Kero ya kusota vituo vya mwendokasi muda mrefu

Kero ya kusota vituo vya mwendokasi muda mrefu

Head prefect

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
225
Reaction score
106
Wakuu Salaam.

Sijui kama watu wengine wanakerwa na huu utaratibu. Kumekuwa na utaratibu abiria wanakaa sana vituo vya mwendokasi haswa Gerezani, Msimbazi B na Msimbazi A huku mabasi yamepaki Gerezani kule madereva wanapiga hadithi.

Ni nini maana ya kuita Rapid Transfer ikiwa abiria anakaa dakika 30 mpaka 45 kituoni? Na yakifika mnagombania na kubanana sana kwa sababu mmelundikwa kituoni abiria mmejaa mnagombania kama daladala za Mbagala zamani.

Hawa wanaosimamia utaratibu wa mabasi kutoka gerezani utaratibu wao ukoje?

Mathalani hizi ruti za mwenge, basi linakuwa limepaki, dereva yupo, mnakaa mpaka mnalalamika mnaambiwa tu dereva anakuja. Kumbe mwenyewe amekaa hapohapo mnapolalamikia anapiga hadithi. Baadae mnaona huyo anainuka kuwasha gari.

Abiria wengi huishia kuchukia na kulalamika kimyakimya. Wahusika ni kina nani wanaoratibu utaratibu wa haya mabasi kutoka? Imekuwa kero mno.

Mamlaka husika iweke kitengo cha huduma kwa wateja kuripoti hizi kero pale inapokuwa too much.

Nawasilisha.
 
Ni tajie project yoyote serikali ya Tz imefanikisha angalau kwa 70%?
 
Kuna ruti ya Kimara - Kibaha, gari zinachelewa Sana halafu ukataji wa tiketi sehemu nyingi lazima uvuke upande wa pili na Kisha uvuke Tena kwenda kusubiri gari.

Vigari wanavyopeleka kule ni vidogo Sana, abiria wanarundikwa hadi milango inagoma kufunga. Madereva wengi Wana viburi hata ilitokea kafungua mlango vibaya ukamgonga mtu,wakiulizwa wanajibu vibaya na kwa kukashifu abiria. Kuna abiria alibeba kuku kwenye mfuko siku moja walimkatalia kupanda.
 
Kuna ruti ya Kimara - Kibaha,gari zinachelewa Sana halafu ukataji wa tiketi sehemu nyingi lazima uvuke upande wa pili na Kisha uvuke Tena kwenda kusubiri gari.Vigari wanavyopeleka kule ni vidogo Sana...
Kuweni wastaarabu na nyie utabebaje kuku kwenye mwendokasi
 
Hili tatizo ni kubwa sana wakati mwingine unakuta madereva wamepaki tu magari wanapiga story chini wala hawana habari na mengine yanapita matupu kabisa na kuacha abiria.
 
Nchi yetu ina tatizo kubwa la usimamizi
 
Back
Top Bottom