Kauli tatu za ajabu sana Tanzania kuhusu vifo vya viongozi

Kwa makamba alitakiwa yeye makamba aje aombe msamaha na rais Samia alitakiwa amfukuze January kwenye uwaziri hata kama geresha ya miezi kadhaa. Unajua wenye kuamini ktk Dkt Magufuli waliona mama alifurahia hiyo kauli
 
Kifo ni njia ya binadamu na viumbe wengine wote. Inakuwaje mtu anafurahia kifo cha mwenzie kwa sababu za kisiasa? Nape na Makamba hawataishi milele; wanaisubiri siku yao ambayo haiko mbali sana ambapo maneno yao hayo yatawarudia.
.... kitabu ulichojiandalia mwenyewe wakati wa uhai wako ndicho kitakachoamua nini kisomwe utakapokufa. Ukijiandalia kitabu chema, watasoma maandishi mema kwenye kitabu chako; lau ukijiandalia kitabu kibovu watasoma upuuzi kutoka katika kitabu chako mwenyewe!

Usilaumu wasoma kitabu; laumu aliyeandaa kitabu!
 
Kauli ya kawaida Sana hiyo Magufuli hakuwahi kutoa kauli ya kufurahia maumivu ya mtu.
Aliwahi kusema atavunja viuno vya mashangazi wa Majaliwa ilihali walikua wanapitia changamoto za korosho. Au kusema wapinzani wakiandamana atawabomoa!! Tena akasema wakae mstari wa mbele kabisa.

Achilia mbali kauli yake ya kuwacheka wahaya kwa kupata matetemeko na ukimwi.
 
Kwa makamba alitakiwa yeye makamba aje aombe msamaha na rais Samia alitakiwa amfukuze January kwenye uwaziri hata kama geresha ya miezi kadhaa. Unajua wenye kuamini ktk Dkt Magufuli waliona mama alifurahia hiyo kauli
Amfukuze January kwa kauli ya baba yake? Mbona Makonda hakufukuzwa kwa kutukana wachagga? More so aliombewa msamaha na Bashiru?

Mama alipinga kauli pale pale na akasema Makamba ameteleza mdomo!! Sasa Cha ajabu watu msamaha wanapotezea Bado wanatembea na kauli ya mwanzo.

Sidhani kama tutasonga mbele tukiendelea kubeba chuki na kusahau msamaha.
 
Unataka nani alaumiwe kama siyo CCM? Acha wafu wazike wafu wao, basi.
 
Maana ya trash inabaki kuwa ile ile tu, uwe umesoma ghorofani au chini ya mti..!! Haiwezi badirika..!!

Kuhusu Idd Amini, tuliaminishwa vile na hadi kwenye nyimbo za mchakamchaka tumeimba sanaa tu..!! Lakini, tatizo ni kuwa hatukuwahi kupata nafasi ya kuujua upande wa pili wa Idd Amini. Kwa bwana JPM tuna upande wake mwingine wa kauli na matendo yake..!! Hakuwa na presidential words/language..!! Kama kiongozi, huwezi waambia watu warudi na mavi yao nyumba, vile vile huwezi waambia watu wapige mbizi kama hawana mia mbili..!! etc. Kulikuwa na namna nyingine ya kuufikisha ujumbe aliokusudia bila kutumia lugha za kejeli..!! Au aliposema jimbo hili haliwezi pata maendeleo kisa wamechagua mpinzani..!! UJINGA MTUPU..!! kwani hao wapinzani hawalipi kodi..!!??

Nakubaliana na ukweli kwamba propaganda ni hatari sana kama zinatumika visivyo..!! Hivi wewe unapotaka kutuaminisha kwa JPM alikuwa mwema sana, HUONI KWAMBA NA WEWE UNAFANYA PROPAGANDA? AU maana ya propaganda ni kuyasema mabaya ya mtu pekee..!!??
 
Baki na mavi yako nyumbani - John Pombe Magufuli, akiwa Magufuli Bus Terminal
Tunazunguzia kumsimanga Marehemu,wakati sisi wote ni Marehemu watarajiwa!ni swala la muda tu!!
 
Unataka nani alaumiwe kama siyo CCM? Acha wafu wazike wafu wao, basi.
Wa kulaumiwa hakuna mwingine zaidi ya CCM..!! Kujenga umoja wa kitaifa ni mchakato, is not a one time event..!! Tumesafiri sana kwa mabasi ya KWACHA, RAILWAY, TRAIN etc yote hiyo ilukuwa ni katika kujenga umoja wa kitaifa, na hasa kwenye kufuta ukabila na some how udini..!! Pale Ifunda Tech tulisoma na watu wanatoka Zanzibar na Mafia. Kwahiyo uunguja wake na some how uislamu wake unakuwa ule wa kupendana na muhehe na mkristo..!! Full stop
 
Tunazunguzia kumsimanga Marehemu,wakati sisi wote ni Marehemu watarajiwa!ni swala la muda tu!!
Hapa marehemu hasimangwi, bali yanatajwa aliyoyatenda..!! Kwani mnapotangaza mnayoyaita mazuri yake, nanyi mnamsimanga? Ni utaratibu ule ule tu wa kuiita sepetu kuwa ni sepetu na si kijiko kikubwa
 
Ila cha ajabu humu msamaha umesahaulika watu Bado wanabeba maneno ya Makamba. Embu tujifunze kutokua na chuki maadam waliomba radhi then we need to move on.
Mzee Makamba kwa umri wake alipaswa kuwa na busara na hekima na hakupswa kuombewa msamaha na mtu ambaye kifikra na kiumri ni mdogo kwake. Na Makamba ule msamaha alipaswa aombe yeye mwenyewe hata kama nikinafiki mbele ya Jamii aliyoikosea.
 
Hapa marehemu hasimangwi, bali yanatajwa aliyoyatenda..!! Kwani mnapotangaza mnayoyaita mazuri yake, nanyi mnamsimanga? Ni utaratibu ule ule tu wa kuiita sepetu kuwa ni sepetu na si kijiko kikubwa
Wwe utasemaje Marehemu asimami tena wakiti hilo linajulikana hata na Mtoto mdogo,au ana ozaa huko, wakati unajua kabisa maiti kuoza ni Jambo la kawaida! Kama hayo siyo Masimango kwa Marehemu ni Nini!!??
 
Unapomsifia anakuwa haozi?
 
1. Mungu kaamua ugomvi
2. Watu wazuri hawafi
3. Keshaanza kuoza.

Naona kama vile kauli hizi zitatutesa sana kwenye umoja wetu kama taifa huko tuendako.
Dhalimu ndio alivunja umoja wa taifa hili. Ni vyema Mungu aliingilia kati.
 
Wwe utasemaje Marehemu asimami tena wakiti hilo linajulikana hata na Mtoto mdogo,au ana ozaa huko, wakati unajua kabisa maiti kuoza ni Jambo la kawaida! Kama hayo siyo Masimango kwa Marehemu ni Nini!!??
Ukipanda ubaya utavuna ubaya.
 
Dullah anamuombea msamaha abdallah........
Hizo kauli zilikuwa msumari wa mwisho tu kwenye Jeneza.
Lakini watu hawakubali tangu mwanzo kwani washatambulika tangu zamani, kama ni genge la mafisadi papa.
 
Hiyo kwake haikuwa chuki bali chuki kwa mujibu wake ni mafisadi kubinywa, wenye vyeti feki kuondolewa kazini
 
1. Mungu kaamua ugomvi
2. Watu wazuri hawafi
3. Keshaanza kuoza.

Naona kama vile kauli hizi zitatutesa sana kwenye umoja wetu kama taifa huko tuendako.
Wanasemaga Kasekaseka kalilalila !! Ukichekacheka baadaye utalialia !! Walioamua kuzifanya siasa kuwa kama uadui itabidi waende wakatubu mapema kabla dhambi hii haijaanza kuwatafuna wao wenyewe !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…