Ndugu zangu, Cheo ni kazini kwako. Na cheo chenyewe kitakutumikia endapo utajihesimu na kufata misingi na taratibu.
Thamani ya uhai, ni sawa kwa kila mmoja. Hakuna cha kanali wala cha dereva boda, thamani ya uhai wetu zinalingana.
Muheshimu kila mmoja na epuka ugomvi kwa gharama yeyote. Usianzishe ubabe wako kwa sababu ya nafasi yako. Tena sehemu yenyewe ni sehemu ya kulewa. Kila mtu akili zimeshamruka. Damu zinatembea kasi, pombe inakuwa kiongozi.
Mimi ni raia, ila kitu ambacho labda kitaniua siku moja ni kutokubali kuonewa. Sipo tayari kuonewa kwa gharama yeyote.
Iwe Generali au kuruta au raia mzibua vyoo, kila mmoja amheshimu mwenzake. Timing ni kitu kibaya sana. Na utajitutumua ukiwa hai tu. Ukishapigwa bisibisi ukafariki, huna tena cha kufanya. Na mateso atakayopokea muuaji wako hayana tena thamani kwako, haitarudisha uhai wako.
Eti umchape mtu makofi kwa sababu wewe ni mwanajeshi? Kuondoa tu gari na kumpisha mtu na mikosi yake apite ingepunguza nyota? Akili finyu.
Nachukia sana hii misemo kuwa kuna baadhi ya watu kwa sababu ni walinzi, wana uwezo wa kujiamulia kufanya chochote. Huu ni upumbavu.
Ukitaka kuheshimika, heshimu wenzako kwanza.