Kesi imesikilizwa tunasubiri hukumu. Mawakili wa Lissu wanafuata nini gerezani, kuna siri gani hawataki isikike?

Hana mawakili kwenye kesi yake. Sijasema kwanini hakuwa na mawakili.

Mwandishi anaposema mawikili wa Lissu wamekwenda kumuona Lissu sio kweli, ni uchochezi. Kwanza walikwenda kufanya nini wakati Lissu anasubiri hukumu yake itakuwaje. Kwanini hawataki mazungumzo yao yasisikilizwe na askari magereza?

Sheria hairuhusu Askari au mtu mwingine kusikia mazungumzo ya mtuhumiwa na mawakili/wageni wake

Vitu vingine Kama hamvijui muwe mnauliza kuepuka aibu Kama hizi mnazoonyesha hapa
 
Moja ya kanuni kubwa sana katika sheria, katiba na haki za binadamu ni usawa wa watu wote mbele ya sheria, katiba na haki za binadamu.

Kwa msingi huo, kwenye suala la haki za kisheria, kikatiba na kibinadamu, hakuna hoja ya "hii ni kesi kubwa".

Hiyo hoja inaonesha ujinga wako.

Unajipa kazi kumwelewesha chizi
 
Ukiweka chuki zako pembeni ukatumia walau 1% ya akili yako ndogo utagundua kwamba Lissu Ana kesi nyingine kisutu na Ana haki ya kuwasiliana na mawakili wake kwa mujibu wa sheria

Kwani hao bwana zako wanaogopa Nini mtuhumiwa kuwasiliana na mawakili wake?
Gentleman,
mtuhumiwa wa uhani ambae shauri lake tayari limesikilizwa mwanzo mwisho,
na anaesubiri hukumu tu, hana nafasi wala fursa ya kuonana hata na mke wake tu, sembuse hao mawakili alio wakana kabla? Kuonana na wakili au mkewe ni hadi baada ya hukumu, na iko hivyo kitaifa na kimataifa.

Nenda kawaambie na wafuata mkumbo wenzako kuhusu jambo hili muhimu na itapendeza zaidi :NoGodNo:
 
Umaalumu wa kesi. Hii ni kesi kubwa kuliko kesi zote nchini, inahusu tukio kubwa sana lililogharim miundombini, mali za serikali na binafsi na vifo. Imeundiwa tume mbili mpaka sasa. Iko mahakamani inasubiri hukumu ya kuachiwa, kifo au nyingineyo. Kesi ya hivyo huwezi kupeleka makongoro yako gerezani kama unavyokwenda kumuona mtuhumiwa wa wizi wa bata na matango gengeni.

Kuna sheria inayodadavua huu mchanganuo wako hapa au ni mihemko yako tu ya kisiasa inakuwasha
 
nchi huru kama tanganyika yenye uongozi thabiti wenye kufuata uongozi bora wa sheria inakuaje inamkatalia mtuhumiwa anayesubiri hukumu kutembelewa na watanganyika wenziwe?
 
Gentleman,
mtuhumiwa wa uhani ambae shauri lake tayari limesikilizwa mwanzo mwisho,
na anaesubiri hukumu tu, hana nafasi wala fursa ya kuonana hata na mke wake tu, sembuse hao mawakili alio wakana kabla? Kuonana na wakili au mkewe ni hadi baada ya hukumu, na iko hivyo kitaifa na kimataifa.

Nenda kawaambie na wafuata mkumbo wenzako kuhusu jambo hili muhimu na itapendeza zaidi :NoGodNo:
acha kudanganya watu gentromeni,,,
sheria haina mihemuko wala uchawa:

Kanuni ya 12 ya Prisons (Prison Management) Regulations, 1968
inaweka utaratibu wa ziara kwa wafungwa.
Kwa mtu ambaye bado hajahukumiwa, kanuni hiyo inasema anaweza kuruhusiwa kuonwa kwa ziada kufuatana na msimamizi wa gereza akiona inafaa regardless kosa analotuhumiwa.....
kwahiyo gentromeni hamna katazo la moja kwa moja kama wewe unavyowa-seti misukule..
 
Hakuna sheria inayomzuia mtuhumiwa kuonana na mawakili wake acha blaa blaa

Jitahidi Sana kudhibiti hisia zako za chuki ili uone Mambo kihalisia

Kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa mwili
 
Unajipa kazi kumwelewesha chizi
Ninachoandika si kwa huyu chizi tu.

Kuna watu anawapotosha, ambao nisipomjibu, wanaweza kumuamini.

Kwa watu hao, ambao pengine hawajui mambo mengi na wanaweza kupotoshwa na chizi huyu, jibu langu linaweza kuwa la muhimu sana katika kuchambua mchele na chuya, ukweli na uongo, uninga na werevu.
 
CHadema wanajaribu kila kitu ili kupata la kulalamikia na wakumlalamikia.

Huu ni muda wa kusubiri hukumu kutoka kwa majaji waliosikiliza kesi ya Lissu. Inakuwaje mawakili wafunge safari kwenda kumuona Lissu kabla ya hukumu kutoka? Si wangojee huku itolewe kwanza ili waende wakiwa na kitu kamili cha kufanya kwa mteja wao?

Kwanza Lissu alikuwa anajitetea mwenyewe mahakamani kwenye kesi yake, hawa ni akina nani? Kuna usiri gani wanataka katika kuzungumza na Lissu hadi Lissu agome kula n kumeza dawa?

View: https://www.youtube.com/live/z1YRvjCEndU?si=7O5bui6DOqEfjkTw

Wewe lazimà utakuwa kavulata kaafumbili tena na kumi!
 
Hakuna sheria inayomzuia mtuhumiwa kuonana na mawakili wake acha blaa blaa

Jitahidi Sana kudhibiti hisia zako za chuki ili uone Mambo kihalisia

Kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa mwili
Gentleman,
jipige kifua kadiri uwezavyo,
but chukua hii kwa mujibu wa sheria kwamba,
hakuna raia anaweza kuruhusiwa kua na faragha yoyote ile na mtuhumiwa huyo wa uhaini anaesubiri hukumu, bila kuwepo afisa usalama wa magereza kati yao.

Mtuhumiwa wa uhaini anaesubiri hukumu, anapaswa kua katika hali ulinzi mkali katika kila eneo ili hatimae afike akiwa salama na mzima wa afya ya mwili na roho siku ya hukumu yake.Full Stop. :1Head:
 
acha kudanganya watu gentromeni,,,
sheria haina mihemuko wala uchawa:

Kanuni ya 12 ya Prisons (Prison Management) Regulations, 1968
inaweka utaratibu wa ziara kwa wafungwa.
Kwa mtu ambaye bado hajahukumiwa, kanuni hiyo inasema anaweza kuruhusiwa kuonwa kwa ziada kufuatana na msimamizi wa gereza akiona inafaa regardless kosa analotuhumiwa.....
kwahiyo gentromeni hamna katazo la moja kwa moja kama wewe unavyowa-seti misukule..
sio kwa mtuhumiwa wa uhani gentleman,
na ndio maana hata sell yake ni tofauti na wahalifu wengine. :1Head:
 
gentromeni sheria itapindishwa ila yenyewe haipindi,,
huyo msusia uchaguzi angekatazwa kuonwa kwenye Kanuni ya 12(4) inayohusu mfungwa/mahabusu ambaye amewekewa adhabu ya kufungiwa katika seli tofauti akiwa tayari ndani..

ingekuwa hivyo usemavyo basi Oktoba 16, 2026 asingeshinda kesi kupitia Kanuni ya 13..

twende kwa vipengele vya kanuni gentromeni, hapo kwenye sheria hakuna ubabaifu..
 
Gentleman,
jipige kifua kadiri uwezavyo,
but chukua hii kwa mujibu wa sheria kwamba,
hakuna raia anaweza kuruhusiwa kua na faragha yoyote ile na mtuhumiwa huyo wa uhaini anaesubiri hukumu, bila kuwepo afisa usalama wa magereza kati yao.

Mtuhumiwa wa uhaini anaesubiri hukumu, anapaswa kua katika hali ulinzi mkali katika kila eneo ili hatimae afike akiwa salama na mzima wa afya ya mwili na roho siku ya hukumu yake.Full Stop. :1Head:
Gentromeni,
nakushauri endelea na praise and worship zile za kuwapanga misukule ila huku ni vipengele ndo vinaongea,,,

Kanuni ya 13 ya Uendeshaji wa Magereza ya Mwaka 1968 inaruhusu askari magereza kuwa eneo ambalo wanaweza kumuona tu mfungwa/mahabusu na mawakili wake kwa ajili ya usalama, lakini wanapaswa kukaa umbali ambao hawezi kuwasikia wanachozungumza.

Gentromeni hizi siyo zama za zidumu fikra za mwenyekiti,,
 
mtuhumiwa wa uhaini ambae anasubiria hukumu hakua na wakili na alijitetea mwenyewe. Drama gerezani haziwezi kumsaidia, in fact ni hot air.

na kwakua tuhuma zinazomkabili ni nzito na zenye kuhatarisha umoja, amani na usalama wa taifa, mtuhumiwa huyo anaesubiri hukumu, anafaa kukaa upweke akisubiri hukumu pekee na sio kuruhusu kufanya porojo na mawakili ambao aliwakataa tangu mwanzo tena kwa dharau kubwa sana.

Magereza wasije kuruhusu madai useless ya huyo kibaraka mropokaji kwa namna yoyote ile 🐒
 
Moja ya kanuni kubwa sana katika sheria, katiba na haki za binadamu ni usawa wa watu wote mbele ya sheria, katiba na haki za binadamu.

Kwa msingi huo, kwenye suala la haki za kisheria, kikatiba na kibinadamu, hakuna hoja ya "hii ni kesi kubwa".

Hiyo hoja inaonesha ujinga wako.
Katiba na sheria ni miongozo inayotuongoza tu wakati kuna amani na utulivu. Kanuni kuu kwa viumbe wote ni survival of the fittest. Wewe tukanaaaa lakini hakikisha kuwa uko fit kuliko unaemtukana. Mwisho wa siku hatutaki milio ya kuomba public sympathy kwetu maana umetukana mwenyewe bila kutuomba maoni yetu.
 
Kwamba hujui Kama Ana kesi nyingine?

Halafu yeye kuonana na mawakili wake ni haki yake kisheria, kwani wewe kinakuuma nini yeye kuonana nao?
Kwani kakatazwa kuonana nao? Asichotaka ni maongezi yao kusikilizwa na maofisa wa gereza. Wanataka kupanga nini cha siri?
 
Katiba na sheria ni miongozo inayotuongoza tu wakati kuna amani na utulivu. Kanuni kuu kwa viumbe wote ni survival of the fittest. Wewe tukanaaaa lakini hakikisha kuwa uko fit kuliko unaemtukana. Mwisho wa siku hatutaki milio ya kuomba public sympathy kwetu maana umetukana mwenyewe bila kutuomba maoni yetu.
Dunia ya survival of the fittest haihitaji katiba, hiyo ni dunia ya wanyama wanaouana msituni, mkubwa anamuua mdogo kwa sababu anaweza tu, si dunia ya watu waliostaarabika.

Umechanganya madawa.
 
Gentromeni,
nakushauri endelea na praise and worship zile za kuwapanga misukule ila huku ni vipengele ndo vinaongea,,,

Kanuni ya 13 ya Uendeshaji wa Magereza ya Mwaka 1968 inaruhusu askari magereza kuwa eneo ambalo wanaweza kumuona tu mfungwa/mahabusu na mawakili wake kwa ajili ya usalama, lakini wanapaswa kukaa umbali ambao hawezi kuwasikia wanachozungumza.

Gentromeni hizi siyo zama za zidumu fikra za mwenyekiti,,
Unatindinganya mambo. Hii kesi is so special. Usiri kati ya ndugu, maragiki au mawakili wa mahabusu unaweza kuleta madhara kwa ama mahabusu, raia/wakili au usalama wa taifa.
 
Dunia ya survival of the fittest haihitaji katiba, hiyo ni dunia ya wanyama wanaouana msituni, mkubwa anamuua mdogo kwa sababu anaweza tu, si dunia ya watu waliostaarabika.

Umechanganya madawa.
Kwani Rais wa Venezuella yuko wapi?, Gadaffi na Saadam je? Palestine wana makosa gani?.

Madini na rasilimali zetu zinasombwa kwenda mabara mengine kwa kutumia kanuni ya survival of the fittest.

Vijana wetu wenye nguvu na maarifa wanafanya umanamba(cheap labours nchi za Magharibi%
 
Logical non sequitur fallacy.
 
Back
Top Bottom