Kazi ya Ualimu imeniharibia maisha yangu. Sisemi msiisomee la hasha!

Kazi ya Ualimu imeniharibia maisha yangu. Sisemi msiisomee la hasha!

Hivi baadhi yenu mnaojiita walimu mna akili timamu kweli?
Yaani unakutana na changamoto za kazini kwako unazihamishia jamiiforums?

Ulishawahi kuona mwanajeshi, askari polisi, usalama wa taifa madaktari n.k wanafungua nyuzi kulalamikia mambo ya kazi zao?

Kwani hamkai vikao mkayasema huko kuliko kujivua nguo humu?

Je, kuna kada yenye ubabe mwingi na kupelekeshana kama za majeshi? Mbona wao hawaji humu kulalamikia changamoto za kazi zao?

Hamna maadili ya kazi!
We ni HRO wa wapi?
Ni DHRO, THRO, MHRO, au Mkurugenzi Rasilimali watu?

#YNWA
 
Basi UALIMU ni kazi? Ni watu wanaohangaika kutafuta unga tu, na ukiona mwalimu ana maji ya Dasani mkononi anatembea nayo ujue aliitwa kwenye kikao cha platnum wanaotafuta waombaji wa Mikopo
Acha dharau kuna walimu ni madon kwa sasa , wana business za kutosha hayo maji ya kunywa ni pesa ndogo mno kwao.

Ni kweli salary ya ualimu ni ndogo kimfumo ila kazi ya ualimu ukiwa makini unatoka kimaisha tu kwa sasa.
Ni mfumo tu mbovu wa nchi yetu ila kazi ya ualimu ni njema kabisa
 
Sijui nikuelezeje lakin huwez acha kazi kisa eti una dharauliwa ww ulipata kazi nzuri, wachungaji wa dini wanadharailiwa Sana lakin kwa sababu ya wito hawaachi kazi, nasema hvi usinge kuwa umepata hyo kazi kweli Sasa hv ungekua Bado mwl ,
Alafu dharau ni jinsi wewe unaichukulia mtu akikudharau ukampuuza nothing will affect you,
Lakin akikudharau ukaweka kichwani utaona umedharauliwa ,
Nchi yetu Bado Haina pesa ya kulipa walim kama USA Kule ili uwe mwl lazima kwanza uwe na div 1 yaan bright ndo wanatakiwa kuwa walim,
Sisi uku kwetu Bado , mtu ana div 4 anaenda kufundisha ,
Shukuru Mungu ulipata huo ualim walio kudharau walikua wanakupa changamoto Sasa ilibidi uishide ,

Mimi sio mwl kozi yangu nimemaliza 2016 since now Sija ajiriwa , before sijasoma hii kozi nilitaka nianzishe twishen eneo nililokua nakaa hakukua na kindergarten, nilitaka niombe pale kanisan niweke kindergarten na ningetoboa,.
Sasa ambae angenidharau si ningemcheka tu,

Bahati nzuri nikaenda somea hii kozi,

My dear dharau Ni jinsi wewe unaichukulia kwa hyo wale wanaume wanao tembeza mboga barabarani au sokonj na ni wanaume nao vip ,
Fikilia Wana dharauliwa kiasi Gani ?
Waache kisa dharau,

NB; hakuna kazi isiyo kuwa na changamoto hata apo ulipo Zinakuja au hujazisema
Hakika ,
Kuna watembeza maandazi mijini wanaingiza mamilion kwa mwezi kuliko mtu aliyeajiriwa.

Jamaa aheshimu kazi , hatuwezi kulingana katika maisha kamwe
 
Walimu wengi wmetoka familia duni. Mshahara 600+ lakini ukoo mzima wanataka mgao [emoji23][emoji23][emoji23] sasa huyu mtu atatoboa lini jameni?
Kutoka familia duni ni watumishi wengi wauma wametoka familia duni sio walimu tu ,udaktari ,uafisa ugani ,usekretari ,ukutubi ,masjala ,uaskari, wote hao
 
Ninapata allowance
(1)usafiri.
Zamani nilikuwa natumia miguu, nikakopa nikununua bodaboda ikawa inanisadia. Nadhani hii ndio Hali wanayoishi walimu kwa Sasa. Hujajiongeza utaishi Kwa taabu.

Kwa Sasa transport allowance IPO. Namshukuru Mungu.

(2) House allowance IPO. Awali nilipangisha. Nikakopa nikajenga Kwa taabu Sana.

Serikali inattuhadaa Sana hapa kujenga nyumba za walimu"kwio"

Najiuliza kwanini sikupata hii kazi mapema? Mwalimu asipojipanga ataishia kuishi maisha ya taabu.

(3) Heshima. Jamani hakuna Jambo muhimu katika maisha kama heshima.
Mkuu hujafafanua ulipata vipi kazi nyingine uliacha au ilikuwaje
 
Kazi ya Ualimu ilikuwa ngumu pale:
  • Shule DED na DEO walipojibinafshia shule za umma kupitia Ike Decentralisation. Kwa sasa mkuu wa shule/ mwalimu mkuu ni mkibarua (kama part time) wa DEO, DED, REO, n.k.
  • Kutaka wanafunzi wenye maandalizi duni kabisa, kushindwa kushindwa kuhesabu, kuandik n.k wafaulu.
  • Kwenye vikao maafisa WA mkoa na wilaya walipoanza kuwafokea wasimamizi wa shule kana kwamba wanafokea ng'ombe kutukana na ufaulu duni ktk eneo husika la utawala; ili hali ukweli unajulikana.
 
Back
Top Bottom