Cesar Saint
JF-Expert Member
- Nov 18, 2016
- 423
- 726
Na askar itakuwa wanapokea mgao make wanawadekeza sana
Hii njia yote ya Mandela Road ni madambwe ya watu wa vitambaa cheupe lile la Uhasibu ni la Malori na daladala zaidi .
Hapa Taifa wanacheza na gari ndogo zaidi ukifika pale Serengeti machinjioni huwa hawakai sana mara moja moja utawakuta hapa kona ya makaburini sogea mbele pale sokota ni malori na wavuka taa nyekundu ukifika Veterinary pale ni mchanganyiko na wanakaa mara moja moja ila Tanzara ni mchanganyiko Bodaboda gari ndogo na hata malori daladala hawanaga mpangonazo ukifika buguruni pale na kwenyewe kwenye kona ya sheli wapo wadau pale hapa mbele kwenye U turn kabla ya daraja kuna wadau pia wanakamata malori na chochote watakachotaka kisha kuna hapa tabata sheli pale jamaa wanakamata mpaka Toyo na makila kitu.
Kisha unafuata mwananchi pale na kwenyewe utakutana na wadau ukiwa na mzigo tu unapigwa mkono kama tabata sheli tu tena wanamtindo wanaingiza namba ya gari ikiwa kwenye taa kuangalia kama inadeni.
Ukivuka hapo unakutana na wadau pale TMDA na external hawa wanakamata zaidi transit international na malori au gari ya mizigo.
Njia pekee ya kuepuka foleni na usumbufu wa jamaa wa kitambaa cheupe wewe nenda kazini early morning yaani saa kumi na mbili uko barabarani na rudi zako late kuanzia saa tatu na nusu au saa nne usiku