Kenya inaongoza uzalishaji Avocado Afrika. Tusipokuwa makini chini ya CCM kuna siku Kenya itailisha Tanzania

Hv unapata wap muda wa kumjibu hyyu nguchiro?????
 
Hamna lolote,wenzenu serikali yao inawatafutia watu wao fursa za masoko ya nje
Ehe tz je,wanaofanya export ni wachache sana na hao hao kila kukicha ndy wanataka wawe mabilionea....

Ova
Hao hao ndio wauza ngada
Yaani hawawezi kupambana bila madawa wengi wao

Avocados zinauzwa kwa bei ya kutupa zinaenda SA na Kenya halafu hizooo ulaya
 
Nchi yetu sijui Ina shida gani, na nani anaweza kuitatua, karibu Bei za mazao yote hadi Madini ni ndogo kuliko kwa majirani, ndio maana Kagera wanatorosha kahawa Kwenda Uganda, wa zenj wanatorosha karafuu Kwenda Kenya, parachichi zinapelekwa kwanza Kenya ndio ziuzwe kimataifa, dhahabu , Tanzanite zinatoroshewa Kenya.

Kwa Nini majirani hawatoroshi bidhaa zao kuleta TZ? Ni sababu sisi ndio tuna bei za karibu na bure. Kwenye Kipindi Cha DW mkenya mmoja anahojiwa anadai mti mmoja wa AVocadro unamsomesha mtoto shule ya private kwa mwaka, TZ hata uwe na acre huwezi.
 
Hiyo ndio diplomasia ya DK.Samia Sasa.
 
Hiyo ndio diplomasia ya DK.Samia Sasa.

..ndio tatizo letu Watanzania.

..tunaabudu wanasiasa na Raisi kupita kiasi.

..Kenya kwenye mambo yao ya biashara, kilimo, ufugaji, utalii, huwezi kuwasikia wanamtaja-taja na kumtukuza Raisi wao.

..Kwa hapa Tanzania, mfanyabiashara, au mkulima, akizungumza sentensi tatu, moja atamtukuza raisi au mwanasiasa.

..Tubadilike KIFIKRA.
 
Hawana namna lazima wamtaje Rais.

Matunda ya diplomasia

 
Hawana namna lazima wamtaje Rais.

Matunda ya diplomasia


..mbona Kenya hawamtukuzi Raisi wao kama tunavyofanya Tanzania?

..mpaka Kenya wanauza avocado China unadhani hakukuwa na juhudi za kidiplomasia?

..Ni suala la kujiamini na kujitambua. Watanzania tunapaswa kubadilika KIFIKRA.

..Naomba usinitoe kwenye mada.
 
Walishamtukuza walipopata hiyo fursa,uwe unafuatilia hotuba za ma hasla basi
 
Wakuu tujaribu kuangalia mambo haya mawili.

1.Kwa nini ni rahisi kupitishia avos bandari ya Mombasa kuliko dar, yaani mzigo unatoka Mbeya, badala ya kupitia Dar port, wafanya biashara wanaona rahisi kupitishia Mombasa sababu ya miundombinu na urasimu pale bandarini. Sasa data zote za export za matunda zitakuwa zinasoma kama origin ni Kenya kumbe avos zingine zimetoka Songea. Vivyo hivyo kwenye airport zetu.

2. post harvest storage, hatuna kabisa hii huduma na hivyo mzigo wetu mwingi hupotea kabla ya safari, wenzetu wana huduma hii na hivyo kuongeza quantity ya final product sokoni.
 
..Majirani wako makini kwelikweli ktk masuala ya kilimo, na wanazingatia viwango.

..angalia video hizi mbili kuna mengi ya kujifunza kuhusu namna ya kufanya kilimo.


Sisi ni kuwasha mwenge kulikotutoa akili au kitu gani? Mbona hatuna focus na chochote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…