Kero: Msafara wa Rais umekuwa mateso kwa watumiaji wa barabara

Kero: Msafara wa Rais umekuwa mateso kwa watumiaji wa barabara

Utakuta anaenda kuzindua kitu kingezinduliwa hata na mkuu wa wilaya
Kwa haraka haraka nimehesabu hizo shangingi zinafika 25 to 30 na sio mia kama ulivyosema.. Na sio zote ni escort za rais nyingine hapo ni za mkuu wa mkoa mkuu wa wilaya, mabalozi na pengine waziri pia... Tusipende kupotosha vitu ovyo ovyo tu.. Huyo ni mkuu wa nchi ulitaka apite na baiskeli ovyo wewe..
 
Ni haki nchi maskini kama Tanzania Msafara wa Rais Kuwa namagari zaidi ya Mia na helkopta mbili angani tutaona matokeo chana kwenye mandishi tu
Magufuli anahitaji ulinzi mkali,anawapiga sana nyundo mafisadi.Hata hivyo nadhani sio wajibu wako kujua kiasi cha ulinzi Rais anachohitaji,kazi hiyo waachie wazee wa kitengo
 
Gari moja ni sawa na shule moja ya Kisasa ya sekondari kama ukishirikisha nguvu za wananchi,
Gharama halisi ni mafuta+posho. Hayo magari hayakununuliwa kwa ajili za ziara pekee
 
Leo kati ya saa mbili kasoro hadi saa 5 kasoro, barabara kutoka stendi kuu ya mabasi Morogoro kuelekea Dodoma ulifungwa kwa masaa matatu kupisha msafara wa Mhe. Rais. Masaa matatu kusimamisha mabasi ya abiri na binafsi ni mengi sana. Naomba watu wa msafara wa viongozi na polisi walitafutie ufumbuzi hiii kero. Tumezoea kusimamishwa kupisha msafara wa viongozi dakika 30 hadi 45 hii ya saa 3 ni muda mrefu sana. Na kama kasimamishwa ghafla na wananchi ni busara wakaruhusu magari yakaendelea na safari kwanza na pale anapomaliza kuongea na wananchi magari yakazuiwa tena.
 
Leo kawa amiri jeshi mkuu, nimemuona amevalia kijeshi kama kawaida katoa na sadaka kwa mwananchi,.
 
Eti kwa sababu ya kutaka sifa kuwa anatumia usafiri wa barabara ndio atese Watanzania wengine ambao pia wanahitaji barabara kwa kufanya shughuli zao!!! Hii haikubaliki kabisa!

Halafu sio kweli kwamba kutumia magari anaokoa pesa....Usikute ndio anazidisha gharama kuliko angetumia usafiri wa anga.
Duh!!

Ni wewe au nimekufananisha?!
 
huu ugawaji wa fedha ovyo mitaani sio jambo zuri lakini inatubidi tuvumilie tu.Rais wetu anashusha hadhi ya pesa bila kujua,Anawafedheesha watanzania bila kujua,anachezea fedha za umma bila kujua,anatuonesha kua sio muhimu watu kulipa kodi pale wanapogain hivyo kushusha ari ya kulipa kodi as you Earn bila kujua.Tubaki kuvumilia na tuombe Mungu tusipate tena kiongozi wa aina hii huko mbeleni.Fedha ni nembo na respectable commodity haipaswi kutolewa tolewa tu na kiongozi wa juu kabisa angalua wangekua ni wasaniii au wahuni wa mtaani tungesema ni matunuzi.Ingekuwa busara Rais awe na bahasha kuliko kuhesabu fedha hadharani na kutoa hadharani tena akiwa juu ya gari.siku akiwa kwenye helicopter anaweza kuzirusha masikini wanyang'anyane chini huku.Haipendezi kuwafedheesha watanzania kiasi hiki.
 
Kama leo katuchelewesha sana tunaoingia ofisini kwa kusign timesheet..... Kama anasafari zake awe anaanza at least saa nne asubuhi ili kupunguza kero
 
Munjombe,
Mkuu wa nchi ni mfalme na hela ya nchi ni mali yake kwa niaba ya serikali kama taasisi vilevile kwa niaba ya wananchi. Hizo hela hazigawiwi kiholela ni pale tu anapoguswa na changamoto zinazomkabili mwananchi binafsi au jamii fulani kujenga miundombinu ya kijamii. Mahali pengine uanzisha mchango kwa viongozi anaoambatana nao kuchangia na mwisho wa siku hiyo kero uisha badala ya kupita tu na kuacha ahadi hewa zitakazochukua miaka kutekelezwa yeye anazitekeleza hapo hapo. Kwavile hiyo hela inatolewa kwa uwazi idara ya uhasibu inaiandikia maelezo na kumbukumbu kuwekwa kwa ajili ya uhakiki. Kumbuka hizi hela zinatolewa kwa ajili ya kutatua changamoto zinazokumba either mtu binafsi au jamii ambao wote ni watanzania na Rais ni baba yetu ukubali au ukatae. Bora anawapa watanzania, wengine wanaiba na kuzitoroshea mabenki ya nje. Rais wetu hajawai kutoka nje ya Africa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya taifa mwenye macho anaona. Naomba tumuache Rais wetu aendelee kufanya kile ambacho anaona ni chema. Mungu mbariki Rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli
 
Nina mashaka na ushindi wa urais wa mzee meko.
Kama umechaguliwa na wananchi ulinzi wote wa nn??

Wizi wa kura umemfanya mzee meko awe na PARANOIA muda wote!
Weeewee! JPM alishinda kihalali. Ulinzi nilazima kwa mkuu wa nchi kuna maadui wa ndani na nje! Hata ukishinda 100% adui mmoja tu mwenye siraha anaweza kukuondoa!
 
Munjombe,
Mkuu wa nchi ni mfalme na hela ya nchi ni mali yake kwa niaba ya serikali kama taasisi vilevile kwa niaba ya wananchi. Hizo hela hazigawiwi kiholela ni pale tu anapoguswa na changamoto zinazomkabili mwananchi binafsi au jamii fulani kujenga miundombinu ya kijamii. Mahali pengine uanzisha mchango kwa viongozi anaoambatana nao kuchangia na mwisho wa siku hiyo kero uisha badala ya kupita tu na kuacha ahadi hewa zitakazochukua miaka kutekelezwa yeye anazitekeleza hapo hapo. Kwavile hiyo hela inatolewa kwa uwazi idara ya uhasibu inaiandikia maelezo na kumbukumbu kuwekwa kwa ajili ya uhakiki. Kumbuka hizi hela zinatolewa kwa ajili ya kutatua changamoto zinazokumba either mtu binafsi au jamii ambao wote ni watanzania na Rais ni baba yetu ukubali au ukatae. Bora anawapa watanzania, wengine wanaiba na kuzitoroshea mabenki ya nje. Rais wetu hajawai kutoka nje ya Africa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya taifa mwenye macho anaona. Naomba tumuache Rais wetu aendelee kufanya kile ambacho anaona ni chema. Mungu mbariki Rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Zaidi ya ushamba tuu! Duniani kote pesa za serikali zinautaratibu wake jinsi ya kuzikusanya na jinsi ya kuzitumia.
Kuvunja utaratibu sio jambo la sifa
 
Ni kawaida kwa viongozi wetu kuwa na misafara mikubwa na yenye mbwembwe kibao, lakini kwa mtukufu rais wangu wa awamu hii umekuwa kero na mateso kwa watumiaji wa barabara kwa kuzingatia kwamba mara nyingi anasafiri kwa barabara, hali imekuwa mbaya na mateso ya hali ya juu.

Leo wakati naelekea Mpwapwa tumekwamishwa kwa zaidi ya saa moja kwenye kituo cha mafuta jirani na kituo kikuu cha mabasi Morogoro, kwa kweli nashauri wahusika wabuni njia mbadala ya kumsafirisha rais wangu.

Sijui ni ushamba na ulimbukeni wa kisukuma au nini, yaani this is unexplainable nuisance. Hivi anajua mateso tunayoyapata kweli,kama anajua he is inhumane and totally uncivilized
 
Back
Top Bottom