Nina wiki mbili toka niajiriwe katika kiwanda kimoja hapa mtwara. Mimi ni msimamizi wa vibarua wa wanaofanya usafi.
Changamoto iliyopo ni kua nikiwapa maelekezo kua usafi ufanyike katika maeneo yao wanaleta dharau, jeuri, kejeli. Wanataka niwe fea ila fea sidhan kama inafaa kazini
Majibu yao ni kua walikuepo hapa zaidi yako Leo wametimuliwa, hili jambo linanipa hofu na kutojiamini. Had hapa nishagombana na watu wawili ile tu kuwapa maelekezo wananimaindi.
Uongozi wa juu nao wananiambia nijitahidi kumalizana nao nisiwe naripoti ripot kila kitu. Nimekuja hapa kuomba ushauri jinsi ya kuitatua hii kadhia. Nahisi kuchoka.
Habari,
Ni kawaida, kwasababu wewe ni “mpya” hapo kazini, wanajaribu kukupima. Hii ni kawaida,sehemu yeyote utayo kwenda,ikiwemo hata ukiamia kwenye department mpya.
Kama kiongozi, nadhani unaweza kuwa na meeting kila hasubui,kabla ya kuanza kazi.unaweza eleza vipaumbele vya siku nzima na unaweza toa kama mtu anakuwa na nyiongeza au dukuduku kuongea. Lengo ni kuwapa picha halisi ya siku na kuwapa nafasi ya kuongea kama wanao wanaonewa.
Baada ya hapo,panga kazi kwa kila mmoja, awe anajua siku hiyo anafanya kazi au usafi sehemu gani. Husiwape kama group, gawa kazi vipande vipande.
Ukifika mwisho wa siku, unaweza kugagua,na kama haijafikia viwango, unaweza kujadili na mhusika. Tengeneza kitu kama file, ku monitor “performance “. Hii itakusaidia kupeleka malalamiko yako kwa management maana utakuwa na evidence.
Husikimbilie kushitaki kila siku, management watajua “hauna” sifa ya kuwa kiongozi. Sifa moja ya kuwa kiongozi ni uwezo wa kutumia mbinu mbali mbali ikiwemo “siasa” kushawishi watu kufanya kazi. Ukiwa na mentality ya kuwa wewe ni “boss” lazima wakusikiliza, sidhani kama utapata matokeo mazuri