Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Sema washua wenye mamlaka huwaga wanajisahau sana , Kuna video nmeona mtandaoni Kuna dogo alikua anaendesha ist alichomekeana na land cruiser flan nyeus jamaa akaamza kumletea ubabe wa ki CIA dogo road kila akienda huku jamaa linamzibia njia dogo akaenda TikTok live akawa ana broadcast the whole shit maana alishahis hatari jamaa kufika makumbusho aka block njia akashuka kwa gar akaonekana na suti yake ya uzalendo nadhan alipigia wadau wakatoka mule chimbo lao la idara wakamuongoza dogo kuingia tunduni aku anaendelea kurusha mubashara tukio watu wa mabaka ya kenge wakashtukia kama mwamba anawarekodi ndo nkajua kabisa mwamba kaisha mule ndani kamera hapapatani kabisa na msala wa dogo sidhan ata familia yake kama inaweza kuusovu labda kwa vile sura za wahusika ziko online zinaweza kutumika kwenye mahakama za jadi kupata haki kama hakuachiwa lakin
Hiyo video ya zamani sana
 
Wacheza karate, Boxing, anaye miliki silaha, mwanajeshi, polisi, usalama wa taifa na hawa field force ni kundi la watu ambao hata ukimkanyaga mguuni bahati mbaya wakati unapanda daladala lazima atataka akuthibitishie kwamba ye ni nani(sio wote baadhi)...

Sasa uraiani watu maisha yamewachanganya, ukitaka kuleta habari zako za ubabe wa kishamba utamalizwa unajiona.
 
Majeshi ni vyombo vinavyotumia nguvu katika utekelezaji wa dhima ya uwepo wake. Hivyo, ni vema kila raia akawa anatambua na kuliheshimu hilo.

Vilevile majeshi huwa na utaratibu wake wa kulinda taswira na hadhi za majeshi hayo. Hivyo, aina yoyote ya kuyakosea adabu hadharani, ni lazima ile kwako.

Pekee kinachohitaji majeshi haya toka kwa raia ni kuheshimika tu. Ukithubutu kumvunjia heshima Mwanajeshi yeyote yule, Wadepo wenzake hawatakuacha.

Wadepo hubaki kama familia hata kama watapangwa kwenye kambi tofauti. Watajikusanya tu wakujie kwa ajili ya heshima ya jeshi.

Ova
 
Wacheza karate, Boxing, anaye miliki silaha, mwanajeshi, polisi, usalama wa taifa na hawa field force ni kundi la watu ambao hata ukimkanyaga mguuni bahati mbaya wakati unapanda daladala lazima atataka akuthibitishie kwamba ye ni nani(sio wote baadhi)...

Sasa uraiani watu maisha yamewachanganya, ukitaka kuleta habari zako za ubabe wa kishamba utamalizwa unajiona.
Yaani inashangaza sana,unampiga mtu makofi,ili?
Sasa amekuchoma na bisibisi umekufa,wakati labda ungemuelimisha tu,kua dogo ngoja nipite,au unatumia saikolojia tu,mnayamaliza.Hii yakuamini askari anaweza akamdhibiti yeyote,inaleta changamoto.Hapo ukute kanali aliwaza tu kua kwasababu yeye ni mwanajeshi,akimpiga makofi,dogo ataomba msamaha,kumbe dogo kavurugwa,mwishowe ni kufa eti kwa kukitwa na bisibisi... aisee.
 
Majeshi ni vyombo vinavyotumia nguvu katika utekelezaji wa dhima ya uwepo wake. Hivyo, ni vema kila raia akawa anatambua na kuliheshimu hilo.

Vilevile majeshi huwa na utaratibu wake wa kulinda taswira na hadhi za majeshi hayo. Hivyo, aina yoyote ya kuyakosea adabu hadharani, ni lazima ile kwako.

Pekee kinachohitaji majeshi haya toka kwa raia ni kuheshimika tu. Ukithubutu kumvunjia heshima Mwanajeshi yeyote yule, Wadepo wenzake hawatakuacha.

Wadepo hubaki kama familia hata kama watapangwa kwenye kambi tofauti. Watakikusanya tu wakujie kwa ajili ya heshima ya jeshi.

Ova
Sidhani kila sehemu,nguvu inahitajika kuliko akili.Muheshimu mwananchi,naye akuheshimu,ukitaka uheshimike wewe tu,eti kisa ni mwanajeshi,matokeo yake ndo hayo,unakitwa na kitu chenye ncha kali,unatangulia.Mambo yamebadilika... ubabeubabe,hata mimi sikubali,ukinivunjia heshima,napambana kulinda heshima yangu pia.
 
kuna cha kujifunza hapa.

Wanajeshi wengi huku mitaani wamekosa nidhamu sana na wanaishi kwa style hiyo hiyo kama ya marehemu, hutumia mara nyingi uanajeshi wao kutaka kupata heshima uraiani.

Jeshi linahitaji kutengeneza nidhamu ya hali ya juu kwa askari wake hasa maisha yao ya uraiani na wananchi wa kawaida, na hii si kwa jeshi tu hata kwa vyombo vingine vya usalama.

Alichokifanya dereva wa bajaji kulingana na maelezo hapo juu kinaweza kufanywa na yeyote asiyependa kuonewa, watambue tu huku uraia sio uwanja wa medani bali huku hata uwe komandoo unaweza kuviziwa ukapigwa ambush ukapoteza maisha.
 
Askari wetu watambue tu mfumo wa maisha umebadirika sana, hali yamaisha imefanya vijana wengi mitaani kutokuwa na nidhamu za uoga tena hata inapofikia mazingira kama haya ya kuonewa.

Ubabe na kutaka heshima za kijinga eti kwakuwa wewe ni askari hayo yamepitwa na wakati na vyombo vya usalama vinapaswa kuelimisha watu wake namna sasa ya kuishi na wananchi huku uraiani maana huko mbele hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Tukifanya masikhara na kushindwa kuchukua hatua, huko mbele panaweza kutokea mapigano ya mara kwa mara baina ya raia na hawa askari.
 
Majeshi ni vyombo vinavyotumia nguvu katika utekelezaji wa dhima ya uwepo wake. Hivyo, ni vema kila raia akawa anatambua na kuliheshimu hilo.

Vilevile majeshi huwa na utaratibu wake wa kulinda taswira na hadhi za majeshi hayo. Hivyo, aina yoyote ya kuyakosea adabu hadharani, ni lazima ile kwako.

Pekee kinachohitaji majeshi haya toka kwa raia ni kuheshimika tu. Ukithubutu kumvunjia heshima Mwanajeshi yeyote yule, Wadepo wenzake hawatakuacha.

Wadepo hubaki kama familia hata kama watapangwa kwenye kambi tofauti. Watakikusanya tu wakujie kwa ajili ya heshima ya jeshi.

Ova
Sasa mkuu wanajeshi wetu tunawapenda sana wakisema wawe wanatumia Nguvu kila sehemu si watatumaliza?
Maana kuna wakati tunakutana kwenye demu moja na kavaa kiraia au yuko kwenye Daladala konda anataka nauli yake.
 
Wacheza karate, Boxing, anaye miliki silaha, mwanajeshi, polisi, usalama wa taifa na hawa field force ni kundi la watu ambao hata ukimkanyaga mguuni bahati mbaya wakati unapanda daladala lazima atataka akuthibitishie kwamba ye ni nani(sio wote baadhi)...

Sasa uraiani watu maisha yamewachanganya, ukitaka kuleta habari zako za ubabe wa kishamba utamalizwa unajiona.
Kwenye hiyo orodha ondoa Karateka, hao huwa ni watu wenye nidhamu ya hali ya juu sana ndani na nje ya Dojo.
 
Inasemekana ( kwa aliyenipa Taarifa Kamili kuwa ) Dereva Bajaji jana Usiku katika Baa Moja maarufu iliyo kwa ndani ( Mafichoni kidogo ) mkabala na Petro Station ya PUMA Kawe alipishana Kauli na Mwanajeshi ( tena Mkubwa wa Cheo cha Kanali ) kuhusu Kuzibiana njia ya kupita.

Ambapo Afande Kanali alikuwa Kapaki Gari lake lililokuwa limezuia njia kwa mbele na Dogo ( Dereva Bajaji ) kuhoji kwanini Afande aliziba njia hali iliyomkwaza Afande ( wa Cheo cha Kanali Muro kama sijalikosea Jina lake ) ambapo Afande Kanali akatoka ndani ya Gari lake na Kumzaba Makofi Dereva Bajaji huyo.

Kisha nae ( Dereva Bajaji ) kwa Hasira akaamua kwenda kuchukua Bisibisi Bajajini Kwake na kuja Kumchoma nayo Afande Kanali upande wa Moyo hali iliyomfanya akimbizwe Lugalo Hospital kwa Matibabu na Umauti kumkuta huko huko Wodini.
Kwahiyo boda boda kaua mwanajeshi?

Duh
 
Wanajitolea au wanalipwa?
Mkuu nijuavyo mimi,wanajeshi wanalipwa mishahara na posho kwaajili ya kutimiza majukumu ambayo yanawapasa.Mimi nawewe,tunalipa kodi,ambazo hizo kodi zinalipwa kwa kila askari wa JW na kada nyingine.Ukisema sisi tumelala,wengine wanatulinda,hujui kuna bodaboda wanakesha pia,kutafuta pesa au kuna madaktari wanafanya C-section usiku huu na yawezekana wakakesha,huku baadhi ya wanajeshi ambao hawako shift usiku huu,wamelala au wanalewa?
Heshimu kila mtanzania.Tunaumia kulipa kodi,ili mambo yaende,kila mtu anapambana kwa nafasi yake.
🙏🏿🧢
 
Majeshi ni vyombo vinavyotumia nguvu katika utekelezaji wa dhima ya uwepo wake. Hivyo, ni vema kila raia akawa anatambua na kuliheshimu hilo.

Vilevile majeshi huwa na utaratibu wake wa kulinda taswira na hadhi za majeshi hayo. Hivyo, aina yoyote ya kuyakosea adabu hadharani, ni lazima ile kwako.

Pekee kinachohitaji majeshi haya toka kwa raia ni kuheshimika tu. Ukithubutu kumvunjia heshima Mwanajeshi yeyote yule, Wadepo wenzake hawatakuacha.

Wadepo hubaki kama familia hata kama watapangwa kwenye kambi tofauti. Watakikusanya tu wakujie kwa ajili ya heshima ya jeshi.

Ova
Kama wao ni wanaume kwanini wanakuja WENGI? Si aje mmoja mmoja bila silaha?
 
Back
Top Bottom