Kauli ya Mwigulu kuhusu Burundi ni hatari kwa Usalama wa Taifa. Serikali ijitenge nae!

CCM na baraza lao la mawaziri Walishamdharau Mama, Ndio Maana huyu Mashamba Anatuambia Tuamie Burudi Kama Hatukubaliane na Utopolo wake wa Kodi za huduma za Kielectronics.
 
ITV ni kituo kikubwa,sijaona sababu ya kurusha kipindi ambacho walikuwa wanajua kuna mabadiliko baada ya Rais kuingilia na walimsikia hata Mwigulu akiongea pia. ITV wamefanya hivyo makusudi ili kumchonganisha Waziri na Umma.Poor ITV
 
Huyu Waziri hafahamu Sheria za nchi,anavaa tai ya Bendera ya Taifa la JMT kila uchao lakini hana huruma/mapenzi na Watanzania wenzake.Ana mamlaka ya ku-Deport Watanzania kwenda Burundi?

Warundi ndiyo huwa hawalalamiki ama hawalipi tozo halali kwa nchi yao?Hili linatia shaka hata ya Udaktari wake wa uchumi.

Katiba hii iliyopo inasemaje kuhusu au sheria zetu zinaweza kutafsirije kauli kavu kama ya Dr Mwigulu?May be Mh.Diallo was right!
 
Hana bahati yoyote nivile anajua kuramba makalio ya wateuzi
 
Hii nchi bana! Kila mtu ana sharubu.

Hadi Yericko?
 
Mtu anaejua mambo ya miili ya kwenye viroba ni hatari kwa taifa na kwa rais pia
Huyu mtu ni hatari zaidi ndio maana maza kamuacha kiaina
Huyu ni kama makonda kwa magu
Ni ngumu kumpiga chini maana anajua mipango mingi miovu!
So what?Hiyo mipango miovu anayoijua ni dhidi ya nani?CCM mnajitetea au mnajichochea kuni wenyewe kwa kauli zetu.Yaani Mwigulu yupo pale kama hongo asitoe siri za mipango ovu ya nani?
 
Mleta hoja iko hivi.
Kipindi kilichorushwa Jana jioni na ITV nitukio ambalo alikwisha rekodiwa kabla ya maelekezo ya Rais na speech yake ya mchana...
Yes, alitakiwa awaambie wasirushe hicho kipindi kwa sababu kuna taarifa kwa wananchi alizoongea kupitia vyombo vya habari kuhusu tozo. Lakini kuacha kipindi kilichorekodiwa kiende hewani, ni dharau kubwa kwa wananchi na kwa Rais aliyempa maagizo aliyoyasema mchana kabla ya kipindi hiki kuruka hewani jioni.
 
Mwigulu nufaika la ccm, lishashiba pesa, yale maesta bus yote linaachaje kuwa na kiburi.
 
Kuna kauli alitoa eti nisikilize mimi Dr nakuakikishia hii kauli ni yamtu ambaye anajifanya kujua kila kitu na niyakibabe sn
 
Kipindi kiliandaliwa kabla ya jana asubuhi.

Mazungumzo ya jana hayahusiani na kipindi maana kipindi hakikua live jana.

Vitu vingine hutakiwi kua na akili kubwa kujua hilo.
Kwa sababu alijua kina hoja za tozo ambazo tayari ameshapewa maagizo na boss wake (Rais), alitakiwa asitishe kipindi hiki kilichorekodiwa kisiruke hewani, ili hoja alizoongea mchana zibaki kuwa final ili kupisha kikao kilichoitishwa na waziri mkuu kufanyika leo kifanyike na utekelezaji wa maagizo ya Rais ufanyike. Kwa ujumla hicho kipindi kilitakiwa kife kifo cha asili (natural death).

Labda mkuu kama hujui protocols za uongozi wa serikali.
 
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania mko wapi mnaacha mtu kama huyu Waziri anakwenda katika Tv kulichafua Taifa na kumchafua Rais wa Nchi? Miiko ya utumishi wa umma na miiko ya viongozi wa Kiserikali juu ya kwenda katika vyombo vya habari iko wapi?

Waziri anaongea kwa dharau kuliko hata kibri walichokuwa nacho Makonda, Mnyeti na Sabaya enzi za udikteta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…