Kaya 644 Magomeni kota zagomea kusaini mkataba kununua nyumba

Si ndo demokrasia na uhuru uliopitiliza. Kila mtu anadhani anauwezo wa kuamka asubuhi na kulia shida zake na zikatatuliwa.
Hili swala sijui lilianzia wapi
 
Hakika,Serikali isimamie hvyo hvyooo
 
ila ninachowaonea huruma, watakaokaa mle, wajue kuna service charge (umeme, maji, majitaka,usafi). ama la, yatakuwa magofu kama ya nyumba za polisi muda si mrefu.
 
Kwahiyo unataka kusema hakuna aliyeunganishiwa umeme kwa 27K
Hata mimi nilifungiwa kwa 27k, lakini hii bei ya magu haiakisi bei halisi ya kuwekewa umeme. Bei tu ya ule waya wa kutoa umeme kwenye nguzo ya tanesco kuuleta kwenye nyumba yako ni 10k kwa mita. Bado mita na vitu vingine
 
Hahaha.. Mbeleko imeanza kutatuka.
 
Nyumba za makazi zikijengwa Chanika hizo biashara kwenye hayo maeneo zitafanywa na wanyama au wadudu?
Kwanza fahamu maana ya CBD, yaani central business district, yaani unasafiri kuja eneo la biashara kufanya kazi na kurudi maeneo ya mbali ya makazi ambayo ni nafuu kimakazi!! Huna kazi yenye kueleweka unang'ang'ania kukaa CBD kimakazi!??? Hapana!! Hata ulaya haipo
 
Ni uhuni uko hapo magomen. Kuna mana tuko mtaa mmoja ameachiwa nyumba na mumewe.

Ameifungia chini tena ipo vizuri. Kaenda kupiga kambi kule magomeni ili ionekane hana nyumba. Na ana mtoto mmoja tu. Tena ni mvuta bangi. Aliyekataa hata kusoma.

Yaani watanzania ni mara nyingi tunalaumu viongozi lakina hata sisi tunu ya uzalendo hatuna. Na anajidai ameokoka. Kwanini asiache wenye uhitaji kweli wakakaa humo? Mungu atusanehe hakii.
 
Basi NHC ina ugonjwa wa kufisha. Kwanini wanatizama hayo yakijiri.?
 
Kwani wakati wanajengewa maghorofa walikubalianaje?

Hapa kuna changamoto hsikutolewa elimu kwa kina.

Bei huenda ikawa sawa, hivi Magomeni kupata eneo pekee(kumhamisha mtu) yake ni kiasi gani?
 
Kwani wakati wanajengewa maghorofa walikubalianaje?

Hapa kuna changamoto hsikutolewa elimu kwa kina.

Bei huenda ikawa sawa, hivi Magomeni kupata eneo pekee(kumhamisha mtu) yake ni kiasi gani?
Walipewa Kodi miaka 3 wakapange kwengine,
Wakaambiwa watarudi wakae bure miaka 3.

Kwa hili nawalaumu serikali.

Inakuwaje mpangaji wa eneo la serikali wageuzwe kama wamiliki wa eneo?
Hao wakazi wa magomeni kota ni wapangaji tu.
walipaswa wapewe notice ya kuondoka ,,
Kama watashindwa kulipa gharama husika.

A tenant will always be a tenant.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Basi NHC ina ugonjwa wa kufisha. Kwanini wanatizama hayo yakijiri.?
NHC wanakuwa hajuwi kama watu wanauziana umiliki wa upangaji.

Mfano Mimi nina rafiki yangu alikuwa mpangaji pale ghorofa za keko NHC.
Ilikuwa ni chumba na siting room,Jiko choo,store,

Jamaa kipindi kile 2005 alikuwa akilipa 50000 tu.
Akaja akatokea mtu akampisha kwa 7 millions cash.
Yeye akahamia kwenye nyumba yake aliyojenga.
Kinachofanyika ni mpangaji wa zamani kwenda NHC na kubadilisha umiliki wa upangaji kwa mpangaji mpya.

Mpangaji ataendelea kulipa pesa Ile Ile kila mwezi,
Hakuna mambo ya pesa ya udalali wala Kodi ya mwaka mzima ..

Kwahyo hizo NHC flats za Posta,kkoo,Upanga zote zilikuwa zinamilikiwa na watu weusi baadae wakawauzia wahindi na waarabu.,

Hao wapangaji wa magomeni kota wasilete janja janja ,,
Kama hawana cash wakanunuwe kisemvule na chamazi.
Watapata nyumba kwa pesa hizo 12 millions na sio magomeni.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Watafutiwe Viwanja chalinze, wajengewe chumba sebule wapewe!, ili kupisha wenye uwezo wazinunue kwa bei stahili 75-80ml.
 
Watafutiwe Viwanja chalinze, wajengewe chumba sebule wapewe!, ili kupisha wenye uwezo wazinunue kwa bei stahili 75-80ml.
Wasijengewe nyumba waliovunjiwa nyumba zao ,
Tena walikuwa wamiliki halali wa maeneo yao,
Wajengewe watu ambao ni wapangaji..


Kamai litaiwezekana hilo basi Africa kweli ni
shit hole

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Duniani hakuna kitu cha bure, hao wananchi walipaswa kulielewa hilo tangu awali...

Kitachofanyika labda ni kupunguziwa makato kwa mwezi lakini sio kukaa bure wakati serikali iliweka mpunga wake hapo...
 

12m? Kweli hamna shukrani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…