Head prefect
JF-Expert Member
- Apr 16, 2013
- 225
- 106
Wakuu Salaam.
Sijui kama watu wengine wanakerwa na huu utaratibu. Kumekuwa na utaratibu abiria wanakaa sana vituo vya mwendokasi haswa Gerezani, Msimbazi B na Msimbazi A huku mabasi yamepaki Gerezani kule madereva wanapiga hadithi.
Ni nini maana ya kuita Rapid Transfer ikiwa abiria anakaa dakika 30 mpaka 45 kituoni? Na yakifika mnagombania na kubanana sana kwa sababu mmelundikwa kituoni abiria mmejaa mnagombania kama daladala za Mbagala zamani.
Hawa wanaosimamia utaratibu wa mabasi kutoka gerezani utaratibu wao ukoje?
Mathalani hizi ruti za mwenge, basi linakuwa limepaki, dereva yupo, mnakaa mpaka mnalalamika mnaambiwa tu dereva anakuja. Kumbe mwenyewe amekaa hapohapo mnapolalamikia anapiga hadithi. Baadae mnaona huyo anainuka kuwasha gari.
Abiria wengi huishia kuchukia na kulalamika kimyakimya. Wahusika ni kina nani wanaoratibu utaratibu wa haya mabasi kutoka? Imekuwa kero mno.
Mamlaka husika iweke kitengo cha huduma kwa wateja kuripoti hizi kero pale inapokuwa too much.
Nawasilisha.