Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaonekana upo horny.... unatafuta kijogoo....Sasa kwa nini unajitungia tu?
Anayelima avocado ni individuals au ccm?NAWAKUBALI SANA KENYA KWENYE SUALA LA SERA YA KILIMO NA ARDHI, HAPA KWETU MTU ANAWEZA AMKA ASUBUHI NA MGOGORO KICHWANI KWAKE NA AKAKUNYANG`ANYA SHAMBA HIVIHIVI NA BADO SHAMBA HILO LIKABAKI BILA UZALISHAJI.
Unapenda sana kubwabwaja wewe🤣Hata nikiweka ushaidi inasaidia nini
Wakati NCHI YENYEWE ishauzwa
Bado tuwekwe BONDI tu sisi
Mana rasilimali zote ZINAONDOKA huko kia na ANTONOV
Not so fast.deo hizi mbili kuna mengi ya kujifunza kuhusu namna ya kufanya kilimo.
Hebu binuka nikubamize.Unaonekana upo horny.... unatafuta kijogoo....
Not so fast.
Siwezi kuwatetea CCM hata kidogo, lakini hapo hapo sikubaliani nawe kuhusu kujifunza kilimo huko..
Unajua Kakuzi ni ya nani, na imekuwepo hapo tangu lini?
Hayo ni matokeo ya makubaliano aliyolazimishwa kuyafanya Kenyatta wakati akiwa mfungwa, kwa masharti ya kuachiwa na kupewa uongozi wa nchi hiyo.
Mwalimu Nyerere asingekubali masharti hayo.
'Biggest Exporter', elewa humo humo yamo na ya Tanzania kwa hisani ya CCM ya leo.
Naona mambo ya Kenya yanakupofusha akili sana. Sijui ni sababu ya lugha ya Kiingereza, au vipi?
Kiswahili chetu ni lugha adhimu sana.
Not so fast.
Siwezi kuwatetea CCM hata kidogo, lakini hapo hapo sikubaliani nawe kuhusu kujifunza kilimo huko..
Unajua Kakuzi ni ya nani, na imekuwepo hapo tangu lini?
Hayo ni matokeo ya makubaliano aliyolazimishwa kuyafanya Kenyatta wakati akiwa mfungwa, kwa masharti ya kuachiwa na kupewa uongozi wa nchi hiyo.
Mwalimu Nyerere asingekubali masharti hayo.
'Biggest Exporter', elewa humo humo yamo na ya Tanzania kwa hisani ya CCM ya leo.
Naona mambo ya Kenya yanakupofusha akili sana. Sijui ni sababu ya lugha ya Kiingereza, au vipi?
Kiswahili chetu ni lugha adhimu sana.
Sijasema Uhuru Kenyatta; na sikumbuki huyu kuwahi kuwa gerezani...tuko hapa kuelimishana.
..naamini wasomaji na wachangiaji watapenda kusikia toka kwako kuhusu Kakuzi.
..tueleze mahusiano yake na Uhuru Kenyatta na masharti unayosema aliwekewa.
..hili ni jukwaa huru, karibu.
..naona Kakuzi imekuletea ukakasi kidogo.
..msikilize muwasilishaji wa karakuta farm.
..kuna mambo mazuri ambayo Watanzania tunaweza kuyaiga.
Sijasema Uhuru Kenyatta; na sikumbuki huyu kuwahi kuwa gerezani.
Kakuzi ni Kampuni ya Kiingereza ambayo imekuwepo Kenya tokea ukoloni, ni mabaki ya 'settlers'.
Hawa ma'settlers' waliwekewa kinga na serikali ya Uingereza (nyumbani kwao) wasinyang'anywe ardhi waliyokuwa wamehodhi; kwa hiyo hapakuwa na ardhi ya kuwapa waafrika (squaters) baada ya uhuru kupatikana.
Na hata pesa iliyokuwa imetolewa kwa ajili ya kununua mashamba ya 'settlers' waliokuwa wamekubali kuuza ardhi, badala ya kununua ardhi hiyo na kuwagawia waafrika ambao hawakuwa na kitu, viongozi wachache (kama akina Kenyatta, Moi, na wengine wakagawiana kinyemela.
Kakuzi ni masalia ya 'settlers', kama walivyo wenye mashamba ya chai na maua.
Tanzania akina Lonro tuliwakataa.
Sijasema hakuna mazuri tunayoweza kuyatumia hapa, hata kama ni kwa kuyabadili kidogo kulingana na hali yetu ilivyo. Si lazima kubeba tu.
Na hapo hapo pia elewa kuwa kuna mazuri yanayofanyika hapa pia, pamoja na ubovu wa CCM yetu.
Vinginevyo tusingeweza kuwauzia mazao yanayopatikana hapa.
Mnaopenda kusifia Sifia Kenya si mhamia huko huko tu mkawe Raia ya Kenya
Kwann mteseke Tanzania ambako kilimo ni tia maji tia maji
Kama Kenya Wana sera nzuri ya kilimo kwann basi msiende huko kuwekeza mjikwamue kiuchumi kuliko kulia lia hapa.
It is too much bored
Yule Jamaa aliyewahi kuwa waziri wa Kilimo (Mkikuyu, nadhani toka Nyeri, jina limenitoka,Kinyanjui), kabla ya yule Mmeru ambaye kamaliza juzi juzi Munya), alifanya kampeni kubwa sana ya kugawa miche ya parachichi huko Central wakati wa uongozi wake. Ukiacha upendeleo wa eneo moja, kama ilivyo kawaida ya huko, kazi hiyo ilikuwa ni kazi nzuri sana ya kuwasaidia wakulima wadogo wadogo...samahani nilikuelewa vibaya, nilidhani umemaanisha Uhuru, kumbe wewe umemaanisha Jomo Kenyatta.
..maelezo yako ni kwamba Kakuzi ina makandokando ya ukoloni au unyonyaji wa mtu mweupe dhidi ya Muafrika wa Kenya.
..ukiondoa hayo makandokando ya kihistoria, je, ni mambo gani mazuri tunaweza kuyaiga ili kuboresha sekta ya Parachichi hapa Tanzania?
Na ninakuhakikishia, Kenya wanayo hofu kubwa sana, siku moja tukipata uongozi wenye dira sahihi. Wanajua majivuno yao ya kuwa kinara katika eneo hili yatafikia kikomo..kaka Ccm inatuchelewesha.
..inatufanya tuwe wasindikizaji wakati tunaweza kuwa viongozi.
Na ninakuhakikishia, Kenya wanayo hofu kubwa sana, siku moja tukipata uongozi wenye dira sahihi. Wanajua majivuno yao ya kuwa kinara katika eneo hili yatafikia kikomo
Hapana...huo uongozi tutaupata lini, kama tumeshindwa kuupata miaka zaidi ya 60 toka tupate uhuru?
..Wakenya kuwa na hofu ndio inawasaidia kujiongeza, sisi tumebweteka na Ccm yetu.