasikia kwenye documentaries za media na kuyaona kwingine kwa tutakaobahatika kuitembelea dunia.
 
Are you ready to be swallowed?"mwanangu" View attachment 2542545
Am ready!, swallow me! If you can, it's up to you!


View attachment 2542549

Am happy, at now, so that I can smile!, happy! happy! happy! View attachment 2542598
*CCM and its leaders are like a green mamba snake that can cross from one branch of the tree to another very smoothly in search of prey. The green mamba can be able to mingle around with any creature including the nightingale bird, but when a bird starts biting a green snake on the head, mouth, eyes, tail, or head very quickly, it will be hit and released its poison that kills the nerves and stops the heart from working, eventually inflicts death.
 
Haya sio maridhiano bali ni mmoja kakubali kuungana na watesi wake ili asiendelee kuteseka.......wanaoridhiana ni wale wanaotoshana nguvu na kuamua kuleta amani.......
Nyie ndio mlikuwa wanufaika wa mshike mshike
 
""Urafiki ni njia nzuri na salama zaidi ya ku crack upinzani kuliko, uadui au jinsi alivyokuwa anafanya mwendazake, "HAPA TUNAJIFUNZA HEKIMA FULANI TOKA KWA MPENDWA WETU MH. RAIS DR. SAMIA"
 
Wengine walikuwa magerezani, sisi tunalala makwetu,
Wengine wamefilisiwa sisi tunaendelea na maisha
Wengine walipigwa risasi, sisi tuko vyema

Leo wao wameahidiwa katiba sisi twaanza lalamika.

Inaonekana tunapenda harakati kuliko siasa.


Alichofanya chadema ni sawa maana mwisho wa siku Tume mpya ya Katiba inaundwa.
 
Are you ready to be swallowed?"mwanangu" View attachment 2542545
Am ready!, swallow me! If you can, it's up to you!


View attachment 2542549

Am happy, at now, so that I can smile!, happy! happy! happy! View attachment 2542598
Hayo ni maoni yake binafsi, sasa msichanganyikiwe kucomment as if ni unabii toka mbinguni, ni view yake na mwingine pia anaweza kuwa na view tofauti. Ndicho maana wapo CCM wanaoona mama anainufaisha Chadema hivyo hawataki maridhiano na upande wa pili. Wapo wapinzani wanaoona Mbowe anawanufaisha CCM (kama huo mtazamo wa kipanya) hivyo hawataki maridhiano. Na jana walitambulishwa kama (wafaidhina).

Ni kawaida kwenye siasa, mambo ya "behind the scenes" ni mengi sana, tusikurupuke kucomment kwenye yale tunayoyaona nje tu, huwezi jua nini kilijiri huko ndani. Mwisho wa siku kila mtu anatanguliza maslahi yake ili awe salama siku za usoni.

Kwa mtazamo wangu, anayehitaji maridhiano zaidi na mnufaika zaidi mpaka sasa ni Chadema. Extreme politics haifai Tanzania maana watanzania wengi ni waoga. Kwahyo, upinzani kuifanya viburi na kutegemea nguvu ya umma na maandamano kusingewasaidia.

Watanzania sio wapambanaji. Kubargain na mamlaka ili kila upande unufaike ni wisest decision. Maana jiulize, kwani mama angekataa maridhiano angepata hasara gani? Angeendelea kuwa in power kama jiwe, ila Chadema ndo wangejifia kabisa maana majukwaa yote ya kupazia sauti yamepigwa pin.
 
Raia wa Tz wali msariti mbowe kwa miezi 9 alio kaa jela bila mandamano au mgomo, hana jinsi bora aungane nao, raia wenyewe anao pigania hawaeleweki na ni waoga.
Raia wengi uelewa wao ni mdogo sana, inahitaji nguvu na akili ya ziada bila kusahau uvumilivu kuwabadili kimawazo, bila kusahau wanasiasa wengi wako hapo kuvimbisha matumbo yao.
 
Ingelikuwa ni chama kingine ndicho kimemwalika mwenyekiti wa ccm kwenye shughuli yao, hayo maneno sasa... Mfano ingelikuwa ni ACT, ila kwakuwa ni wao basi wanasems ni mbinu ya kisiasa.
huwezi kuwa mwanasiasa halafu ukaogopa maneno, ganya lile lenye maslahi kwako wanaosema na waseme, hawa waswahili husema mwamba ngoma huvutia kwake,hvyo hizo ni sarakasi za kawaida kwenye siasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…