Kauli ya Chongolo ni ufedhuli kwa wasomi wa vyuo vikuu. Ipingwe!

yuko sahihi , ila kuna wakati nashangaa kwa nini serikali inashindwa kuajiri walimu hasa shule za kata unakuta shule mwalimu wa hesabu mmoja shule nzima au fizikia.
 
Sasa why mfungui hizo ofisi ili muwe mmejiajiri?.
 
Kweli wa JKT waende na VETA waende iyo miezi 3 na cheti juu .
 
Elimu ni ujuzi au maarifa unayopewa ili upambane na mazingira yako,

Kama umefika huko panapoitwa Chuo na ukahitimu labda Shahada ya Uchumi lakini miaka 3 au 4 baada ya kuhitimu ukakosa ajira ya kujiajiri au kuajiriwa,ukaona ngoja uende Veta ukapate mafunzo ya Udereva na Ufundi Makanika mbona utakuwa umejiongezea kitu muhimu katika maisha yako na tena unaweza ukapata ajira kupitia mafunzo ya Veta kwa haraka kuliko hilo li karatasi lako la Chuo,
Vijana wa Kitanzania mliopo Vyuo acheni Upumbavu wa kujiona nyinyi ni kundi muhimu sana kuliko mtu yoyote,kufika Chuo haimaanishi huwezi kuwa Fundi Mwashi,Mchomeleaji au Seremala.

Nchi zilizoendelea mtu mmoja unamkuta ana Shahada na bado ana vyeti vidogo hata 10 vya kazi za mikono,hapa Tanzania mtu ukifika tu Chuo basi wewe ni Elon Musk,

Chongolo yupo sahihi,wanachuo acheni ulonyolonyo nendeni Veta!
 
Poyoyo.
Nchi ipo chini ya CCM Alafu Mnajitekenya nakucheka wenyewe
 
Ipi afadhali, VETA au tumehuru? According to Mr Tundu all these problems of ajira and ugumu wa maisha na bei kupanda, jibu lake ni tumehuru.
 
Kwahiyo Chongolo anataka vijana wote wa vyuo vikuu wawe mafundi mchundo ??

Muwe mnaangalia mantiki ya hoja iliyotolewa kwanza kabla ya kukimbilia kuunga mkono hoja mfu.

Daniel Chongolo anapowaambia vijana wa vyuo vikuu waende veta wawe na uwezo wa kujiajiri maana yake elimu yao ya chuo kikuu haina maana yoyote isipokuwa elimu ya veta na kwamba chuo kikuu wamepoteza muda wao bure.

Kuna la maana hapo ??
 
Vitendo katika fani ipi?Anayesomea maendeleo ya jamii anaweza fanya mafunzo ya vitendo vipi ili mtaani ajiajiri?.
Kuna fani zilipaswa kufutwa vyuoni Kama tungekuwa serious. Kama ccm inajua fani hizi hazina practical application mitaani kwann zifundishwa?? CCM ni wangese
 
Isomi wako usio na Tija una manufaa gani Kwako na jamii zaidi ya kuwa mzigo?
Aliyesababaisha niwe mzigo ni ccm. Walipaswa wawekeze vya kutosha ktk vyuo vikuu ili wanafunzi wasome kwa vitendo na siyo kuhubiriwa na kupewa notes tu darasani. Chongolo anapaswa kuwajibika ktk hili.
 
Msomi ndiyo ulipaswa utengeneze PRIVATE SECTOR ndani ya nchi na nje ya nchi,lakini eti wewe unawaza watu waje toka nje ya nchi ndiyo wa anzishe PRIVATE SECTOR ndiyo wewe uajiriwe!.Aisee!Hii ni aibu kwa msomi kuwa na mawazo ya aina hii.
Kwani Singapore wasomi ndo walitengeneza Google?
Sera nzuri ya Serikali ya Singapore iliwaruhusu Google kuja kufungua ofisi nchini kwao na kutengeneza ajira.
 
Kuna shida tu kwenye uandishi wako na unataka utuaminishe ulichokiandika?
 
Mfumo mbovu kwani ni mfumo unique au ndio mifumo ya Dunia?
We mjinga sikiliza. Vyuo vikuu kutoa degree za mahubiri bila vitendo siyo mfumo wa dunia. Nenda kasmea hata diploma tu huko nje utaiona tofauti.

Tatizo lako umesoma chekechea mpk kidoto cha 6 huko Matipwinyo Nanguruwe. Halafu ukaenda kuchukua "digrii" Tandabui University
 
Kasema kweli, shida ni kwamba Serikali imewekeza saba kwenye vyuo vikuu badala ya vyuo ya kati, VETA vilitaliwa kuwa ni vyuo vyenye kupata fund ndefu sana kutoka Serikalini lakini sio hivyo
 
Kasema kweli, shida ni kwamba Serikali imewekeza sana kwenye vyuo vikuu badala ya vyuo ya kati, VETA vilitaliwa kuwa ni vyuo vyenye kupata fund ndefu sana kutoka Serikalini lakini sio hivyo
Unajua maana ya kuwekeza Sana?? Ingekuwa imewekeza Sana wanafunzi wangekuwa wanasoma kwa vitendo zaidi kuliko kuhubiriwa.
 
Toa upumbavu wako hapa wewe fala,watu wangapi wamesoma vyo vya Nje na ni jobless hapa Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…