Kauli hii ya mke wangu ina maana gani?

Demu Hana msimamo kabisa yaani[emoji23]
 
mtu ukiwa umepelekwa kuishi mkoani hasa kijijini kama Kule mbinga huwa na akili nazo zinalala uwezo wa kufikiri zaidi unapungua, na ndiyo maana uliweza kunipata na kunioa Ila ingekuwa tumekutana hapa Dar es salaam, wala hilo lisingewezekana
Akili kumkichwa ISHI NAE KWA AKILI kashakusoma akili yako mkuu, akili sasa imeamka jiji linaamsha akili za watu hili
 
Siku hizi imekuwa kawaida kwa vijana kuja kuweka hadharani mijadala wanayofanya na wake zao wakiwa vyumbani mwao halafu wanakuja kutaka maoni ya akina sisi ambavyo hayatuhusu na wala hatujui mambo yanaendelea vipi huko nyumbani. Ni sawa na mtu kukuonyesha clip ya mjadala halafu anataka maoni yenu.

Hivi hii dunia ya kisasa ikoje? kwani mpaka kila siri ya nyumbani uilete kwenye mitandao kwa mjadala? Matokeo yake unaambia 'huyo hakufai', 'mwache' ... kitu ammbacho kinakufanya uchanganyikiwe wakati pengine bado unampenda mwenza wako.

Imefika muda sasa tuone madhara ya haya mambo na kuwa na umakini nayo.
 
Ushauri mzuri mno
 
dah,ila inauma kwani ni lazima kila kitu uongeee jamani,hali hiyo huwapata watu wengi ila unakaa kimya
mwambie hivi hata mi nashangaa ilikuwaje nikakuoa au uliniwekea limbwata?
by the way haya maisha ukiwa serious sana utapoteza kila kitu emu mpuuzie yawezekana ni hasira au nawe umekuwa ukimsumbua,mpotezee tu
 
msamehe mkuu shida wanawake wakija mjini wanakuwa malimbukeni wanajazana ujinga anaanza kukulinganisha na wanaume wengine,na kama unavyojua mjini kutongozana na kusifiana basi unakuta anaambiwa maneno kama haya kwamba kwa uzuri uliokuwa nao ilibidi uishi maisha ya kifahari kwa hiyo akiangalia ulivyo anaona alikosea anasahau kama wale wanampamba tu
(baadhi ya maneno yao huwa ni kama,*we ni mtoto mzuri sana hutakiwi kuishi maisha ya shida na mwanamke akiwa empty set anayachukua kama yalivo#
 
Wee sio type yake, ulimpata kule Mbinga sababu hakukuwa na type zake ila wee kidg ulikua na nafuu akaona akubali, ila huku Dar ndo kaona wengi wa type yake.

Sasa kazi kwako, kuzika hapa hapa au kusafirisha. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
mtu ukiwa umepelekwa kuishi mkoani hasa kijijini kama Kule mbinga huwa na akili nazo zinalala uwezo wa kufikiri zaidi unapungua, na ndiyo maana uliweza kunipata na kunioa Ila ingekuwa tumekutana hapa Dar es salaam, wala hilo lisingewezekana.
Dah ..aliyesema usimwamini binadamu hata kidogo alikuwa akili kubwa sana.

Hadi hapo huna mke na ameshapoteza sifa ya kuwa mkeo.
Mpe yellow kadi na akizingua zaidi mpe red maisha bila stress yanawezekana.
 
Ushauri wako sio mzuri.
Ndoa haitakiwi kuimarishwa kwa hela au six packs gym.

Unataka afe kisa stress za kuongeza kipato×3 ya alichonacho kisa mke?

Huo muomekana unaomshauri auboreshe ili amuimpres wife inawezekana ila vipi akipata ajali akawa mlemavu utamshauri afanye nini kwenye huo muonekano wake mpya ili wife avutiwe?

Pia tutajuaje kama mkewe kasema hivyo baada ya tabia chafu za huyu ndugu yetu?
Au tuyajuaje mkewe ni wale wanawake wakiwa period hormones zinawapelekesha wanakua kama machizi kwa hasira wanaropokwa hovyo halafu period ikiisha wanajutia?

Hiyo kauli sio nzuri ila mleta mda jaribu kutafuta kinachofanya wife ajione mjinga kuwa na wewe.
Kama kagundua una michepuko basi jitafakari.
Kama anatamani mahandsome boy walamba lips wa Dar au anatamani wenye hela zaidi yako wala usijiue gym wala usiibe kwa ajili yake akitaka asepe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…