Kesho Mwanza CHADEMA itaifunika CCM sherehe za uhuru. Wakuu wa chama kuhudhuria

Kesho Mwanza CHADEMA itaifunika CCM sherehe za uhuru. Wakuu wa chama kuhudhuria

Naipenda sana hii. Halafu watu wasiojua maana ya hii watapinga.
Nataman wanachama wote wa cdm waende kwa wingi wakaonyeshe kabisaa kuwa bado wapo na hawaterereki kwa lolote lile
 
Mkuu, kusherekea uhuru wa Taifa lako sio usaliti. Siasa sio ugomvi.
Nimesikitishwa Jana kuona kamati kuu ya chadema ikitamka kwa kinywa kipana kwamba kesho 9/12/2019 mwenyekiti mbowe ataongoza ujumbe wa viongozi kusherehekea uhuru wa tanganyika ccm kirumba mwanza mbele ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania! Hivi kweli mbowe umesahau mwezi uliopita ulitangaza kususia uchaguzi wa serikali ya mitaa/vijiji ukisema serikali ya ccm imewaengua wagombea na kuwanyima haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa je leo nini kimebadilika? Mikutano ya kisiasa imefungiwa kwa miaka 4 kinyume cha katiba ya nchi bado huoni unasema unaenda kwenye uhuru!! Tukisema wamekufika bei kama ulivyokua unawatuhumu kina mrema utabisha?..ivi unakwama wapi ndg au kesi zimekufanya uchanganyikiwe sasa unatafuta huruma ya watawala kuomba poo! Bila kujali ni wanachama wangapi wameumia kwaajiri ya kutetea misimamo ya chama ulioitoa..usipobadilika utaongoza chama kikiwa dhaifu sana maana unataka kuwa mwenyekiti mwenye ndimi 3 nilizani umejifunza makosa ya 2015 ya kusomba mafuriko hewa.
 
Uhuru wa nchi ipi?mchonga meno mzee wa riwaya aliwaona wazee wetu mafala sana
 
Nasema hivi, njoo na verified user Kisha uweke hiyo elimu na tuone ulicho achieve, Ni kipi so far umelifanyia taifa hili. Nipo kwenye mitandao muda wote maana simu yangu ninayo mkononi muda wote, naweza kupiga simu, kujibu sms nk. Kuwepo mitandaoni sio kama kwenda
kanisani useme unazima simu. Niko huru maana nimejiajiri na kutoa ajira kwa wengine, mimi sio mtumwa wa kazi za wanaume wengine kama ww. Kwakuwa ww umeajiriwa na wanaume wenzio unapaswa kuripoti kwenye hiyo ajira kuanzia asubuhi mpaka jioni, kinyume na hapo ukifukuzwa kazi ukija mtaani lazima uolewe.
Mkuu Tindo,
Umemjibu vema sana huyu kilaza wa Lumumba street! Mwambie Mombasa kuna ajira za madumejike yenye IQ kama zake…!
 
Basi tuwe na Chama kimoja SIMPLE
Haiwezekani, kwa kuwa tutakuwa tunaivunja Katiba ya nchi.. ......

Kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) inatamka hivi nikinukuu " Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakuwa na mfumo wa kidemokrasia na ya vyama vingi" mwisho wa kunukuu
 
Kama kuna karata CDM mmejua kucheza ni hii, Leo Dunia itashuhudia unafiki wa mtu .
Kwa kuwa najua kuwa wale makada wa CCM watawaelekeza mapolisi "wao" wawashughulikie hao wapinzani wao wa Chadema, na kwa kuwa sherehe hizo zitapata "coverage" ya vyombo vya habari vya dunia, hapo ndipo tutakapobaini kuwa kumbe Jiwe ni mnafiki no. 1 nchini!
 
Mkuu una hoja za kipuuzi sana.Mimi sio msukuma lkn huwa siangaiki na anapoongea kisukuma. Anaongea kisukuma kutokana na hadhira iliyopo na sijawahi msikia mnananchi wa kawaida akitoa povu zaidi ya bavicha wa kwenye media
Magufuli viwango vyake havitoshi kabisa ni grade ya chini unaongeaje ki lugha wakati inajulikana lugha ya taifa ni Kiswahili
 
Haiwezekani, kwa kuwa tutakuwa tunaivunja Katiba ya nchi.. ......

Kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) inatamka hivi nikinukuu " Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakuwa na mfumo wa kidemokrasia na ya vyama vingi" mwisho wa kunukuu

cc: John Joseph Pombe Magufuli!
 
Kamati kuu ya Chadema kwa kauli moja imeazimia kushiriki katika sherehe za Uhuru zitakazofanyika Mwanza kitaifa.

View attachment 1284723
Kosa kubwa la kwanza kwa CDM ilikuwa kumpokea Lowassa. Mwisho wake tumeuona.

Kosa la pili ni hili la kuhudhuria sherehe za Uhuru zikiongozwa na mtu aliyeapa kuwaangamiza kwa njia zozote zile.

Sikutegenea hili baada ya umafia waliofanyiwa kwenye uchaguzi uliogeuka uchaguzi. Na kesho wataamkia mahakamani kwenye kesi za kubambikwa.

Uongozi CDM ujitafakari.
 
Back
Top Bottom