Kazi ya Ualimu imeniharibia maisha yangu. Sisemi msiisomee la hasha!


Shukuru Mungu ulipata pa kuanzia. Kuna wenzio wanasota mpaka leo hawajui waanzie wapi. Ualimu ukituliza akili unatoboa vizuri sana mi mwenyewe nimeanzia huko ila leo hata ada ya 10m kwa mwaka namlipia mtoto.
 
Wanaopokea Hy 600+ ni wachache wengi mishahara tayari ina virus unakuta mkononi mwl anaondoka na 250+ bas
Acha uongo kijana.

Mshahara una madaraja serikali kote

TGTS
TGS
PUTS
PHSS
LSSE.

hakuna mwalimu mwenye certificate anaeliowa laki mbili labda awe amaechukua mkopo mkubwa.

Mnatia chumvi sana humu ndani hakuna uhalisia

Mnachuki na walimu.
 
Noma sana walimu wenye miaka 9 kazini wenye bachelor saizi ndio wanapokea 990k

Daktari anayeanza anakunja 1.3m[emoji3]

Hatari sana
Daktari anaanza anakunja 1.4 point something.

Akikatwa Makato na bodi ya mkopo anabakiwa laki 8 na ushee.

Akikopa ndio kisanga kabisa

Wafanyakazi wa serikalini wote wanafanana Hali zao basi tu Kuna baadhi ha vitengo vina viposho vya hapa na. Pale.

Walimu wanekuwa na posho Kila mwezi mngona fujo zao mtaani
 
Ukienda shule hakuna wa kukunyangasa hata kama kakuzidi cheo na mshahara.

Sababu muda wowote meza inapinduka nenda

Kama ni mwalimu wa cheti aende akale bachi na masteri uone kama watakusumbua
 
Professional teachers wanalipwa kiasi gani take home mwenye ufahamu
Inategemea elimu Yako na daraja la mshahara ulioanzia.

Na. Muda uliofanya kazi

Kwa. Mfano kama Kuna mwalimu Yuko around 50 hivi ana aliajiriwa kwa shahada ya kwanza straight from Chuo

Huyu ana basic yenye around 2.9m atakuwa kamaliza madaraja yote ya mshahara hadi TGTS I, na alianza na TGTS D.

Kama ni alianza na cheti kwa huo umri wake na amefanya kazi mda mrefu atakuwa na 1.6m TGTS G huko.

So inategemea

Pia uko upande gani serikalini Halmashauri, wizarani, taasisi za elimu huko Kuna marupurupu kibao
 
Nina Umri wa miaka 25 kazini. Kazi hii ya ualimu nimeifanya yapata miaka 17. Baada ya hapo nikaipata kazi nyingine.

Umeongea point
 
Shukurani sana mkuu
 
Hizo ni mbwembwe tu za mtoa madam japo ameandika vizuri na kwa heshima kuliko anavyoandikaga Mpwayunga kwa dharau.

Mimi ni Mtumishi wa umma NIWE muwazi na ni kweli huwezi endelea ukiwa Mtumishi bila kufisadi somewhere ila kama unaakili kazi yoyote ya umma ni nzuri kwani inakupa mdhamana sehemu yoyote pia inakupa na mtaji. Binafsi nipo mkoani ni nimeshafanya kazi mikoa mingi kidogo Kuna walimu wapo Katavi kule Mpimbwe, Mamba na Majimoto wanapiga maisha. Nimewaona walimu wengine DABAGA kule Iringa wanapiga maisha kwenye Kilimo na ufugaji pia na issue za mbao na maliasili. Kikubwa kwenye utumishi wa umma ni mentality ya kujiajiri na kufanya kazi nje ya kazi ya umma na sio kusubiria mshahara to mshahara. Kazi yoyote ni nzuri msidanganywe humu japo kujiajiri ni kuzuri zaidi japo Hadi usimame kwenye kujiajiri sio mchezo. Mungu awabariki wachakarikaji wote kwani Nia YETU ni tuwe na maisha mazuri na tuweze kuclear bills zetu za Kila siku zaidi na zaidi tuishi tukimkumbuka na kumtegemea Mungu atupaye riziki zetu za Kila siku.
 
Hongera kwa kujikomboa mwenyewe. Kiukweli kazi ya ualimu inachangamoto nyingi ambazo zinaifanya kazi hii inaonekana mbaya na hasa kutokana na watawala waliopewa dhamana kuwa watu wa kuwanyanyasa walimu, watu wa kutokutoa sitahiki za walimu kwa muda muafaka. Hayo yote yanamfanya Mwalimu aonekane mtu wa dhiki hasa zaidi katika maeneo ya vijijini ambako haki za mwalimu ukanyagwa wazi wazi.

Utashangaa malipo ya pesa za likizo yanafanywa kwa kujuana wakati ni haki kisheria unapokuwa na likizo ya malipo wanapaswa wakulipe pesa ya nauri kama inavyopendekezwa.
Lakini kwa baadhi ya halmashauri ni changamoto kweli kweli yaani mtu anaweza akapitisha hata miaka mitano au Saba hajawahi hata cku moja kulipwa pesa za nauli. Au bado tunaendelea na msemo unaosema unapotaka kula basi kubali pia kuliwa kidogo?

Kiukweli changamoto ni nyingi katika kada hii na baadhi ya changamoto zinatokana na mifumo ya kiutawala kuwa mibovu na iliyopitwa na wakati. Hii inaonekana zaidi maeneo ya vijijini. Mifumo ya maeneo haya inapaswa kutazamwa upya. Maana viongozi wanaonekana kujitengenezea mazingira ya kunufaika na mifumo hii mibovu.
 
Kujenga n kununua usafir bado unaona si kitu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…