Kenya inaongoza uzalishaji Avocado Afrika. Tusipokuwa makini chini ya CCM kuna siku Kenya itailisha Tanzania


Unajua wakulima walichopitia baada ya wao kugoma? Gunia la mahindi kwa tshs 30,000? Acheni mentality za ushindani wa chandimu usio na faida yoyote zaidi ya hasara. Wenye busara waliona ni tatizo ndio maana wakakaa mezani. Sasa wewe naona una vielements vya kujiboast kama vile unaweza kuthrive kiuchumi bila win win situation ya kibiashara baina ya nchi jirani.
 
..Majirani wako makini kwelikweli ktk masuala ya kilimo, na wanazingatia viwango.

..angalia video hizi mbili kuna mengi ya kujifunza kuhusu namna ya kufanya kilimo.


Halafu wala hata hawabwabwaji , nyie wabongo miche yenu minne kule Njombe mnataka kupiga kelele dunia nzima !
 
À

Weka picha jamaa wakikata majani ya ng'ombe tuone.
tatizo lako unamahaba amboyo yanakufanya ubishe vitu vipo adharani panda gari nenda hai shuka kwa sadala tembelea shamba la kibohehe ujuonee mwenyewe picha za nini nchi yetu sote tumecheza chipukizi tumeimba nyimbo za kusifu chama pendwa sana hata kuliko wewe ila kama wanateleza kubalini kukosolewa na pia mjirekebishe mwekezaji alikuwa anaingiza watu 1000kwa siku kwa 5000per day unadhani zilikuwa zinapona kaya ngapi pale alikuwa ameandaa heka 1000za parachichi unadhani leo hii tungekuwa tunapata kodi shilingi ngapi kisa walishindwana mkuu wa wilaya eti kumkomoa mbowe shame on you
 
Mbona unaandika insha?
 
Hebu angalia packaging zao jinsi wanavyohifadhi mpaka JK eti akatuma watu wakajifunze namna ya package daa

Kwa kweli sisi ni zaidi ya washamba na hatuwezi fanya lolote la maana huo ndio ukweli
Jaribu kupita kariokoo tu angalia wauzaji walivyo nyuma yale maboksi yaliyoleta mizigo toka China eti ndio hayo hayo Yakiwa yamepasuliwa pasuliwa halafu ndio wanafungashia tena mizigo inayotupiwa kwenye malori na kupelekwa mikoani

Mzigo unafika maboksi yamepasuka vibaya

Tunashindwa kuongeza ubora na thamani ya vifaa kwa packaging nzuri lakini tunaona ni hasara kuweka maboksi mapya wakati wenzetu wana viwanda kwa ajili ya boxes na tape pia

Huku nilipo kuna soko kubwa linaitwa western international market matunda na mboga zinatoka UG na Kenya ila hakuna hata pilipili za Tz mnajua kwanini
Hata uhifadhi hamjui na vibali kuna mahasidi wanakuzungusha mpaka unakata tamaa

Utasema labda mama yake ndio analeta matunda Ulaya kumbe wapi hata yeye hajatoka hata nje ya nchi tangia amezaliwa

Badilikeni nyie watu
 
Kwa majirani zetu huwa wana muda mwingi wa kufanya research ndo kinachowafanya watoboe katika sekta ya kilimo.
 
Ni wapi nilipoonyesha kutojali biashara kama siyo mawazo yako kuyawasilisha yawe mawazo yangu.
Kwani hiyo "win-win" inapatikana huko pekee.

Ninajua unachopambania hapa, lakini ukweli ni kuwa ni upungufu wa akili kupapatikia soko moja ambalo kila mara ni la kuzungushana akili.
 
Imeandikwa, kondoo mmoja akipotea mchungaji mwema huweza kuwaacha wengine 99 ili kumtafuta huyo aliyepotea. Mjasiliamali halisi ni yule anayeguswa na upotevu wa hata mteja mmoja. Sasa kama wewe si mpungufu wa akili kama unavyotuita wenzio, tuletee hayo masoko mbadala yanayoishinda Kenya.
 
Wanalangua parachichi Tanzania, wanaenda kuweka label kama zimelimwa Kenya. Nenda Njombe pale wana ofisi za kununua parachichi wanapeleka Kenya. Zikifika Kenya wanasema zinalimwa Kenya
Mananasi tu sahv hapo kiwangwa wakenya kibao wamekuja kununua

Ova
 
Uko sawa ,hawa watu wanashindwa kuwa Kenya wanatembelea kwa mgongo wetu mfano,Mlima Kilimanjaro husema ni wa kwao,Mbuga ya Serengeti,kilimo cha mpunga,mahindi,parachichi,ndizi,ng'ombe,mbuzi na hata samaki.
Sawa,nyie mazao na mazagazaga mengine mnayFanyia nini
Vp serikali yenu imejaribu kuwatafutia fursa ya kwenda kuuza nje
Au ndiyo fursa wanatafutiwa wachache tu na ndomana hao hao kila leo wanakuwa mabilionea tz

Ova
 
Kamwe Kenya haiwezi kuiambia kitu Tanzania kwenye suala la kilimo. Wapinzani wetu kwa nchi zilizo karibu ni Zambia, South Africa labda na ile Zimbabwe ya zamani.
Hamna lolote,wenzenu serikali yao inawatafutia watu wao fursa za masoko ya nje
Ehe tz je,wanaofanya export ni wachache sana na hao hao kila kukicha ndy wanataka wawe mabilionea....

Ova
 
Hamna lolote,wenzenu serikali yao inawatafutia watu wao fursa za masoko ya nje
Ehe tz je,wanaofanya export ni wachache sana na hao hao kila kukicha ndy wanataka wawe mabilionea....

Ova
Wanachotuzidi ni ujanja tu wa biashara (lobby) na sio kulima.
 
Mnataka mbembelezwe kununua bidhaa huku nyinyi wenyewe mkiwa na njaa? Mwenye dhiki habembelezwi, atakuja tu mwenyewe, kama alivyokuja. Hakuna mbwembwe kwenye njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…