Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Ndugu zangu, Cheo ni kazini kwako. Na cheo chenyewe kitakutumikia endapo utajihesimu na kufata misingi na taratibu.

Thamani ya uhai, ni sawa kwa kila mmoja. Hakuna cha kanali wala cha dereva boda, thamani ya uhai wetu zinalingana.

Muheshimu kila mmoja na epuka ugomvi kwa gharama yeyote. Usianzishe ubabe wako kwa sababu ya nafasi yako. Tena sehemu yenyewe ni sehemu ya kulewa. Kila mtu akili zimeshamruka. Damu zinatembea kasi, pombe inakuwa kiongozi.

Mimi ni raia, ila kitu ambacho labda kitaniua siku moja ni kutokubali kuonewa. Sipo tayari kuonewa kwa gharama yeyote.

Iwe Generali au kuruta au raia mzibua vyoo, kila mmoja amheshimu mwenzake. Timing ni kitu kibaya sana. Na utajitutumua ukiwa hai tu. Ukishapigwa bisibisi ukafariki, huna tena cha kufanya. Na mateso atakayopokea muuaji wako hayana tena thamani kwako, haitarudisha uhai wako.

Eti umchape mtu makofi kwa sababu wewe ni mwanajeshi? Kuondoa tu gari na kumpisha mtu na mikosi yake apite ingepunguza nyota? Akili finyu.

Nachukia sana hii misemo kuwa kuna baadhi ya watu kwa sababu ni walinzi, wana uwezo wa kujiamulia kufanya chochote. Huu ni upumbavu.

Ukitaka kuheshimika, heshimu wenzako kwanza.
Wewe andika tu, hujawahi kuwana bad day. Hujawahi tukanwa wewe mpaka ukahisi umedharauliwa sana. Omba isikutokee
 
Ubishi muda mwingine bhana, ona sasa kaacha cheo chake kizembe

Apumzike panapo mstahili ila tu naomba hii kesi iendeshwe kwa uwazi maana huyo dereva wanaweza kumzima pia

Ikumbukwe hayo ni mauaji kama mauaji mengine tu anastahili kupelekwa mahakama za kawaida tu na sio za kijeshi,

Pole sana dereva bajaji huko uliko kama nakuona hivi ambavo washakufanya hamna.
hkuna kesi apo tunadeal nae vizuri tu ataenda kusomewa mashtaka kuzimu
 
Sasa dogo kafanya tukio kubwa kama hilo angetakiwa kupotea mazima na bajaj yake.
Alichokosea alipomchomoa Bisibisi Afande ( Kanali ) na kuona Kamjeruhi vibaya ( nadhani kwa Kuchanganyikiwa ) akaamua Kukimbia na kuiacha Bajaji yake ambayo ilikamatwa na ndiyo imerahisisha pia hata Yeye Kukamatwa kwani Watu wake wa Kijiweni walitoa Ushirikiano.
 
Inasemekana ( kwa aliyenipa Taarifa Kamili kuwa ) Dereva Bajaji jana Usiku katika Baa Moja maarufu iliyo kwa ndani ( Mafichoni kidogo ) mkabala na Petro Station ya PUMA Kawe alipishana Kauli na Mwanajeshi ( tena Mkubwa wa Cheo cha Kanali ) kuhusu Kuzibiana njia ya kupita.

Ambapo Afande Kanali alikuwa Kapaki Gari lake lililokuwa limezuia njia kwa mbele na Dogo ( Dereva Bajaji ) kuhoji kwanini Afande aliziba njia hali iliyomkwaza Afande ( wa Cheo cha Kanali Muro kama sijalikosea Jina lake ) ambapo Afande Kanali akatoka ndani ya Gari lake na Kumzaba Makofi Dereva Bajaji huyo.

Kisha nae ( Dereva Bajaji ) kwa Hasira akaamua kwenda kuchukua Bisibisi Bajajini Kwake na kuja Kumchoma nayo Afande Kanali upande wa Moyo hali iliyomfanya akimbizwe Lugalo Hospital kwa Matibabu na Umauti kumkuta huko huko Wodini.
Hapa ndipo shetani alipochukua point zake..dah hasira hasara
 
Alichokosea alipomchomoa Bisibisi Afande ( Kanali ) na kuona Kamjeruhi vibaya ( nadhani kwa Kuchanganyikiwa ) akaamua Kukimbia na kuiacha Bajaji yake ambayo ilikamatwa na ndiyo imerahisisha pia hata Yeye Kukamatwa kwani Watu wake wa Kijiweni walitoa Ushirikiano.
Yeah too bad alipanic aisee.
Hapo hawatomuacha salama.
Sijui hata ndugu kama wakienda police kuhimiza ndugu yao ashtakiwe mahakamni kama watasikilizwa.
 
Duuh inasikitisha sana kama ni kweli ila hawa jamaa muda mwingi wanakosea mengi kwa kujiona hawagusiki........sasa kama nikweli mtu mwenye mafunzo mpaka cheo hiki anakufa kibwege namna hii? Kwasababu ya parking? Afande gani mwenye mafunzo na inaonyesha alikuwa senior jeshini anakosa busara na hekima kiasi hiki.
Ni kukosa busara na ulevi wa madaraka
 
Sasa mkuu wanajeshi wetu tunawapenda sana wakisema wawe wanatumia Nguvu kila sehemu si watatumaliza?
Maana kuna wakati tunakutana kwenye demu moja na kavaa kiraia au yuko kwenye Daladala konda anataka nauli yake.
Watawamaliza nyie mayai mayai. Tutamalizana. Kwani hapo aliyemalizwa mpaka sasa ni raia au mwanajeshi? Acheni woga. Wanajeshi ni watu tu kama wengine
 
Inasemekana ( kwa aliyenipa Taarifa Kamili kuwa ) Dereva Bajaji jana Usiku katika Baa Moja maarufu iliyo kwa ndani ( Mafichoni kidogo ) mkabala na Petro Station ya PUMA Kawe alipishana Kauli na Mwanajeshi ( tena Mkubwa wa Cheo cha Kanali ) kuhusu Kuzibiana njia ya kupita.

Ambapo Afande Kanali alikuwa Kapaki Gari lake lililokuwa limezuia njia kwa mbele na Dogo ( Dereva Bajaji ) kuhoji kwanini Afande aliziba njia hali iliyomkwaza Afande ( wa Cheo cha Kanali Muro kama sijalikosea Jina lake ) ambapo Afande Kanali akatoka ndani ya Gari lake na Kumzaba Makofi Dereva Bajaji huyo.

Kisha nae ( Dereva Bajaji ) kwa Hasira akaamua kwenda kuchukua Bisibisi Bajajini Kwake na kuja Kumchoma nayo Afande Kanali upande wa Moyo hali iliyomfanya akimbizwe Lugalo Hospital kwa Matibabu na Umauti kumkuta huko huko Wodini.
Huyo mjeshi kifo kakitaka Hawa askari wanazidi Sana ubabe Kwa raia watu wnaa stress bwana
 
Sema washua wenye mamlaka huwaga wanajisahau sana , Kuna video nmeona mtandaoni Kuna dogo alikua anaendesha ist alichomekeana na land cruiser flan nyeus jamaa akaamza kumletea ubabe wa ki CIA dogo road kila akienda huku jamaa linamzibia njia dogo akaenda TikTok live akawa ana broadcast the whole shit maana alishahis hatari jamaa kufika makumbusho aka block njia akashuka kwa gar akaonekana na suti yake ya uzalendo nadhan alipigia wadau wakatoka mule chimbo lao la idara wakamuongoza dogo kuingia tunduni aku anaendelea kurusha mubashara tukio watu wa mabaka ya kenge wakashtukia kama mwamba anawarekodi ndo nkajua kabisa mwamba kaisha mule ndani kamera hapapatani kabisa na msala wa dogo sidhan ata familia yake kama inaweza kuusovu labda kwa vile sura za wahusika ziko online zinaweza kutumika kwenye mahakama za jadi kupata haki kama hakuachiwa lakin
Wana masifa mnoo àfu wanapenda ubabe
 
Pole sana kwa familia ya marehemu.Tukio hilo,litumike kama funzo kwa waliobaki,kupiga wananchi,siyo vema,unampiga mtu makofi,akiriakti?
Inasikitisha sana,unaacha familia hivihivi,ulifunzwa kupambana na adui hasa mwenye bunduki au bomu,leo unauawa na bisibisi,aisee.
Mungu tu kamdhalilisha huyo askari
 
Magari yamepita asubuhi Mzee wewe umelala yamepita malori kibao yamebeba wanajeshi yanatoka Lugalo, endelea kulala wao hawalali wanakulinda wewe na mipaka ya Nchi yako
acha kusifia ujinga,mipaka ya nchi inalindwa kwa kupiga raia?.

na jeshi la polisi litakuwa na kazi gani kama jwtz wanaingia mtaani kukimbizana na vijana wa bodaboda?.
 
Majeshi ni vyombo vinavyotumia nguvu katika utekelezaji wa dhima ya uwepo wake. Hivyo, ni vema kila raia akawa anatambua na kuliheshimu hilo.

Vilevile majeshi huwa na utaratibu wake wa kulinda taswira na hadhi za majeshi hayo. Hivyo, aina yoyote ya kuyakosea adabu hadharani, ni lazima ile kwako.

Pekee kinachohitaji majeshi haya toka kwa raia ni kuheshimika tu. Ukithubutu kumvunjia heshima Mwanajeshi yeyote yule, Wadepo wenzake hawatakuacha.

Wadepo hubaki kama familia hata kama watapangwa kwenye kambi tofauti. Watakikusanya tu wakujie kwa ajili ya heshima ya jeshi.

Ova
Ndo kafa sasa Kwa kuchomwa bisibisi Kwa kulamisha hizo nguvu
 
Kwa nchi za wenzetu ukishamkorofisha mtu kama ivo ukamuona anazama katk gari yake kwa jazba juwa anatoka na silaha, ila unaweza kuta dogo hakutumia ustaarabu katik kuomba njia hata mimi ukini disrespect hata kama upo na haki nakunasa vibao mengineyo ni ajali kama ajali zingine
 
Back
Top Bottom