Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Yani una ndugu kigogo halafu waendesha bajaji?😂🤣only in bongo
 
Acha yamkute Bangi, Ushamba na kutaka Sifa za Kijinga kwa Wana ( Washikaji ) Kijiweni zimemuongoza vibaya.
Hawa boda na bajaj wabadilike kuna wengine jambo dogo tu wanalifanya linakuwa kubwa sijui ni uelewa mdogo. Na silaha wanazipenda sana wengine wanatumia kufanya uhalifu kwa mteja hasa nyakati za usiku.
 
Vijana wengi walishavurugwa (tulishavurugwa) kisaikolojia, wapo wengi ambao hawalipi kuchukua maamuzi magumu kama huyo mtuhumiwa, TUNAKOENDA NI TATIZO KUBWA SANA ZAIDI YA HILI. Kwani vijana hawana ajira, hawako vizuri kichwani, matatizo kibao kila upande, huyo ni mmoja ambaye kamezeshwa sumu na mfumo wa maisha ya sasa, na sio peke yake wapo wengi tu kama huyo,,,
 
Watamdedisha tu
Na ndugu nao hawatakubali watamalizana
 
Kanali upumbavu gani?ukileta ujinga Ahera madukani inakusubiri,yaan mtu anacheo cha tano jeshini anakua na akili za makuruti.


NapitaKamaRadi
Hawa wanajeshi huwa wana ubabe wa kifala sana kuna siku aling'ang'ania kumbeba binti pale mnarani kwenye bar ya fire ila tukamuokoa yule binti badala utongoze unaleta ubabe wa kifala eti mnanijua mimi ni nani
 
Ubabe umezua umauti.
 
Nchi za ulimwengu wa tatu zina mambo mengi sana ya ajabu ajabu
 
Kwahiyo ukimezeshwa sumu ndio uende kuua ?


Kila mtu mwenye ugumu wa maisha akisema awe violent nchi itakalika?


Hawa bodaboda Huwa wanajiona wajanja sana

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu zangu, Cheo ni kazini kwako. Na cheo chenyewe kitakutumikia endapo utajihesimu na kufata misingi na taratibu.

Thamani ya uhai, ni sawa kwa kila mmoja. Hakuna cha kanali wala cha dereva boda, thamani ya uhai wetu zinalingana.

Muheshimu kila mmoja na epuka ugomvi kwa gharama yeyote. Usianzishe ubabe wako kwa sababu ya nafasi yako. Tena sehemu yenyewe ni sehemu ya kulewa. Kila mtu akili zimeshamruka. Damu zinatembea kasi, pombe inakuwa kiongozi.

Mimi ni raia, ila kitu ambacho labda kitaniua siku moja ni kutokubali kuonewa. Sipo tayari kuonewa kwa gharama yeyote.

Iwe Generali au kuruta au raia mzibua vyoo, kila mmoja amheshimu mwenzake. Timing ni kitu kibaya sana. Na utajitutumua ukiwa hai tu. Ukishapigwa bisibisi ukafariki, huna tena cha kufanya. Na mateso atakayopokea muuaji wako hayana tena thamani kwako, haitarudisha uhai wako.

Eti umchape mtu makofi kwa sababu wewe ni mwanajeshi? Kuondoa tu gari na kumpisha mtu na mikosi yake apite ingepunguza nyota? Akili finyu.

Nachukia sana hii misemo kuwa kuna baadhi ya watu kwa sababu ni walinzi, wana uwezo wa kujiamulia kufanya chochote. Huu ni upumbavu.

Ukitaka kuheshimika, heshimu wenzako kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…